2/28/2005

MAKALA MPYA YA PADRI KARUGENDO

Ninaamini kuwa waliokuwa wakitaka kumsoma Padri Karugendo wanatabasamu. Bado ziko makala zake nyingi za kuweka hapa na habari nyeti kuhusu uhusiano wake na kanisa lisilopenda mabadiliko linaloongozwa na wanaume wasiooa la Katoliki. Soma makala yake mpya iitwayo: PESA ZA KUNUNULIA KURA ZINATOKA WAPI? kwa kubonyeza hapa. Kuna makala zake nyingine katika safu yake iitwayo Kalamu ya Padri Karugendo (iliyoko mkono wa kuume hapa bloguni, shuka chini ya makala zangu na za Freddy Macha utakuta safu hiyo).

TANZANIA YAZIDI KUENDELEA

Tanzania inazidi kupiga hatua katika maendeleo ya wananchi wake. Muda sio mrefu daladala zitapigwa marufuku ili mwekezaji anayekula sahani moja na vitofali (sio vigogo tena siku hizi) aweze kuleta mabasi yake!
Hatua nyingine kubwa kimaendeleo inaonekana katika suala la mama lishe, ambao kampeni ya CCM ilidai kuwa ina fungu la fedha la kuwasaidia. Duka la kaburu la Shoprite jijini Dasalama hivi sasa linauza ugali na maharage kwa bei ya chini zaidi ya mama ntilie. Hali hii inatishia kipato cha akina mama hawa, wengi wao wakiwa wana familia kubwa zinawategemea, na hivyo kuimarisha upenzi wa wananchi wa kawaida kwa sirikali yao inayowajali sana sana kiasi cha kuwa na sera, mikakati, na kila mbinu za kuwalinda dhidi ya misukosuko ya soko huria ambayo ndio kwanza wanaionja.
Hatua ya juu kabisa ya maendeleo ambayo itafanya Tanzania kuwa ni moja ya nchi za dunia ya kwanza na pengine kuingia katika kundi la nchi tajiri duniani la G8 na kufanya kundi hilo kuwa G9 ni pale kilio na sala zangu vitakaposikiwa na mungu ambaye aliacha kuongea na wanadamu zamani sana toka alipoongea na manabii na mitume wa kwenye biblia na kurani. Mungu anayetupenda sana kiasi cha kumwacha shetani aje duniani kutushawishi ambapo baadaye tukifa atatuchoma moto wa milele...ingawa pia anasifika sana kwa huruma! Mungu huyu pia anachoma moto watoto wadogo wanaofariki kabla ya kubatizwa kwa mujibu wa teolojia ya kiluteri (msije mkasema nimetunga) kwa kuwa eti wamerithi kitu kinaitwa dhambi ya asili toka kwa Adamu na Hawa. Basi mungu huyu akisikia kilio na sala zangu kuhusu kubinafsishwa kwa ikulu na Tanzania kuwa na rais kaburu, nchi yetu itakuwa imeruka toka ulimwengu wa nne hadi wa kwanza.
Wale wanaotaka kujiunga na kampeni yangu hii tuwasiliane maana hili jambo sio la mchezo. Wenzetu wa Kenya nao ambao wamechoshwa na wazee kama Kibaki wanaweza wakaiga mfano wetu. Waamue kimoja kama sisi. Warudishe wazungu maana hawa jamaa wana akili kweli. Si mnaona nchi zao zilivyoendelea na jinsi zina "demokrasia" ya kweli? Halafu wana upendo sana. Si unaona wameanzisha mashirika kama Benki ya Dunia au Shirika la Fedha Duniani ili kutusaidia? Lazima watakuwa wameshika dini sana. Lazima. Wana upendo wa ajabu kabisa. Yaani wanaanzisha kabisa shirika linaitwa Shirika la Fedha Duniani! Jamani. Upendo ulioje.
Akina Nyerere, Dedan Kimathi, Nkrumah, Kaunda, n.k. walikosea sana walipogombea uhuru. Uhuru kitu gani. Wangeacha hawa jamaa wenye roho njema namna hii waendelee kutawala. Sitaki wala kusherehekea tena sikukuu ya uhuru. Nimegundua uhuru ilikuwa ni kosa kubwa sana. Sasa tunahitaji mashujaa wa kurudisha ukoloni. Tuwatungie nyimbo na kuwajengea masanamu ili tuwasahau kabisa wale waliotupoteza njia.
Mimi namtaka kaburu tu. Sina haja na wengine. Wakenya wanaweza kuwarudia Waingereza. Waganda nadhani wameshamkamata Mmarekani. Mimi nimeshamwahi kaburu. Asije mtu akaniingilia. Bila kumpeleka kaburu ikulu sitalala. Yaani tuwape tu mashirika na machimbo ya madini na mashamba? Hata, sikubali. Tuwape na ikulu kabisa. Ikishindikana nitakwenda hadi mlingotini Bwagamoyo kutafuta kizizi cha kuleta kaburu matata iya!

MAHOJIANO YANGU NA MREMA WA TLP

MAHOJIANO KATI YANGU NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA TANZANIA LABOUR PARTY, AUGUSTINE LYATONGA MREMA:

Ndesanjo: Jina lako nani vile?
Mrema: Agustino Lyatonga Mrema.
Ndesanjo: Agustino? Inaandikwa A-G-U-S-T-I-N-O au inaandikwa A-U-G-U-S-T-I-N-E?
Mrema: Hembu rudia...

Naamua kumwandikia kabisa. Anasoma kisha anasema kuwa jina lake ni Augustine. Nami namwambia mbona haitamkwi Agustino?

Mrema: Tuendelee na masuala ya maana yaliyokuleta hapa ndugu mwandishi.
Ndesanjo: Hili ni moja ya masuala ya maana yaliyonileta hapa. Suala hili linaitwa utumwa wa
akili. Kwanini unakuwa na jina ambalo hata kulitamka huwezi? Unadhani kuwa hili
sio suala la maana?
Mrema: Wewe umetumwa na CCM! Lazima ni shushushu wa CCM.
Ndesanjo: Hapana, nimetumwa na mizimu ya mababu zako. Wanasikitika mno. Wanatoa
machozi kila kukicha na kabla ya kwenda kulala. Wanasema
mambo unayofanya yanasikitisha sana. Kwa mfano, niambie kirefu cha jina la kile
chama ulichohamia baada ya kuondoka CCM (yaani NCCR). Wananiambia kuwa
uliingia chama chenye jina ambalo hata kusema kirefu chake ulikuwa hujui.

** Inaendelea baadaye. Nimekuonjesha utamu kidogo.

NGUVU YA UMMA NDIO HII

Watawala wa nchi fulani za Afrika ambazo sitaki kuzitaja hasa ile yenye jina linaloanzia na T wasije wakadhani kuwa mambo kama yanayotokea Lebanon hivi sasa yanatokea kwa wengine tu. Usicheze na nguvu ya umma. Hoja yangu kubwa siku za hivi karibuni imekuwa ndio hii: wananchi wana nguvu kubwa kushinda nguvu za dola, nguvu za pesa viongozi walizoiba kwa wananchi...wana nguvu kushinda hata hofu ya kifo. Nguvu yao na kauli yao inashinda kitu chochote kile.

Inachukua muda wananchi kujua nguvu waliyonayo, ila wakishajua hakuna kurudi nyuma. Tazama nguvu ya umma huko Lebanon kwa kubonyeza hapa.

BLOGU ZA SAUTI ZA HUTBA YA LOUIS FARRAKHAN

Nilijaribu kutuma kwa njia ya simu baadhi ya vipande toka kwenye hutba (uliyenipa neno hili unajijua, uko Texas) ya Louis Farrakhan wa Taifa la Waislamu. Vipande vyenyewe ni vifupi kwa sababu mbili: 1. Unapotuma ujumbe kwenye blogu kwa njia ninayotumia huwezi kutuma kwa muda mrefu.
2. Kwakuwa nilikuwa na Ndesanjo mdogo, Ukweli Macha, ambaye ana miaka miwili na nusu, kuna wakati alikuwa akitaka kuishika simu ili acheze nayo. Ilikuwa ikitokea anaitaka simu inabidi nitume na kuizima simu.

Kuna baadhi ya vipande nimeviondoa maana sauti ya Ukweli ilikuwa inasikika zaidi ya Louis Farrakhan, nami leo sikuwa na nia ya kuwasikilizisha Ukweli bali Farrakhan.

Baadaye nitaandika kwa ufupi aliyoyasema. Hata hivyo, sikiliza vipande vichache nilivyoviweka.

2/27/2005

FARRAKHAN: MAREKANI NI ZAIDI YA SODOMA NA GOMORA

this is an audio post - click to play

FARRAKHAN: MUISLAMU NI NDUGU YANGU, ILA MTU MWEUSI NI DAMU YANGU

this is an audio post - click to play

FARRAKHAN: UISLAMU DINI YA CHUKI, UKRISTO DINI YA UPENDO?

this is an audio post - click to play

FARRAKHAN ANAENDELEA

this is an audio post - click to play

FARRAKHAN: MTUME ALIYETABIRIWA ANAYEFANANA NA MUSA SIO MUHAMMAD

this is an audio post - click to play

FARRAKHAN: 7+0=7, 5+2=7, 6+1=7

this is an audio post - click to play

FARRAKHAN: ITIKADI YA UTENGANO YA TAIFA LA WAISLAMU NI KAMA YA YESU

this is an audio post - click to play

FARRAKHAN: YESU ALISEMA ATATUMA MSAIDIZI: UNAMJUA?

this is an audio post - click to play

FARRAKHAN: HUWEZI KUUA AKILI WALA ROHO

this is an audio post - click to play

FARRAKHAN: FAKE JEWS, FAKE MUSLIMS, FAKE CHRISTIANS!

this is an audio post - click to play

FARRAKHAN: MABEPARI NI WANYONYA DAMU

this is an audio post - click to play

LOUIS FARRAKHAN AKITOA SALAMU

this is an audio post - click to play

MCHUNGAJI WA KIPENTEKOSTE AKIONGEA KABLA YA FARRAKHAN

this is an audio post - click to play

TUNASUBIRI HUTBA YA FARRAKHAN

this is an audio post - click to play

WASANII WA JABALI AFRIKA NA VITUKO VYA POLISI WA AFRIKA

this is an audio post - click to play

JIFUNZE KISWAHILI

Photo copier: Mashine ya Kurudufu

WANABLOGU WANAOINGIA MITINI

Kumbe rafiki yangu wa karibu aliingia kwenye ulimwengu wa blogu na kutoweka bila hata mimi kujua. Kaka yangu, Walter, kanipatia habari hii na kiunganishi cha blogu ya Ras Onaeli Mandambi (bado unaendesha kipindi cha Rege Radio One??). Blogu yake hii hapa.

HIVI BLOGU ZINA MWISHO?

Je wanablogu huwa na blogu zao maisha yao yote au kuna wanaoishia njiani? Agana na mwanablogu huyu toka Kenya anayeishi ughaibuni. Kongoli hapa.

MAREJEO YA KITABU KUHUSU MWALIMU NYERERE

Soma marejeo ya Idrian Resnick ya kitabu cha mkusanyiko wa insha kuhusu Mwalimu Nyerere kilichohaririwa na Colin Legum na Geoffrey Mmari. Kitabu kinaitwa Mwalimu: The Influence of Nyerere. Bonyeza hapa.

Nchi ya Liberia ilipata "uhuru" mwaka 1847. Neno "Liberia" linamaanisha "nchi ya watu huru." Mwanzoni nchi hii ilipokaliwa na Wareno iliitwa Pwani ya Nafaka/Punje. Mji mkuu wa Liberia ulipewa jina lake, Monrovia, kutokana na jina la aliyekuwa rais wa Marekani na rais wa chama kilichokuwa kikiendesha kampeni ya kuhamisha waafrika weusi wa Marekani waliokuwa wameachiwa toka katika makucha ya utumwa. Rais huyo aliitwa James Monroe na chama hicho kiliitwa America Colonization Society. Idadi ya wahamiaji wa kwanza, waliojulikana kama Americo-Americans, ilikuwa ni 86. Toka mwaka 1861 hadi 1847, watumwa walioachiwa huru waliohamia Liberia walipata 13,000. Jeshi la majini la Marekani liliongoza juhudi za mikataba ya uhusiano mwema kati ya wahamiaji na wenyeji. Watu wengi hudhani kuwa Waafrika Weusi toka Marekani walipohamia nchi hiyo, hakukuwa na watu. Kulikuwa na wahamiaji walitoka sehemu mbalimbali kama Mali, Ghana, Sudan, n.k. Wahamiaji walijitofautisha na wenyeji kwa kutumia neno "Mr" kwa wanaume, na walishika sehemu zote muhimu za uongozi. Rais wa kwanza wa nchi hiyo, Joseph Jenkins Roberts alizaliwa nchini Marekani. Rais wa kwanza mwenyeji toka makabila ya wenyeji (ambao hawakuhamia toka Marekani) alikuwa ni Sajenti Meja Samuel Doe aliyechukua madaraka kwa nguvu mwaka 1980.

MALCOLM X ASEMA...

"Our people have made the mistake of confusing the methods with the objectives. As long as we agree on the objectives, we should never fall out with each just because we believe in different methods or tactics or strategy...." -- El Hajj Malik El Shabazz (Malcolm X)

2/26/2005

MHUBIRI LOUIS FARRAKHAN NI HAPO KESHO (27/2/2005)

Wale waliopanga kumsikiliza mhubiri na kiongozi wa kundi la Taifa la Waislamu, mchungaji Louis Farrakhan, msisahau kuwa ni kesho. Kama unafuatilia kwa njia ya satelaiti, nenda hapa ili ujue utakapokwenda kutazama (kutegemea na ulipo: Marekani, Uingereza, Karibiani, n.k.). Kama ulipo hakuna pa kutazama, hotuba yake itaonyeshwa pia kwa njia ya urushaji matangazo kwa intaneti (webukasiti/webcast). Kongoli hapa na hapa.

JAMAA WA RESEARCH ICT AFRICA dot NET

Kwa wale wanaofuatilia masuala ya teknolojia mpya na maendeleo barani Afrika. Bonyeza hapa.

UKIENDA NCHI ZA WATU FUNGA MDOMO!

Inaelekea kuwa rais wa Botswana, Festus Mogae, anatuambia kuwa ukienda nchi za watu ukaona mabaya yanatendeka usiseme. Kaa kimya. Kongoli hapa uone yaliyompata Profesa wa Chuo Kikuu cha Botswana, Kenneth Good. Soma hapa waliyosema viongozi wa kanisa huko Botswana kuhusu adhabu aliyopewa Profesa Good na rais wa nchi hiyo. Lakini pamoja na kitisho toka kwa serikali ya Mogae, Profesa Good hakufunga mdomo na hivyo kushangiliwa kama shujaa. Kongoli hapa.

2/25/2005

BONGO FLAVA na DANSI

Usiwe unasahau kufuatilia bongo flava kwa jamaa wa Mzibonet (hapa), mtembelee Balozi Dola, pia BongoXplosion (hapa)
Ukitaka mambo ya dansi nenda Bongo Dansi (hapa)

HADITHI MPYA TOKA KWA FREDDY MACHA

Freddy Macha leo kaja na hadithi iitwayo Mzee Umombo. Hadithi hii iko katika mkusanyiko wake utakaochapwa kitabuni nchini Tanzania hivi karibuni uitwao Mpe Maneno Yake. Hadithi za Freddy zinaandikwa kwa staili ya aina yake: maudhui, lugha, lugha ya picha na vionjo vingine vya kifasihi vinafinyangwa kama tonge la ugali wa saa sita mchana siku ile ambayo una njaa sana. Nenda katika kona yake iliyoko upande wa kuume chini ya makala zangu.

GROWING UP X: KITABU CHA BINTI WA MALCOLM X

Ilyasah Shabazz, mmoja wa mabinti sita (Attallah,QuBilah, Ilyasah, Gamilah, Malaak, Malikah ) wa shujaa Malcolm X, ana kitabu ambacho wanaoweza kukipata (maktaba, maduka ya vitabu, amazon.com, marafiki, n.k.) ni kizuri cha kusoma. Kinaitwa Growing Up X.

PADRI KARUGENDO AJA NA: UISLAMU NA UKRISTO NDIO TATIZO TANZANIA!

Sasa ndio jua linaanza kuchomoza. Padri Karugendo ana makala mbili nzuri sana katika safu yake iitwayo Kalamu Ya Padri Karugendo (ambayo iko chini ya makala za Freddy Macha, mkono wa kuume wa blogu hii). Ukisoma makala zake hizi utazidi kujua kwanini kanisa lisilopenda mabadiliko, kanisa lisiloambilika la Katoliki la Kirumi haliwataki watu kama Karugendo. Mimi nami nimeingiwa na mori, ninaanda makala juu ya kanisa hili linaloongozwa na wazee wanaojifanya kuwa wanaishi maisha ya useja. Wazee wasio na wake. Moja ya makala yake inaitwa: Kanisa Sasa Liongozwe na Wanawake.
Makala hii ni kinyume kabisa na kanuni za kanisa katoliki zilizotungwa na wanadamu wenye dhambi pengine kushinda hata mimi na wewe.
Makala nyingine ambayo inatisha, hasa ukichukulia kuwa imeandikwa na Padri, inaitwa: Adui wa Tanzania: Uislamu na Ukristo!

TUBINAFSISHE IKULU!

Kwanza kabisa kwa wale ambao kiswahili kipya kinawapiga chenga: UBINAFSISHAJI = PRIVATIZATION
***************************************++++*****************************************
Nimeamua kabisa kuandika makala nzima juu ya mapendekezo yangu matatu ya nani awe rais wa Tanzania baada ya walaji walioko sasa hivi kumaliza kipindi chao mwishoni mwa mwaka huu. Moja ya mapendekezo yangu ni kubinafsisha ikulu. Kubinafsisha urais. Hili kuna watu wametaka ufafanuzi. Kwakuwa makala yenyewe haijatoka bado nchini Tanzania (hadi jumapili hii), sitaweza kuiweka hapa ukumbini. Ila hoja yangu kuu katika hili ni hii: tukishindwa kuendesha kiwanda tunafanya nini? TUNABINAFSISHA. Tukishindwa kuendesha mabenki tunafanya nini? TUNATABINAFSISHA. Tukishindwa kuendesha migodi (hata ile ambayo madini yake hayana ushindani wowote maana yanapatikana tu Tanzania kama vile Tanzanite!), tunafanya nini? TUNABINAFSISHA. Tukishindwa kuendesha viwanda tunafanya nini? TUNABINAFSISHA. Tukishindwa kuendesha TANESCO tunafanya nini? Tunaagiza uongozi mpya toka nje ya nchi.
Je tukishindwa kuendesha nchi tufanye nini? Tubinafsishe uongozi. Tubinafsishe ikulu. Tuwape wanaoweza kuendesha viwanda vyetu, mabenki yetu, mashamba yetu, migodi yetu (hasa wale wanaopeleka makontena ya mchanga Japani), n.k. Tuwape. Kama tumeshindwa kuendesha kiwanda cha nguo au benki au biashara ya madini ya Tanzanite yasiyopatikana nchi yoyote ile (kwahiyo hatuwezi kulalamikia ushindani), TUTAWEZAJE KUENDESHA NCHI?
Suala hapa ni nani wa kumpa. Mzungu yupi poa zaidi. Kaburu (mbaye anaitwa mwekezaji siku hizi)? Muingereza? Mjeremani? Mmarekani? Tumpe nani? Hili ndio bado linaniumiza kichwa.

MRADI WA NYARAKA ZA INTANETI (INTERNET ARCHIVE)

Huu mradi wa nyaraka za intaneti una mambo chungu nzima. Kwa mfano, kuna ule mradi wa vitabu Milioni Moja, mradi wa Gutenberg, n.k. Nyaraka hizi ni kwa ajili ya mtu yeyote na bure kabisa. Pia kuna maonyesho ya wanamuziki na bendi mbalimbali zaidi ya 20,000. Uhondo wenyewe nenda kwenye tovuti yenyewe ya mradi uitwao Internet Archive.

SIMU ZA MKONO, UJUMBE WA SIMU ZA MKONO N.K

Hii ni kwa watu wanaofuatilia yanayojiri katika teknolojia ya simu za mkono (mobile phones). Utaona, kwa mfano, wanafunzi wanavyotumia ujumbe wa simu za mkono (sms) kuibia mitihani. Au watu wanavyonunua kadi za umeme za "luku" kupitia simu hizo, au kutafuta njia wanapopotea kwa simu za mkono, pia waandamanaji wanazitumia ili kuweza kuwapiga chenga polisi (badala ya kutangaza kupitia vyombo vya habari juu ya maandamano, wanaoandamana wanatumia ujumbe kupitia simu za mkono ambapo polisi wanashtukia watu wamejazana "viwanja vya jangwani), huko Finland ukibisha hodi kwa mtu kama hayuko nyumbani simu yake italia na ataweza kuongea nawe kupitia kidude kilichoko kwenye lango kuu (getini), n.k.
Nenda kwenye tovuti ya textually.org

2/24/2005

AFRICAN SCIENCE ACADEMIES

Misaada kama hii huwa ni vigumu kujua kama inatolewa kwa nia nzuri au ni yale yale ya Mangungo wa Msovero. Mtoto wa nyoka si nyoka, au kuna wakati anakuwa mjusi?
Soma hapa.

2/23/2005

KILICHOMTIA PADRI KARUGENDO MATATANI NA KANISA KATOLIKI

Nimeweka mada kuhusu Ukimwi aliyoandika Padr Karugendo kwa ajili ya mkutano wa kitaifa wa Ukimwi mjini Arusha mwaka 2002. Aliyoandika humu ndio moja ya chanzo cha kanisa lisilopenda mabadiliko hata kidogo, kanisa katoliki la kirumi (roman catholic) (ambalo sijui linafanya nini Afrika!), kumfukuza kazi. Nenda kwenye kona ya Padri huyu mchambuzi, na mpenda mabadiliko anayesumbua akili za maaskofu wa dini zote Tanzania na viongozi wa sirikali, inayoitwa Kalamu ya Padri Karugendo. Mada yake hiyo ya Ukimwi inaitwa: CHANGE THE WORLD BY CHANGING ME.

Nitaendelea kutoa maandiko yake ambayo yamemtia hatatani na uongozi wa kanisa hili la katoliki. Na pia kutakuwa na habari za kina kuhusu mgogoro wake na kanisa hili linalomtaka aache kutii dhamira yake na kuendeleza uongo na unafiki kwa jina la mungu.

FREDDY MACHA AJA NA HADITHI

Soma hadithi ya Freddy Macha kwenye kona yake ndani ya blogu hii. Hadithi hii inaitwa JE NIMEPENDEZA? Hadithi hii iko katika mkusanyiko wa hadithi zake zitakazochapwa karibuni nchini Tanzania katika kitabu kipya kiitwacho MPE MANENO YAKE.

NANI ANAFAA KUWA RAIS WA TANZANIA?

Nimeulizwa hili swali mara elfeni: Ndesanjo, unadhani nani anafaa kuwa rais wa Tanzania?
Nina majibu kadhaa ya swali hili.
Jibu la kwanza: Kwakuwa Watanzania wengi wanajifanya kuwa ni waumini wa dini hizi mbili za kuja, uislamu na ukristo, naona basi tuwe na marais wawili. Tuwe na shehe mkuu na askofu mkuu maana watu hawa inadaiwa kuwa wanaongozwa na mungu. Nani zaidi ya watumishi wa mungu wenye mawasiliano ya moja kwa moja na mungu wanaoweza kuongoza taifa ambalo linaweza kuelezewa kuwa ni sawa na merikebu isiyo na nahodha? Kwahiyo tuwe na hawa "watumishi" wa mungu kama marais wetu maana kwa maneno mengine, mungu wa ukristo na uislamu ndiye atakuwa rais wetu. Sina uhakika kama mungu wa dini hizi mbili za kuja ni mmoja au ni wawili tofauti, tusije tukawa kama tuna marais wawili! Nadhani dini hizi mbili zina miungu tofauti maana mungu wa dini moja anasema kula nguruwe ni sawa, na wa dini nyingine anasema sio sawa. Mungu wa dini hii anasema kuwa Yeshua/Isa (Yesu) alisulubiwa, wa dini nyingine anasema hakusukulubiwa. Wa dini hii anasema kuna kitu kinaitwa utatu na mungu wa dini nyingine ambaye hajui kichagga au kisukuma bali kiarabu anasema kuwa hakuna utatu...dhana ya utatu ni shirk. Mungu wa dini hii anasema kuwa biblia ndio kitabu chenye ujumbe wake, na wa dini hii anasema maneno yake yako kwenye zaburi, torati, manabii, injili, na kurani! Nadhani hawa ni miungu wawili tofauti. Kama sio, basi atakuwa anasahausahau sana!
Narudi kwenye urais Tanzania:
Hili ni jibu la pili kuhusu nani anafaa kuwa rais wa nchi yetu (kama bado tuna nchi!): Naona ili "tuendelee" kama wenzetu waliokuja zamani na kutupa biblia kisha wakatuambia tufumbe macho kusali, na tulipofumbua tukakuta tumebaki na biblia na wao wamechukua ardhi, maliasili, ndugu zetu (watumwa) na nafsi zetu... na ili kuendana na mtazamo kuwa ubinafsishaji ndio njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na HURU, tubinafsishe kiti cha urais! Kwa kuwa tunabinafsisha viwanda, migodi, mabenki, mashamba, n.k kwa kuwa tumeshindwa kuendesha wenyewe, kwanini tusibinafsishe ikulu kutokana na ukweli kuwa tumeshindwa kuendesha nchi yetu?
Ndio, tuzunguke huku na huko kwa wazungu, kutafuta mzungu atakayeshinda tenda ya kuwa mnyapara wetu. Tutakachofanya ni kumpaka masizi ili ngozi yake ifanane na sisi kama walivyo watawala wetu wanaoitwa "viongozi" ambao ngozi zao ni kama zetu ila akili na nafsi zao sio. Wananikumbusha kitabu cha Frantz Fanon cha Black Skin, White Mask.
Aah, kuna jibu la tatu ambalo limenijia akilini sasa hivi: Kwanini tusimwombe rais Joji Kichaka wa Marekani ambaye pia ni rais wa Afghanistani na Iraki aongeze Tanzania katika nchi anazoongoza??????
Nyie mnasemaje?

Siku ya hukumu (kwa wale wanaoamini kuwa kuna siku kama hii) utaulizwa, "Nilikuja nikiwa na ugonjwa wa ajabu, mbona hukunisaidia?" Nenda hapa utajua ninazungumzia nini.

WAGOMBEA URAIS WA MAISHA!

Niliwahi kuandika juu ya "wagombea urais wa maisha" nchini Tanzania. Kama hamkunielewa nilichokuwa ninasema soma habari hii hapa. Watu kama hawa wakipata urais wanaweza kujitangaza kuwa wafalme!

BONGO FLAVA NA MITIKASI MINGINE

Usiwe unasahau kutembelea tovuti ya Dar Hotwire ili kupata mpya kuhusu mambo mbalimbali Tanzania. Zaidi ni kuwa utakuwa unasikiliza na kutazama video za wanamuziki mbalimbali wa Tanzania. Utakula miziki hadi mwenyewe unyooshe mikono. Huamini? kongoli hapa ujionee na kujisikilizia.
**Binti Mtandao ulinishtua siku nyingi juu ya hawa jamaa.

2/21/2005

MAKALA MPYA YA KARUGENDO

Soma makala nyingine ya Padri Karugendo iitwayo NANI ADUI WA UMMA? Iko kwenye kona iitwayo KALAMU YA PADRI KARUGENDO. Kona hiyo iko upande wa kuume, chini ya makala zangu na za Freddy Macha. Naamini wote ambao mmekuwa mkiulizia makala zake mnasuuzika na roho zenu. Na huo ndio mwanzo maana nina rundo la makala, sijui kama mtazimaliza mwaka huu! Kazi kwenu. Safari ya kujikomboa kifikra na nafsi ndio kwanza inaanza.
Haya, nakwenda kulala. Nilipanga kufanya mambo zaidi lakini macho yamekataa katu katu.

MALCOLM X KWA MDOMO WAKE

Malcolm X kwa mdomo wake mwenyewe. Hapa. Ukifika hapo kwenye tovuti bonyeza panaposema "multimedia."

MANENO YA MALCOLM X

Ni miaka 40 toka kuuawa kwa shujaa mtetezi wa haki na usawa wa binadamu, Malcolm X. Haya ni baadhi ya maneno toka kinywani mwake:

"The Negro revolution is controlled by foxy white liberals, by the Government itself. But the Black Revolution is controlled only by God." Speech, Dec. 1, 1963, New York City.

"I for one believe that if you give people a thorough understanding of what confronts them and the basic causes that produce it, they'll create their own program, and when the people create a program, you get action."

"Concerning nonviolence, it is criminal to teach a man not to defend himself when he is the constant victim of brutal attacks."

"We are nonviolent with people who are nonviolent with us."

"If violence is wrong in America, violence is wrong abroad. If it is wrong to be violent defending black women and black children and black babies and black men, then it is wrong for America to draft us, and make us violent abroad in defense of her. And if it is right for America to draft us, and teach us how to be violent in defense of her, then it is right for you and me to do whatever is necessary to defend our own people right here in this country." Speech, Nov. 1963, New York City

CHECHE TOKA KINYWANI KWA MALCOLM X

Kwa ajili ya kumbukumbu za miaka 40 toka maadui zetu wamuue kwa risasi Malcolm X, tafadhali nenda hapa umsikilize mwenyewe Malcolm X. Au tovuti hii kwa mambo zaidi juu yake.

MIAKA 40 TOKA KUUAWA KWA MWANAUME WA SHOKA MALCOLM X

Leo ni mwanzo wa kumbukumbu duniani kote kwa ajili ya miaka 40 toka kuuawa kwa mwanaume wa shoka, mhubiri, mtetezi wa haki za watu weusi, Malcolm X. Kwa kuanza soma habari hii.

MAKALA MPYA YA PADRI KARUGENDO

Kuna watu walikaribia kunikamata koo kwa kuchelewa kupandisha makala za Padri Privatus Karugendo. Kulikuwa na tatizo kwenye blogu hii ambapo upande wenye makala ulikuwa unatoweka mara tu unapoingia. Sasa kila kitu kimerekebishwa. Nimeweka makala mpya ya Padri Karugendo, inaitwa: YU WAPI DESMOND TUTU WA TANZANIA?
Padri Karugendo anaandika makala zake kwa ajili ya gazeti la Rai nchini kila alhamisi.

Pia makala yangu mpya ambayo ilikuwa haisomeki sasa inasomeka. Nenda kwenye kona yangu uisome. Inaitwa: KAMA UNAPENDA UTAMADUNI MBONA UNAVAA NGUO?

Wale wapenzi wa Freddy Macha nitaweka makala zake mbili baadaye, leo usiku.

2/20/2005

BUSH/JOJI KICHAKA NA "BANGI NIBANGUE"

Joji Kichaka aliwahi kupuliza lile jani huku akisema, "Bangi nibangue..." Sina uhakika kama ameacha kupuliza hilo jani. Soma habari yenyewe hapa.

NDESANJO NA TAIFA LA WAISLAMU

Napenda kutoa ufafanuzi kidogo. Mimi sio mfuasi wa Taifa la Waislamu ingawa ninafuatilia kwa karibu sana mambo yao. Ninafanya hivi kwasababu za kitaaluma na sio kidini. Na ninapenda Waafrika wengine wajue kwa undani juu ya vuguvugu hili la waislamu weusi. Kuna mambo anayosema Farrakhan ambayo ninakubaliana naye, ila kuna mambo ambayo sikubaliani naye. Kwa mfano, sikubaliani naye kuwa dini ambayo mungu alimpa mwanadamu baada ya kumuumba ni uislamu. Taifa la Waislamu wanaamini kuwa mungu alipomuumba mwanadamu hakumwacha bila dini. Na dini aliyompa, dini ya kwanza ya mwanadamu, dini ya kweli, dini ya asili ni uislamu. Wakifikia kwenye kipengele hiki mimi huziba masikio!

POROJO ZA KIJIWENI

Nakumbuka ile siku nilipofika Chicago kwa mara ya kwanza. Miaka miwili iliyopita. Sikupapenda hata kidogo. Mbio sana. Shimeshime. Utu hakuna. Hakuna wa kumsimamisha kumuuliza saa.
Chicago kuna kila kitu. Kuna utajiri uliokithiri na kuna ufukara unaokutoa machozi. Kuna baadhi ya mitaa ukifika unajiona kama uko sokoni Kariakoo. Tena kule shimoni. Na mingine ukienda lazima uwe na roho ya paka. Silaha nje nje. Vibaka kama utitiri. Michoro ya majina na alama za magenge kila ukuta. Milio ya ving'ora vya polisi na risasi kila saa.
Ninapokuwa katika mitaa kama hii huwa najiuliza, "Anayeita Marekani ni ulimwengu wa kwanza anamaanisha kuwa mitaa hii nayo ni ulimwengu huo wa kwanza?" Unajua kuna Marekani nyingi sana. Mapicha ya kwenye magazeti kama Ebony, sinema, filamu za muziki, n.k hupotosha sana kwa kutufanya tuamini kuwa Marekani yote inang'ara. We! Tembea uone.

Naanza kuhisi kuzeeka maana nimeanza kuchukia sana miji mikubwa, majengo makubwa ya orofa, magari yanayokwenda kwa kasi, n.k. Napenda miji midogo yenye mandhari mchanganyiko wa mji na kijiji. Napenda miji-vijiji. Nadhani kwakuwa nimezaliwa kijijini na kwenda shule mjini. Napenda miji yenye miti, mito, nyumba za ukubwa wa wastani, mashamba, milima, bustani, wakulima, ng'ombe, kuku, mbuzi, bata, masoko yenye mazao ya wakulima wadogowadogo, n.k.

Bado niko Chicago. Basi, si unajua wale vijana wanaouzia abiria kwenye mabasi maji, mikate, magazeti, na bidha nyingine pale Bongo? Kuna sehemu kule Chicago namna hiyo. Ninapita hivi mara moyo ukanidunda du! Nikashtuka, ala! Machinga mpaka huku? Jamaa walikuwa wanauzia abiria na watu wengine maji baridi. Nikawasemesha kiswahili maana nilidhani huenda wametoka Bongo. Wakanikodolea macho. Sasa sijui walijikausha au labda ni machinga wa hapa!
Ngoja nibadili usemi. Nilisema sipendi miji mikubwa. Nadhani mji wa Seattle nitautoa katika kauli hiyo. Mji poa mno mno. Seattle. Seattle. Mji maridai. Watu wastaarabu. Ajabu sana ukisikia honi za magari. Karibu kila mtu anatembea barabarani akinywa kahawa. Huu ni mji ambao kila dakika unaweza ukafirikia kuna tukio la kufurahisha linatokea au kuna sherehe fulani. Nikifika pale huwa napoteza muda kwenye maduka ya vitabu, hasa duka la Left Bank Books na pia lazima nitembelea soko la "kariakoo" la Seattle la Pike Place Market ambapo zaidi ya kutazama wauza samaki ambao huwa ni kiburudisho kwa watu wengi kwa jinsi wanavyokata kwa haraka na kurushiana minofu ya samaki wakubwa kama gari aina ya Anglia (sijui kama mnafahamu gari hili la zamani sana!) kwa staili ya pekee, huwa napenda sana kutazama watumbuizaji kadhaa ambao wametapakaa sokoni hapo. Zaidi napenda kumuona msanii huyu hapa aitwaye Artis au Spoonman, ambaye alinipa CD yake mwaka jana baada ya kukaa siku nzima nikimsikiliza! Artis ni mwanamuziki anayepiga muziki kwa kugonganisha vijiko! Muziki anaoutengeneza ukiusikia huwezi amini masikio yako. Ukifika Seattle lazima umtafute Spoonman. Mwingine ambaye huwa lazima nimtafute kila nikienda sokono hapo ni mwanaharakati, mpiga gitaa, na muimbaji Jim Page. Huyu bwana kwangu mimi sio mwimbaji kama watu wanavyomwita bali ni msimulizi wa hadithi. Nyimbo zake ukisikiliza anaongea nawe kama anakusimilia kisa fulani. Na anaandika mashairi acha mchezo. Mtazame hapa.
Nikukumbushe kuwa mji wa Seattle unakumbukwa kutokana na watu waliozaliwa, kuishi, au kufia hapo kama vile Jimmi Hendrix (mlami mweusi aliyemaliza kabisa kupiga gitaa...hakuna kitu kipya cha kupiga tena kwenye gitaa baada ya mlami huyu!), Bruce Lee, Kurt Cobain wa kundi la Nirvana.
New York... kule ndio hata nikiambiwa nikaishi bure siendi. Kutembelea sawa. Sio kukaa.
Kila mtu yuko nyuma dakika tano, kwahiyo kila mmoja ana haraka ya kuwahi mahali. Amechelewa, hivyo mpishe haraka apite.
Kila mtu anataka kukuuzia kitu.
Kila mtu anataka kukuomba senti za sigara.
Kila mtu anataka uingize mkono mfukono. Anataka kukutoa kitu kidogo. Ukikuta mwanamuziki au mchekeshaji anatumbuiza usisimame na kutazama kama huna hela ya kumpa. Hakuna onyesho la bure ndugu yangu. Unataka akale polisi?

Ukitembelea Harlem, kuna mitaa fulani pale unaweza kudhani kuwa uko Dakar, Senegal kwa jinsi walivyojazana Wasenegali. Hii ndio ile mitaa ambayo kabla mwanamuziki hajatoa albamu yake rasmi, jamaa wanakuwa wameshaanza kuiuza! Wanatoa wapi? Usiniulize.
Nikienda New York, kijiwe changu huwa ni Nuyorican Poets Cafe. Kongoli hapa. Au unaweza kunikuta katika duka hili liitwalo Hue-Man Bookstore and Cafe. Unajua kama unanitafuta popote pale nilipo dunia hii, usisumbuke sana nenda kwenye maduka ya vitabu utanikuta humo. Ndio sebuleni kwangu. Pengine ninapopapenda nikiwa upande huo wa New York ni Schomburg Center for the Study of Black Culture. Nenda hapa.
Hiyo ni New York. Palipotokea yale maafa ya ile tarehe inayofanana na namba ya kuita mapolisi: 911 (yaani tare tisa mwezi wa kumi na moja.) Hivi wale jamaa waliopeleka yale madege kwenye lile jengo walichagua siku hiyo kutokana na tarehe hiyo kufanana na namba ya mapolisi au?
New York ndipo kijana Amadou Diallo toka Afrika Magharibi aliuawa na polisi kwa risasi 41 akiwa hana kosa lolote. Risasi 41! Mwanamuziki nimpendaye Bruce Springsteen alitunga wimbo uitwao American Skin (41 shots). Ukienda hapa unaweza kumtazama video ya Bruce akiimba wimbo huu na pia kusoma mashairi ya risasi 41. Ukifika katika tovuti hiyo, shuka chini hadi uone palipoandikwa AMERICAN SKIN VIDEO. Bonyeza hapo. Usisahau kufuatilia mashairi ya wimbo huo katika tovuti hiyo.
Nimekumbuka pia kuwa Jean Wycleaf aliyekuwa katika kundi la Fugees na Lauryn Hill alimuimba pia Diallo katika albamu yake ya Ecleftic. Soma mashairi ya wimbo huo uitwao Diallo hapa, ambao alimjumuisha Yossou N'dour na MB^2.
Pale Toledo, Ohio, nilipoishi miaka miwili sijui jinsi ya kupaelezea kwa kina. Iko siku. Leo nitagusia mambo mawili matatu: Mji wa Toledo ni mji dada wa mji wa Tanga. Kuna mahusiano makubwa ya shughuli za maendeleo kati ya miji hii miwili. Kwa mfano, kulikuwa na gari la zimamoto toka Toledo kwa mji wa Tanga kama zawadi. Sijui kama limefika. Pia shirika la Great Lakes Consortium , lililoko Toledo, lina miradi mbalimbali kupitia serikali ya Marekani na mpango wake wa AGOA wa "kusaidia" wafanyabiashara wadogo ili kuweza kupata masoko hapa Marekani. Mwaka jana wafanyabiashara kadhaa toka Tanzania walitembelea Toledo.
Pale Toledo kilichokuwa kinanitisha ni wizi wa kutumia silaha. Kila taarifa ya habari jioni unasikia fulani na fulani wamekamatwa wakiiba kutumia silaha. Fulani na fulani wameuawa na majangili. Duka hili na na kituo kile cha petroli (hapa petroli wanaita gesi!) vimeingiliwa na majambazi. Nilitishika zaidi wakati sheria ilipopitishwa ya kuruhusu wakazi wa mji ule kutembea na silaha zao mitaani. Hii nchi ambayo inajivuna kuwa mfumo wake wa sheria na utawala umejengwa juu ya amri kumi, ambazo Musa alidai kupewa na mungu, sijui kwanini inakuwa na upenzi mkubwa namna hii wa kubeba silaha badala ya biblia! Katiba ya Marekani inatamka wazi kuwa ni haki ya kikatiba kwa raia kubeba silaha. Ni haki ya kikatiba pia kwa raia kuunda majeshi yao binafsi. Na hayo majeshi yapo. Hili tutazungumzia siku moja.
Pale Toledo kuna mitaa ambayo barabara zake zinanikumbusha barabara za Tabata miaka ya nyuma (kabla hazijatengenezwa kama sasa.) Halafu watu pale washamba sana, hawajui dunia inakwenda wapi au imetoka wapi. Kila wanachoona kwenye luninga wanaamini. Ukiwatajia Afrika wanachoona ni vita, njaa, ukimwi, n.k. Nimekutana pale na watu wana mapengo, kwa kutokuwa na bima ya afya, wananiuliza juu ya tabu za Afrika, nawaambia, "Nilipotoka hakuna mtu ninayemjua mwenye umri kama wako ambaye ni kibogoyo!" Wakiongelea juu ya Afrika kuwa nyuma kiteknolojia, huwa ninawauliza mara ya kwanza kuwa na anuani ya barua pepe. Wengi hudhani kuwa ninadanganya ninapowaambia kuwa nilikuwa na anuani toka mwaka 1996-97, wakati wengi wao walikuwa wakisikia "email" kwenye bomba! Na situmii mfano huu kwakuwa nadhani kuwa hicho ni kipimo bora cha maendeleo ya teknolojia au kudhani kuwa maendeleo ya teknolojia ni sawa na maendeleo ya watu, hapana. Nataka kuwaumiza vichwa kwa kuwaonyesha kuwa mtazamo wao juu ya Afrika ni finyu sana. Wanaongelea juu ya sisi kuwa nyuma kiteknolojia wakati bila nambari 1 hadi 9 wasingekuwa na teknolojia waliyonayo leo. Na nambari hizi ni mababu zangu ndio waliowapa! Maaluni kabisa!

Hiyo ni tisa, kumi...nina hamu sana ya ugali kwa kisamvu cha nazi kwa mama ntilie, ndizi za mama pale Moshi, mtori kwa sana, chipsi mayai "zikaushe na weka kila kitu pamoja na ukwaju"(pale American Chipsi kinondoni au mitaa ya Kariakoo mida ya saa tatu usiku), juisi ya miwa pale Kariakoo au Buguruni kwa Wapemba, mbege ya Moshi, wali wa nazi kwa maharage kwa mama lishe....acha jamani. Nchi yetu...acheni tu. Tatizo letu ni hawa "viongozi" wetu wanaouza kila kitu kama vile wameishiwa akili.
Mwisho wa gumzo. Umechoka? Niendelee nisiendelee? Wanaotaka niendelee wanyooshe vidole...

KISA KIFUPI: DUNIA IMEJAA WENDAWAZIMU

Maneno yaliyomtoka ni kama ya yule mwanamke asiye na makazi niliyekutana naye hivi majuzi. Alipomaliza kuongea nilijiuliza imekuwaje wakaniambia jambo hilo hilo? Wanafahamiana?
Yule mama ni mzungumzaji. Niliongea naye kwa dakika chache na toka siku ile sijamuona tena. Huyu bwana anapenda tu kutabasamu kwa chati. Akikusalimu, anakusalimu kwa haraka wala hakutazami machoni. Ukimsalimu, anakujibu kwa mkato. Inadaiwa watu wa kabila lake wako hivyo. Katoka kabila la wahindi wa asili ya Marekani la Navaho. Toka nimetambulishwa kwake wiki kadhaa zilizopita hajasema neno.
Lakini jana kafungua mdomo. Maneno yale yale ya yule mama: Dunia imepata wendawazimu. Kila mtu kawa kichaa. Tumepandwa na wazimu. Tumerukwa na akili. Nati zimechomoka. Walimwengu tunaokota makopo bila kujijua.
Kweli? Kwanini anasema hivyo? Nilimuuliza.
Sikiliza taarifa za habari. Alinijibu, akaendelea: Hivi ukitazama luninga unaona chochote siku hizi? Damu si imechafua kioo? Hivi risasi hazijawapata watangazaji?
Aliuliza huku akinitazama kama vile anasubiri jibu. Nilitumia nguvu zangu zote kujizuia kucheka. Sio kumcheka. Kujicheka mimi na walimwengu wenzangu lakini sababu hasa sijui.
Akaniambia: Usipende kuganda mbele ya luninga. Utakuwa mjinga. Kwanza ukitazama sana kuna siku bomu litakosa njia likuangukie sebuleni.
Nilijiuliza kama anayosema ni mafumbo au kuna tatizo akilini mwake.
Kisha akauliza swali jingine. Yale mengine sijamjibu: Hivi hawa jamaa bado wako Iraki au wameenda kwingine?
Alikaa kimya kidogo akinitazama kama vile hanioni, akaendelea: Bila bangi mimi nami ningekuwa kichaa tayari kama ninyi. Sijui mnaishije kwenye dunia yenu hii bila bangi!
Alitikisa kichwa huku akiondoka.
Hiyo ilikuwa ni jana. Leo hajasema lolote. Nikimtazama, anatazama pembeni. Nikimsalimu, anajibu kwa mkato. Nasikia ameacha kusoma magazeti, kusikiliza redio, au kutazama luninga.

JOJI KICHAKA ALISEMA NINI SIRINI?

Kuna jamaa alimrekodi Joji Kichaka siku za nyuma kabla hajaiba kura kuwa rais wa Marekani. Soma hapa aliyoyasema.

JE MHUBIRI LOUIS FARRAKHAN ANACHUKIA WAYAHUDI?

Nilipotoa tangazo la sikukuu hii inayosherehekewa na Taifa la Waislamu (Nation of Islam) baadhi ya wasomaji walioniandikia wanaongelea jambo ambalo limejaa kwenye vyombo vya habari vikubwa: 1. Farrakhan anachukia wayahudi 2. Taifa la Waislamu wanachukia watu weupe.
Mhubiri Farrakhan sio peke yake anaandamwa kuwa anachukia wayahudi. Mwanazuoni Profesa Tony Martin aliyeandika kitabu cha The Jewish Onslaught naye amekuwa akiandamwa hata kwa vitisho vya kuuawa kwa madai kuwa anachukia wayahudi. Kutokana na wayahudi kushikilia vyombo vikuu vya habari pamoja na makampuni makubwa ya filamu na muziki, mtu yeyote akiongea jambo baya juu yao ataandamwa kila kona kiasi ambacho kila mtu ambaye hafanyi utafiti wa kina ataamini kuwa huyo mtu anachukia wayahudi.
Kama nilivyowahi kusema, watu wengi wanamfahamu mhubiri Farrakha kwa kupitia CNN na mashirika mengine ya habari. Huwezi kumjua Farrakhan kamwe kwa njia hiyo. Msikilize wewe mwenyewe ndipo utoe uamuzi juu yake. Kuamini upande mmoja unakuwa sawa na hakimu ambaye anasikiliza upande wa mashtaka bila kutoa nafasi ya kusikiliza upande unaoshtakiwa. Wewe ni hakimu, umesikiliza upande wa kina CNN na waongo wengine wakisema kuwa Farrakhan anachukia wayahudi. Sasa mpe Farrakhan nafasi ya kujitetea kwa kusikiliza kauli toka mdomoni mwake.
Hivi majuzi nikiongea na rafiki yangu Philin, ambaye kila dakika tunayokutana lazima tuwe na jambo la kubishana, aliniambia kuwa ni kweli kuwa Farrakhan anachukia wayahudi. Nikamwambia kuwa kama Farrakhan anachukia wayahudi kwa kuwasuta na kuwaandama juu ya madhambi na mapungufu yao, basi mtu wa kwanza kabisa kwa chuki dhidi ya wayahudi sio Farrakhan bali ni mwokozi wake (Philin ni mkristo) yeye ambaye ni Yeshua (Yesu Mzanareti). Anachosema Farrakhan leo juu ya wayahudi hajaanza yeye. Yote yalishasemwa tena kwa ukali zaidi zaidi ya miaka 2000 iliyopita na Yeshua (Yesu).
Farrakhan amewahi kupata vitisho mara nyingi vya kuuawa au kupelekwa mahakamani au mbele ya seneti toka kwa wayahudi . Mambo wanayomfanyia Farrakhan walimfanyia hata Yeshua (Yesu). Yeshua alipokuwa akiongea juu ya wayahudi, wayahudi hao walimjia juu kwa kunyanyua mawe ili wampige. Sikiliza kwa makini yanayotoka mdomoni mwa Farrakhan, kisha fuatilia chuki na tuhuma za uongo toka wayahudi na wengine dhidi yake. Kisha rudi nyuma miaka 2000 iliyopita uone yaliyotokea kwa mhubiri mwingine aliyedaiwa kuwa anachukia wayahudi. Ili urudi nyuma wakati huo, soma mwenyewe kitabu cha Injili ya Yohana 8:31-59. Kama huna biblia nenda hapa. Soma vyema mstari wa 59.
Mwenyewe utaniambia.

MAAFA YA NAGASAKI

Mwaka 1945 Marekani iliweka "rekodi" kwa kuwa nchi ya kwanza na pekee hadi leo hii kutumia bomu la atomiki dhidi ya binadamu wasio na hatia yoyote ile. Bomu hili lilitengenezwa kwa madini ya uraniumu toka nchi ya Jamhuri ya "Kidemokrasia" ya Congo. Tazama picha hizi za maafa haya yaliyofanywa na taifa hili linalojipa ukiranja wa kupeleka "demokrasia" nchi nyingine kama Afghanistani, ambako inadaiwa kuwa wanawake wamekombolewa (sijui kwanini hawaendi kukomboa wanawake wa Saudi Arabia ambao hawaruhusiwi kupiga kura, kugombea nafasi za uongozi, kuendesha magari, kupewa visa au pasi ya kusafiria bila kuandamana na mwanaume, n.k.). Bonyeza kwenye neno "next" ili uweze kutazama picha zote.

2/19/2005

MIZIKI IKIPIGWA MARUFUKU NA MABEPARI

Mapebari na makupe yanayotawala soko la muziki yakipiga marufuku muziki kwa madai ya kuvunjwa kwa hatimiliki nenda hapa ukaisikilize.

ETI SISI MASIKINI TATIZO LETU NI UZEZETA!

Hivi kwanini nchi nyingine zinaendelea na nyingine haziendelei? Eti kuna wanazuoni wanadai kuwa eti sisi wananchi wa nchi masikini tatizo ni akili zetu finyu. Maaluni kweli hawa jamaa. Hebu wasome hapa.

TOVUTI ZA VYUO VIKUU VYA AFRIKA

Hizi hapa ni tovuti vya vyuo vikuu vya nchi mbalimbali za Afrika.

TOVUTI ZA SERIKALI ZA AFRIKA NA IDARA ZAKE

Nenda hapa uone serikali za Afrika zilizoko katika mtandao wa kompyuta.

HISTORIA YETU: MICHORO YA KWENYE MIAMBA

Bara la Afrika limejaaliwa kwa michoro ya kwenye miamba. Mwezi wa pili mwaka jana, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (umoja ambao mwanamuziki Fela Kuti alikuwa akiuita Dis-United United Nations!), Koffi Annan, alizungumzia umuhimu wa michoro ya kwenye miamba barani Afrika ambayo ni urithi wa dunia. Ukienda hapa naweza kuona baadhi ya michoro hii iliyosambaa katika nchi mbalimbali za Afrika. Kongoli juu ya majina ya nchi zinakotoka picha hizo ili uweze kuona picha kubwa zaidi. Moja ya fundisho tunalopata kutokana na michoro hii ni ufundi wa hali ya juu ya kisanii waliokuwa nao waliotutangulia.

2/18/2005

SAMITE WA UGANDA

Kama hujawahi kumsikia Samite wa Uganda nenda hapa.

FILAMU ZA WATANZANIA

Baada ya Josiah Kibira kutengeneza filamu iliyopendwa sana ya Bongoland Mtanzania mwingine anayeishi Uingereza, Allan Kalinga, anatengeneza sinema iitwayo Vice-Wife (nyumba ndogo). Kibira naye anatarajia kutoa filamu nyingine katikati ya mwaka huu itakayoitwa Tusamehe.

SAMAHANI KUNA TATIZO

Kuna tatizo kwenye blogu yangu. Baadhi ya watu wakiifungua, upande wa kuume wenye picha, makala zangu, kona ya Freddy Macha, Kalamu ya Padri Karugendo, viunganishi vya blogu na tovuti nyingine, n.k. unahama na kwenda chini kabisa. Ninashughulikia tatizo hilo. Pia usiku nitaongeza makala za Freddy Macha na Padri Karugendo kutokana na maombi ya wengi. Pia kutokana na mimi kuzipenda.

2/17/2005

WONDERS OF THE AFRICAN WORLD

Yale malumbano ya wanazuoni yaliyotokana na filamu ya Wonders of the African World hapa. Niliwahi kuweka hapa bloguni aliyoandika Ali Mazrui na majibu ya Gates, Jr., aliyetengeneza hiyo filamu.

GOOGLEFIGHT.COM!

Umewahi kuona mpambano katika tovuti hii? Mpambano unaamuliwa kutokana na orodha iliyoko katika injini ya msako ya Google.

WANGARI MAATHAI KATIKA LUNINGA YA PBS

Kituo cha luninga cha PBS kitaonyesha mahojiano kati yake na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobeli, Mama Wangari Maathai, katika kipindi cha NOW hapo kesho. Kama ulipo unapata matangazo ya PBS basi usikose kusikiliza. Hata kama hupati kituo hiki au umekosa muda wa kufuatilia, PBS wana kawaida ya kuweka video za vipindi vilivyopita katika tovuti yao. Ukienda hapa unaweza kuona video za vipindi vizuri sana vya nyuma.
Mama Afrika (Wangari) anajulikana sana kutokana na juhudi zake kupitia shirika la The Green Belt Movement.
Pia ukienda hapa unaweza kuona video au kusoma hotuba aliyoitoa akipokea Tuzo ya Amani ya Nobeli huko Oslo, Norway.
*** Binti wa Mtandao usikose kabisa kipindi hiki!

NINASOMA THE BAGHDAD BLOG

Leo nimeanza kusoma kitabu kiitwacho Salam Pax: The Baghdad Blog. Kitabu hiki kinatokana na blogu ya kijana mmoja wa Iraki aliyekuwa akitupasha habari za hali halisi nchini Iraki. Alikuwa akiblogu hapa. Kitabu chake kinatarajiwa kuwa filamu.

Katika blogu yake na pia ndani ya kitabu amemnukuu ujumbe huu: "the West won the world not by the superiority of its ideas or values or religion but rather by its superiority in applying organized violence. Westerners often forget this fact, non-Westerners never do, " toka kwa Samuel P. Huntington aliyeandika kitabu ambacho ukikipata usiache kukisoma kiitwacho The Clash of Civilizations and the Remaking of World Order. Katika kitabu hiki, hoja yake kuu ilikuwa ni hii: mgongano mkubwa wa karne hii na zijazo hautakuwa kati ya taifa na taifa au juu ya itikadi au uchumi bali kati ya tamaduni na tamaduni. Kwa undani zaidi soma hapa.

MANISPAA YA ZANZIBAR NAYO KWENYE MTANDAO WA KOMPYUTA

Yakhe, sisi nasi tumo ati! Hapa.

SERIKALI KWA MTANDAO WA KOMPYUTA

Mtwara na Lindi nao hawako nyuma katika kuingia katika mtandao wa kompyuta. Kongoli hapa.

SERIKALI YA ELEKTRONIKI (E-GOVERNMENT)

Wilaya ya Kinondoni nayo ina tovuti. Hapa.

TEKNOLOJIA VIJIJINI: AMINI USIAMINI

Amini usiamini. Kijiji cha Lunga, kata ya Lugoba, wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani, kina tovuti! Tovuti yake ndio mfano hasa wa jinsi ambavyo tovuti za bunge, ikulu, ofisi ya mlaji mkuu (au nimwite waziri mkuu nisije shtakiwa), n.k. zilipaswa kuwa...nazungumzia lugha. Kama unaishi ughaibuni na nyanya yako anaishi kijiji cha Lunga, basi unaweza kumtumia barua pepe. Tovuti yao hii hapa.

MWANABLOGU HUYU MTANZANIA ALIISHIA WAPI?

Kuna mwanablogu Mtanzania aliyeblogu mara moja katikati ya mwaka jana kisha akatoweka. Yu wapi? Msome hapa.

WILAYA YA MUFINDI MTANDAONI

Wilaya ya Mufindi, Iringa, ikoa katika mtandao wa tarakilishi. Kongoli hapa uende Mufindi dakika hii. Ila usisahau kuwa na kamusi ya kiingereza. Jamani! Nilie, nisilie?!

VITABU 100 BORA VYA AFRIKA KARNE YA 20

Orodha kamili ya vitabu 100 bora Afrika vya karne ya 20 hii hapa. Tazama Tanzania kuna vitabu vingapi. Kama vipo au kipo umekisoma au kuvisoma? Mjadala mkali uliozuka kutokana na orodha hii huu hapa.

2/16/2005

TAFADHALI MSOME PADRI KARUGENDO NA FREDDY MACHA

Natangaza tena kuwa safu ya Padri Karugendo imeanza. Safu hiyo inaitwa KALAMU YA PADRI PRIVATUS KARUGENDO. Safu hiyo, kwa sasa, iko upande wa kuume wa blogu hii, chini ya safu ya Freddy Macha.
Pia kona ya Freddy Macha ambayo ilikuwa na matatizo sasa iko hai. Kuna makala mbili mpya. zote zinamhusu hayati Bobu.

MSANII WA TANZANIA ULINDULA MWAKISOPILE

Tazama hapa kazi za msanii wa Tanzania, Ulindula Mwakisopile.

UNAWAFAHAMU AFRICANCOLOURS.NET?

Tembelea tovuti hii uone kazi za sanaa za Waafrika. Nadhani makao makuu ya hawa jamaa yako Nairobi, Kenya. Hapa.

HISTORIA YETU: VITABU 100 BORA VYA AFRIKA KARNE YA 20

Soma mjadala uliotokana na orodha ya vitabu 100 bora vya Afrika vya karne ya 20. Nenda hapa. Hili ndio lilikuwa jopo la waliochagua orodha hiyo:
Professor Njabulo Ndebele (Chairperson)
Ms. Wangui wa Goro
Dr. Alastair Niven
Dr. Fatoumata KeitaProfessor
Fatima Mendonca
Dr. Ato Quayson
Dr. Zifikile Mguni-Gambahaya
Professor Ali Mazrui
Professor Helge Ronning
Professor Bankole Omotoso
Professor Eldred Jones
Mr. Bernard Magnier
Dr. Adotey Bing
Dr. Nana Wilson-Tagoe
Mr. Samir Saad Khalil
Professor Alois S. Mlambo (Ex-officio)

JIFUNZE KISWAHILI

Apple = tofaa
Review = marejeo

TUZO ZA BLOGU

Habari ndefu kuhusu tuzo za blogu. Kongoli hapa.

2/15/2005

MACHO YA LAURA

Umesoma kitabu cha George Orwell au kutazama sinema ya 1984? Macho ya Laura inazungumzia jambo kama hilo kwa sanaa mpya ya mtandao. Yatazame macho ya Laura hapa.

KONA YA FREDDY MACHA NA KALAMU YA PADRI KARUGENDO

Nenda kwenye kona ya Freddy Macha, chini ya makala zangu. Kuna makala mbizi kuhusu Bob Marley. Pia Kalamu ya Padri Karugendo imeanza. Iko chini ya kona ya Freddy Macha. Karugendo ana makala nzuri sana kuhusu Sumaye na Urais wa Tanzania.

2/14/2005

KITABU KIPYA KIZURI SANA TANZANIA

Tafadhali sana. Tena sana. Wasomaji wangu walioko Tanzania, kanunue kitabu kipya kiitwacho PAMBAZUKO GIZANI kilichoandikwa na Karumuna Mboneno. Kama uko Dar Es Salaam, nenda duka la TPH mtaa wa Samora. Kwa mikoani, nitawaeleza baadaye mnakoweza kukipata.

HISTORIA YETU: UNALIJUA ZIWA NAMLOLWE?

Ziwa Namlolwe ni ziwa ambalo hivi sasa, kutokana na ukoloni na utumwa wetu wa mawazo waliotuachia wakoloni, linaitwa Ziwa Vikitoria (Lake Victoria.) Waluo walikuwa wakiliita ziwa hili Namlolwe.
Huyu malkia mwenye ziwa Afrika Mashariki sijui alitufanyia nini watu wa Afrika Mashariki kiasi cha kuamua kulipa ziwa hili jina lake. Hivi kuna ziwa au mto gani kule Uingereza uliopewa jina la Mwafrika?
Kule Zimbabwe kuna maporomoko yanaitwa Maporomoko ya Vikitoria (Victoria Falls). Jina la asilia la maporomoko haya ni Mosi O Tunya (yaani moshi utoao mlio kama radi).

MSIKILIZE MWALIMU NYERERE

Nimemtaja Mwalimu. Kwanini usimsikilize? Nenda hapa.

WAGOMBEA ULAJI

Msururu wa wagombea ulaji, wengine wanauita urais, unaendelea kuwa mrefu. Wako wanaotangaza nia yao kichinichini, wako waliotamka hadharani, wako walioanza kuchukua fomu. Katika hawa nasikia Sumaye naye yumo. Sijui anafikiria nini. Hivi hana washauri?
Mwaka 1995 mjini Dodoma, hayati Mwalimu Nyerere alitaja sifa ambazo mgombea urais wa Tanzania anapaswa kuwa nazo. Alisema kuwa mgombea urais lazima aonekane kukerwa na rushwa. Mtu huyo lazima awe tayari kukabiliana na tatizo hilo.
Mwalimu akawaambia wajumbe wa CCM, "Ndugu wajumbe mkiulizwa mgombea huyu ana uwezo wa kupambana na rushwa jibu liwe ndio, litoke ndani ya moyo na si mdomoni...."
Toka mwaka huo 1995 hadi leo hatujapata mtu ambaye ameonekana kuchukia rushwa kwa moyo wake wote na kupambana nayo.
Nikiulizwa kama Sumaye ana uwezo wa kupambana na rushwa (ambayo naye ametuhumiwa mara nyingi kushiriki!) siwezi kusema 'ndiyo' toka moyoni. Sio hivyo tu. Siwezi hata kusema 'ndiyo' toka mdomoni!

HAKUNA KIUMBE DUNIANI AU KWINGINEKO...

Nilipokuwa nawaeleza juu ya watu wanaotaka niache kublogu nilisahau kusema haya: HAKUNA KIUMBE AWAYE YEYOTE, DUNIANI AU KWINGINEKO, ATAKAYEWEZA KUNIZUIA KUTUMIA UHURU WANGU WA KUTOA MAONI, KUFIKIRI, KUANDIKA, NA KUWASILIANA. HAKUNA. NASEMA HAKUNA.
UMESIKIA?

JE UNAJUA?

Unajua kuwa wauza maua wamepigwa marufuku kuuza maua mekundu ya siku ya Valentino huko Saudi Arabia?
Unafahamu pia kuwa Saudi Arabia ilikuwa na uchaguzi wa mitaa wa kwanza hivi majuzi? Katika uchaguzi huo wapiga kura na wapigiwa kura walikuwa ni wanaume tu. Wanawake hawakuruhusiwa kugombea au kupiga kura!

JE UNAJUA?

Unajua kuwa Indonesia ni nchi inayotokana na visiwa zaidi ya 14,000?

KITABU CHA 'DARK SIDE OF MWALIMU'

Rafiki yangu, 'Binti Mtandao,' kanitumia viunganishi vya kitabu alichonitajia wiki kadhaa zilizopita. Kitabu hiki kinaitwa The Dark Side of Mwalimu. Kimeandika na Ludovick Mwijage, mkimbizi wa kisiasa toka Tanzania anayeishi Denmark. Mwijage, ambaye nilikuwa nikimsoma zamani sana kwenye gazeti la Africa Events, alitiwa kizuizini mwaka 1983 hadi 1985.
Kusoma kitabu chake nenda hapa na hapa. Mwijage ameandika kitabu kingine kiitwacho Of Magic and Mutiny. Kinauzwa hapa na kuzungumziwa hapa.

2/13/2005

UTAKUWA WAPI TAREHE 27 MWEZI HUU WA PILI?

Kwa miaka miwili nimekuwa nikifuatilia kwa njia ya satalaiti hotuba za Siku ya Mkombozi inayosherehekewa tarehe 27, Februari na waumini wa Taifa la Waislamu (Nation of Islam.) Nadhani kama unataka kujua staili, kipawa, na utamaduni wa wahubiri weusi wa Marekani, msikilize Louis Farrakhan. Watu wengi wanamfahamu Farrakhan kijuujuu, mara nyingi kupitia vyombo vya habari ambavyo wanachosema juu yake ni kuwa anachukia Wayahudi na watu weupe. Wakisema jambo zuri juu yake watazungumzia tu Maandamano ya Wanaume Milioni Moja (Million Man March) ambayo aliyaandaa Oktoba, 1995. Aliita wanaume Waafrika wa Marekani milioni moja, wakaja zaidi ya milioni moja!
Nadhani kumfahamu Farrakhan vyema unapaswa kumsikiliza. Nenda hapa ujue jinsi utakavyoweza kumwona na kumsikiliza kwa satalaiti siku hiyo kutegemea na mahali ulipo. Nikiwa Ohio nilikuwa nakwenda kumsikiliza na waumini wa msikiti namba tano katika hoteli moja katikati ya mji wa Toledo. Ni wakati huu niligundua kuwa sijawahi kukutana na Waafrika wa Marekani walio na unyenyekevu, usafi (wa lugha, mwili, na nguo), na upenzi wa maarifa na elimu usio na kifani. Ni kipindi hiki nilikutana na wanawake Waafrika wa Marekani ambao wanavaa mavazi ya kusitiri mwili wakiamini kuwa akili na nyonyo zao ni bora kuliko sehemu zao za mwili ambazo huachwa wazi na wanawake wengi hapa.

MWEZI WA HISTORIA YA WAAFRIKA WA MAREKANI: IJUE 'BLACK POWER'

Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, hapa Marekani, kina onyesho la miaka 40 ya vuguvugu la 'Black Power.' Nenda hapa upate undani wa vuguvugu hili lililokuwa na vitu kama mtindo wa nywele wa Afro, kauli mbiu ya "I am Black and Proud," chama cha Black Panther, n.k. Ukifika hapo tazama mkono wa kushoto kuna orodha ya mambo kadhaa ambayo unaweza kujifunza kwa kupitia picha na maandishi. Bonyeza upendapo.

HOTUBA YA BALOZI ILIYOZUA KIZAAZAA KENYA

Balozi wa Uingereza nchini Kenya, Sir Edward Clay, hana tabia ya kuficha chuki aliyonayo dhidi ya rushwa nchini Kenya. Soma mwenyewe aliyoyasema nchini Kenya tarehe pili mwezi huu katika hotuba yake hii.

2/12/2005

BWANA UKWELI

Bwana Ukweli kaanza kutumia "cha" kama kwenye , 'kiti cha Ukweli.' Ambacho hajajua ni kuwa husemi "cha" kwa kila kitu. Kwa mfano anavyosema, "Mpira cha Ukweli." Au alivyosema leo asubuhi, "Kofia cha Ukweli."

Umri?
Anakaribia miwili na nusu.
Anaongea lugha ngapi? Tatu!
Tatu?
Ndio, tatu. Ya kwanza alianza nadhani akiwa na miezi sita au saba. Wakati huo alianza kujifunza lugha ya ishara kama wanayotumia viziwi. Ufundishaji wa watoto lugha ya ishara unaanza kuenea kwa kasi. Wanasaikolojia walitafiti wakagundua kuwa tunapoacha watoto waishi kwa miaka kadhaa kabla hawajaweza kuwasiliana nasi zaidi ya kulia ni kama mateso.

Watu wazima tunashindwa kujizuia hata tukiwa tumekutana na watu tusiowajua. Yanayotokea ndani ya mabasi unajua. Mwanzoni mkaa kimya kama vile hamjui kuongea, lakini wakati wote huo kuna kisu kinawakata ndani kwa ndani, mnataka kuongea na kumjua mwingine. Hiyo ni kiu ya kuwasiliana.

Mtoto mchanga haina maana hana mambo anayotaka kukwambia. Anayo mambo mengi ila mfumo unaotumiwa kukueleza jambo inabidi ajifunze kwa muda mrefu zaidi. Hapo ndio unaona mtoto akitaka kitu analia. Mzazi anaanza kutumia "utabiri" kujua mtoto anataka nini.

Kulia kwa mtoto wakati mwingine sio kwamba anataka kitu bali kuna jambo anataka kukwambia ila anashindwa. Kulia kunakuwa ni njia ya kupambana na kuchanganyikiwa. Fikiria wakati mwingine unapopata hasira unapomwambia mtu kitu lakini hakusikii. Mtoto naye anaposhindwa namna ya kukwambia anapata ghadhabu.

Kwahiyo watoto wanafundishwa jinsi ya kutumia alama za mikono. Uwezo wao wa kutumia mikono wakati huu uko juu zaidi ya uwezo wa kutumia sauti na kuunda maneno.

Mwanzoni nilifikiri kuwa hii ni porojo. Mtoto atumie alama za vidole na viganja? Nilijiuliza nikiwa ninasita kuamini kwa haraka. Baada ya Mama Ukweli kumpatia Bwana Ukweli shule ya matumizi ya ishara kuongea nilishuhudia mwenyewe. Bwana Ukweli alianza kujua kusema, "Naomba kunyonya," "Naomba maji," "Nataka kulala." "Acha," "Miti," "Ndege," "Asante,"
"Zaidi," n.k.

Sikumbuki kule juu nilianza na kitu gani. Na kwakuwa nimechoka sana, siwezi kurudia kusoma. Ninaishia hapa. Ninywe maji ya moto nilale. UWE UNAKUNYWA MAJI YA MOTO KABLA YA KULALA.

NATANGAZA MAMBO MAWILI

Kwanza, ni kweli kuwa kuna watu, kwasababu wanazojua wao na waliowatuma, wamenitaka niache kublogu. Kwani unadhani nilitaka kujua eti kwanini niache kublogu? Huko ni kupoteza muda muhimu. Natatumia muda huo kuzungumza na ukimya. Sina haja ya kujua sababu maana hakuna sababu zozote zinazoweza kunisimamisha kublogu. Napenda kuandika na kuna watu wanapenda kusoma. Nukta! Kituo! Mimi kama raia wa nchi yangu nina haki ya kikatiba ya kutoa maoni na kuyasambaza kwa wengine (ndio, ili wanyanyuke na kuwanyang'anya ulaji). Nina haki hiyo pia kama binadamu.

Pili, jamaa ambaye kisa cha Mswahili na mtoto wa kizungu kinatokana na maisha yake, ameshtukia stori. Anasema kuwa ingawa sijamtaja jina, anajua kuwa nimeandika maisha yake na hataki kusoma mtandaoni. Bado tunabishana juu ya kukiondoa au kukiacha kisa chenyewe ndani ya blogu. Hivi nilifanya kosa? Kisa chenyewe kinasisimua. Na isitoshe sikumtaja jina na mambo mengi nimebadili hata watu wenyewe aliohusika nao wakisoma hawataelewa chochote. Kosa liko wapi?

Ngoja nifikirie.

UNAWEZA KUMSIKILIZA CASTRO KWA MASAA MANGAPI?

Kiongozi wa Cuba, Fidel Castro, anafahamika kwa tabia yake ya kuhutubia kwa muda mrefu. Jana jijini Havana, katika mkutano wa kimataifa juu ya ubinafsishaji, Castro alihutubia kwa masaa sita.

Castro anaweza kuhutibia mkutano wa hadhara kwa masaa hayo sita na kisha anaendelea na hotuba yake redioni baada ya muda.

UNATAKA KWENDA KUSOMA FINLAND???

Mwanablogu toka Kenya, Sanaa, anayeishi Finland anatoa ushauri kwa wanaotaka kwenda kusoma Finland. Kwanza utaelimika na pili utacheka sana. Hivyo jiandae:

Is Finland the land of milk and honey or ice and black bread...
plus all sorts of weird sausages?

You decide.

So many people after reading my blogg have emaild me and asked me on how to apply for schools in Finland and are in a rush to come and study here...well, i don't know what image i painted of Finland (esp to the people in Kenya as they seem to compare everything with worse off kenya and seem to think every place is better than Kenya even Iraq)

My intentions are not o misguide anybody...and to save myself the trouble or replying every single email on How to get to Finland ...Fastest way to get to Finland!
am going to write it here and you can decide on your own.There are two types of institutions for adults in finland.Polytechnic and Universities. Both offer the same kind of studies leading to undergraduate degrees and have small differences such as ..in the Polytechnic you MUST attend class and in the University you can do as you please, read on your own but have to attend exams.

Well that just applies to us foreigners...you miss school for three days and they send the dogs after you! cops rather lol.Both Universities and Polytechnics have a Bi-annual application period..one starting on January to end of feb. and the other in the months of spring....April to summer....june. The schools in the capital city have a shorter and earlier application period than the schools outside the big cities.On application if you pass the preliminaries...u know essays and crap then you get invited for an Entrance exam.. If you applied for a school in Helsinki..they invite you to do an exam in Finland...meaning you have to get a short visa which will only be extended when you pass your exams. If by any chance you come to finland and fail your entrance exam...you must return t kenya...and Finland is not one of those places where you hide at your friends place for a month and leave the house at night. you just have to go back.

It helpes to apply for several schools at once so you can have the option of sitting for many entrance exams and depending on your IQ you have increased chances of staying.If on the other hand you apply for a school in smaller cities (gishagi) then you will be invited to sit for an entrance exam in KENYA at the Finnish Consulate. If you pass then you can apply for for a visa.Well , on being granted a visa you have to deposit 6000 euros (lol) in a bank account in Finland under your name...sio ile u take your mothers bank statement with 4 million and take it to the embassy. They only need 6000 euros in your account in a Finnish bank in Finland.well, whoever said that living in Finland is a circus must have lied. Its hard to live in Finland. If your not living in the big cities which are only 3 then your life will be a living hell.

Nowdays the embassy is cautious on issuing visas for schools that are in big cities coz they want to make it harder for African leeches to enjoy their free education and free metro rides (lol) Education is free but rent and food is not lol...If you have to move to Finland...your parents must be very rich or you must have saved up some crazy loot to last you through the Great Finland Depression which lasts close to 3 years for everybody..because after three years you can be able to at least say hello and good night in finnish.Its not easy to get a job and its nearly impossible esp for people living outside the three big cities Helsinki, Tampere and Oulu.

People living in big cities...if they are lucky they will land a cleaning job yaani janitor..(we call it kazi ya Dj coz you get to spin the floor) if your even luckier you will get a Hotel job( house keeper...cleaning out used condoms n dirty linen n crap like that...or a kitchen assistant...just standing in the kitchen and having the chef gossip about you in their weird language...thank God you wont understand...or you can be the dishwasher...dunno why they call it that coz there is a dishwashing machine...your bound to develop some muscles after cleaning industrial size sufurias lol)

People in smaller cities are most of the time jobless and if they are lucky they will land a Newspaper delivery boy job..we call it minoxia (minox ama boder border only this time you don't have chicken on your bicycle but wet ,heavy newspapers..that pple throw in the trash soonest you deliver them) lol where you have to wake up at 3.00 am and drag your bicycle in the snow with bulky (heavier when wet) news papers...Elevators are an un common thing in apartments here coz the people like to keep fit! so you have to drag your 60 news papers up the 6 floors...i can assure you people who deliver newspapers are under 50kgs in weight...as if dragging newspapers in the snow is not worse...you finish the deliveries at about 6.00 am in the morning and you have to rush home like a vampire before day break....Only to go home and drink a cup of coffee and rush to school..because if you miss school then they call the cops on you...Its always safe to keep your bags packed in case of anything say deportation...and trust me when they dont want u here they use all means to deport you..like drugging you with paralysing (coma inducing) drugs and throw you in a plane to Kenya.

If your among the chosen few in the gishagi cities you may land a floor dj job (janitor)....and it doesnt get better.Well surviving and paying bills is one thing and staying in school is another. School may be free even for foreigners but if your a foreigner you have to pass in school every year if not...your visa will be revoked which is renewed every year...with the same amount of money 6000 euros.

Cops from time to time demand for your bank statement...and transactions to see how you spend your money...if you have insufficient funds...or if you have suspicous amounts of money from nowhere...yeah its that bad!I hope by now you have a clear image of what its like to study in Finland...if you cant take the heat of all the above...you can do like the rest of the world does...get married or get pregnant..(thats a different story all together.)

Finland may be one of the safest, less populated, cleanest cities with little criminal acitivity..but it s most definately not a place where you can holiday while studying. This is one of those countries that has so many old people with so much money...it should be more of a Retirement Home...due to the clean air....less population and hefty price of items. You either have a lot of money while coming here or a Game plan that works.

When i moved here,i knew about the benefits of studying and living here..but no one told me the cons of this shitty place...i blame my friend (unajijua) and still blame her but like they say..invite a friend to share your misery and its lessened by half. You need to be of strong character to survive here utoto yote unawacha nyumbani. Its maddening and am still in the process of losing my mind..i guess it explains my maddening behaviour and rants on this blogg.

Oh and one more irrelvant fact about Finland...Finland has the largest selection of bread in the world and when you get invited for dinner and have to eat black salty bread that tastes like a mix of pancake and marram (lami) ...do not by any means throw away any piece as it is considered bad luck...and Do not eat the last piece of black bread as it is considered taboo and will ensure an everlasting supply of food in the house.....(and i thought wajinga waliuwawa..kumbe walikuja finland)

Hope this has been informative to all who have been asking me on how to study in Finland.

UMEWAHI KUISIKIA CAPOEIRA?

Michezo ya kuimarisha uwezo wa kujilinda, kutunza afya, kuimarisha akili na roho, kama vile Kung Fu, Taekwondo, karate, Goju Ryu, n.k. inajulikana na wengi. Lakini mchezo wenye mantiki kama hii ya kutoka Asia uitwao Capoeira haufamiki na wengi. Mchezo huu ambao asili yake ni Afrika unaanza kupata umaarufu hivi sasa ingawa umekuwepo kwa miaka mingi. Soma juu ya asili yake hapa.

SUMAYE ACHA KUTANIA!

Nasikia kuwa Sumaye, yaani Waziri Mkuu wa Tanzania, ametangaza rasmi kuwa anataka kugombea urais. Niliwahi kuandika ndani ya blogu hii kuhusu madai kuwa Sumaye ana nia kama hiyo. Nilisema kuwa watu wanamsingizia maana ninaamini kuwa anajua fika kuwa hawezi kabisa kazi hii. Kama kazi ya Uwaziri Mkuu ameshindwa, atawezaje Urais?

Kumbe nilikuwa ninaota. Sasa ametamka kuwa anataka urais. Anataka kukimbilia kule Mwalimu Nyerere alikowahi kuwauliza, "Kuna nini, mbona mnakimbilia huko?"

Hoja yangu kuu niliyoitoa nikisema kuwa Sumaye hawezi urais ilikuwa ni hii: Tanzania inapitia kipindi kigumu sana cha mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kitamaduni, na kisiasa. Kipindi hiki kimevaa shati la rushwa, suruali ya ubadhirifu, na viatu vya mikataba ya kitapeli. Kwa misingi hiyo tunahitaji viongozi wenye kuwa na njozi. Vingozi wenye visheni. Viongozi ambao wana uwezo wa kuongoza zaidi ya kuhutubia na kuzunguka huku na huko kuzindua kitu wanaita, "miradi ya maendeleo."

Tazama Tanzania: barabara toka enzi za mkoloni mpaka leo. Kilimo tumeshindwa huku tumebaki na wimbo wa "kilimo uti wa mgongo wa taifa." Nadhani wanachosema katika wimbo huu ni kuwa kilimo ni ugonjwa wa uti wa mgongo wa taifa. Neno ugonjwa huwa wanalisema kimya kimya.

Biashara tumeshindwa. Viwanda tumeua. Elimu bado tunayo ile ya mtu kujua kusoma na kuandika. Kwenye afya, wanawake wanazalia sakafuni, wengine nje ya hospitali. Migodi tumeshindwa kuendesha. Utalii wakenya wametunzunguka hadi mlima kilimanjaro umekuwa wa kwao!

Rafiki yangu mmoja kaniambia kuwa wageni wakishachuma maliasili, utafika wakati hata funza hawaitaka Tanzania.

Tembelea tovuti hii ya ofisi ya Sumaye. Kwanza tazama lugha gani imetumika. Kisha ukikutana na Sumaye muulize anapohutubia wananchi huko Newala, Bariadi, Lushoto, Babati, n.k. huwa anatumia lugha gani? Kama anatumia Kiswahili, kwanini tovuti yake imejaa kimombo cha kule kwa Malikia Lizabeti? Kisha mdhihaki kidogo, mwambie kuanzia sasa aanze kuzunguka nchi nzima akihutubia kwa kiingereza! (Nimeandika gumzo la wiki juu ya suala hili, ambayo nitaiweka ikishachapishwa kule Tanzania).

Ukishafika kwenye tovuti hiyo tazama picha yake akijifanya yuko "bize." Kila nikimwangalia ninajiuliza, "Hivi ni mkataba gani wa ulaghai alikuwa anasaini alipopiga hiyo picha?" Hawa watu wananitisha sana ninapowaona na suti zao na kalamu za gharama wakitia wino mikataba. Inanikumbusha Mangungo wa Msovero!
Nenda hapa.

WATU WEUSI DUNIANI: JE UNAJUA?

Je unajua kuwa taifa la kwanza lenye watu wengi weusi duniani liko barani Afrika, Nigeria, na la pili liko nje ya Afrika, Brazili!

BLOGU NA VIBARUA VINAVYOOTA MAJANI!

Blogu zina mikasa yake. Soma yanayowapata wanablogu wanaojadili masuala ya waajiri wao mtandaoni. Hapa.

2/11/2005

JE UNAJUA?

Je unajua kuwa mwezi huu wa pili ndio Wachina wanasherehekea mwaka mpya wao?

MAKALA YA FREDDY MACHA KUHUSU BOB MARLEY

Tafadhali soma makala nzuri sana kuhusu miaka sitini toka kuzaliwa kwa Bob Marley iliyoandikwa na Freddy Macha kwa ajili ya safu yake katika gazeti la Mwananchi, nchini Tanzania. Kongoli hapa.

MAKALA MPYA KUHUSU UTAMADUNI

Kutokana na mwezi huu kuwa ni wa kumbukumbu ya historia ya waafrika wenzetu wa Marekani, nimeandika makala kuhusu utamaduni. Nenda katika kona ya makala zangu uisome. Inaitwa: KAMA UNAPENDA UTAMADUNI, MBONA UNAVAA NGUO?

Napenda pia kuwaomba msamaha wasomaji wangu kwa kuwa sijatimiza ahadi ya kuweka makala za Padri Karugendo ambaye ameshanitumia. Kona yake itakuwa tayari kabla ya mwisho wa wiki. Pia ile kona ya Freddy Macha itakuwa imefanyiwa ukarabati na kuongezewa makala mpya.

2/09/2005

MJADALA WA MAZRUI NA GATES

Kutokana na mwezi huu kuwa wa historia yetu, nimeamua kuweka tena ule mjadala mkali kati ya Profesa Ali Mazrui na Dakta Louis Gates, Jr. Nenda hapa.

2/07/2005

BLOGU YENYE PICHA NA HABARI ZA TAMASHA LA BOB MARLEY

Kwa wale wapenzi wa Bob Marley, nenda hapa.

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com