1/06/2006

Unajua Jinsi Ya Kuandika Kuhusu Afrika?

Binyavanga Wainaina ameandika makala moja nzuri sana ambayo inatumia kejeli kutazama jinsi ambavyo watu weupe wanavyolitazama bara la Afrika. Katika makala hii anatoa ushauri wa jinsi ya kuandika habari za Afrika. Lakini, kama nilivyosema hapo awali, ushauri wenyewe ni kejeli fulani hivi. Bonyeza hapa usome makala yenyewe.
Binyavanga ni mwanzilishi wa jarida la fasihi nchini Kenya liitwalo Kwani?, ambalo unaweza kulisoma kwa kubofya hapa. Pia unaweza kusoma zaidi juu yake kwa kubonyeza hapa.
Asante Kenyan Pundit kwa makala hii.


3 Maoni Yako:

At 1/06/2006 05:11:00 AM, Blogger mwandani said...

Mwandishi huyu nilimsoma hapo nyuma kidogo kupitia Africa Unchained, ambapo aliunganishwa kupitia:
http://www.granta.com/extracts/2615
Kwa wakati huo sikuipata kejeli nikadhani na yeye ni Brutus na jambia lake anaimaliza Afrika kimtindo. Sasa nimesoma tena, naona wanunuzi wa vitabu ulaya watafikiria kidogo wakisoma mawazo ya huyp bwana.

 
At 1/06/2006 05:37:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Ndio kiuongo kilekile, ngoja nipunguze haraka
Tunga

 
At 1/07/2006 01:13:00 AM, Blogger mark msaki said...

mwandishi amefanya kazi nzuri hapa. na naona amekuwa makini kutumia lugha ya walengwa ili waupate ujumbe vyema. itabidi badaye auweke pia kwa kiswahili ili kutuwezesha na huku ndani!

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com