12/20/2005

Blogu Ziitwe Ngwanga?

Mjadala huu huwa unazuka na kutokomea. Jeff ameuanzisha tena. Bonyeza hapa usome aliyoandika. Pia tazama sehemu ya maoni. Soma changamoto ya Mwaipopo (ambaye nasikia ataingia rasmi kwenye blogu hivi karibuni). Da Mija akapokea wito wa Jeff. Anapendekeza neno Ngwanga litumike badala ya neno "blogu" ambalo baadhi wanaona kuwa neno hili tumelichukua kutokana na uvivu tu. Yaani tumechukua neno la Kiingereza "blog" tukaongeza "u." Bonyeza hapa. Pia tazama maoni yaliyotolewa hapo kwa Da Mija. Unaweza kuchangia hapo kutokana na pendekezo la Da Mija.

5 Maoni Yako:

At 12/20/2005 07:57:00 PM, Blogger Gatua wa Mbũgwa said...

This comment has been removed by a blog administrator.

 
At 12/21/2005 01:45:00 AM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Ndesanjo, tunaomba uisimamie hii shughuli ya jina mbadala la blog. Mwaka huu tuumalize tukiwa na jina letu. Unasemaje?

 
At 12/21/2005 08:34:00 AM, Blogger Gatua wa Mbũgwa said...

Ndugu Ndesanjo,
Nafurahi sana kuusoma mjadala wenu wa kutafuta neno la Kiswahili halisi badala ya kulitumia neno "Blogu", ambalo ni la mkopo kutoka kwa kiingereza.

Nami nimekuwa na fikra kama hizo zenu kuhusu neno hilo hilo (blog) kwa lugha yangu ya Gĩgĩkũyũ.

Basi nafurahi kuwaambia kwamba nimeona neno "Kĩhũngĩro" linafaa zaidi kuliko kusema mburogo ama mburogu, tena neno hili lina maana sawa ingawa ni letu wenyewe.

Kheri kwenu wote ndugu zangu,

Gatua

 
At 12/21/2005 07:54:00 PM, Blogger Gatua wa Mbũgwa said...

Tuseme nyuki huenda kutafuta "nectar". Basi pahali hapo nyuki huenda panaweza kuitwa "kĩhũngĩro" kwa lugha ya Gĩgĩkũyũ. Pili, watu hukutana pahali ili wapashane habari za kwao ama za kwingineko. Pahali hapo wanapopashania habari panaweza kuitwa kĩhũngĩro tena. Nasi wanablogu tunaingia mtandaoni kukusanya na kupashana habari kutoka tovuti mbalimbali ama kutoka kwingineko. Hapo pahali tunapokusanyia habari si panaweza kuitwa kĩhũngĩro? Basi nikaita blogu vile!

Kheri!

Gatua

 
At 12/22/2005 03:24:00 PM, Blogger Boniphace Makene said...

Waungwana baada ya kimya nami nimechangia na nimefafanua sana katika bustani ya Jeff nini mawazo yangu kuhusu blogu kuanza kuitwa Gazeti Tando.

Naomba niwasilishe hoja.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com