12/17/2005

Samaki Mkunje Angali...
Samaki jamani lazima umkunje mapema mapema. Ndio anavyokunjwa mwanamapinduzi wa kesho, Ukweli Ndesanjo, kama unavyomuona hapo kwenye picha ya juu. Hiyo ilikuwa ni Oktoba mwaka huu wakati wa maandamano ya Vuguvugu la Mamilioni na Zaidi. Hapo anamtazana na kumshangilia mwanamuziki aliyehamia Marekani toka Haiti, Jean Wycleaf. Picha ya chini yakea ndio Wycleaf mwenyewe anaonekana kwenye luninga (iliyokuwa ikirusha matangazo kwa walioko mbali na jukwaa kuu). Ingawa anamshangilia Wycleaf kwa furaha, Ukweli anawapenda zaidi Fela Kuti na Bob Marley. Masikini, hatakaa awaone wakitumbuiza hadharani.

7 Maoni Yako:

At 12/17/2005 11:28:00 PM, Blogger Boniphace Makene said...

Ndesanjo hongera kumlea huyo hapo Capitol. Najua Mwaipopo mwanablogu mpya ajaye atacheka sana maana anajua utani wa kulea watoti hapo Capitol.

Kazi nzuri na picha safi sana katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

 
At 12/18/2005 10:18:00 AM, Anonymous mwaipopo said...

Bony nshakupata.

 
At 12/18/2005 12:08:00 PM, Anonymous mshairi said...

Mpicha nzuri sana!

 
At 12/20/2005 12:39:00 AM, Blogger mloyi said...

Kidume cha shoka? angalia amerika isimwaribu. Muulize busta rhymes.

 
At 12/20/2005 02:01:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Akihitaji mchumba yupo, ni kiasi cha kutoa hoja tu.

 
At 12/20/2005 03:58:00 AM, Blogger mwandani said...

unamfunza kiswahili lakini?
usisahau kumleta likizo ndefu nyumbani kila inapobidi. Utamaduni muhimu. Hapa niliko kuna vijana weusi wa rangi tu lakini utamaduni na akili zao kama wenyeji wa hapa...

 
At 12/20/2005 05:31:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Ukweli anaongea lugha tatu: Kiswahili, Kiingereza, na lugh ya ishara (kama wanayotumia viziwi). Lugha hii ya ishara alijifunza toka akiwa na miezi saba. Utamaduni wa kufunza watoto lugha ya ishara (ambayo wanaishika kwa haraka kabla hawajaweza kuongea) unakua kwa kasi. Faida yake ni kuwa kabla mtoto hajaweza kuongea kwa kuunda maneno mdomoni, anakuwa anaongea nawe kwa kutumia ishara. Anayetaka funza mwanaye awasiliane nami.

Ukiacha lugha hizo, anajua maneno ya hapa na pale toka lugha mbili: Kichagga na Kispaniola.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com