12/16/2005

Wanaume wa shoka....Wanaume hawa wa shoka ni akina nani? Hawa ni walinzi wa kiongozi wa kundi la New Black Panther Party, Malik Zulu Shabazz. Malik ambaye ni mwanasheria ni machachari sana kwa siasa zake kali ziilizojengwa juu ya falsafa za akina Malcolm X, Marcus Garvey, Kwame Toure, n.k. Malik Zulu Shabazz ndiye aliyeko mbele katika picha hii. Picha hii niliipiga siku ya maandamano ya Vuguvugu la Watu Zaidi ya Milioni, Washington, DC.

4 Maoni Yako:

At 12/16/2005 07:17:00 PM, Anonymous Fred Massawe said...

Nimevutiwa sana na hilo jeshi lililojaa wanaume shupavu wa kiafrika, hususani huyo aliye kuwa kushoto mwa Malik! Hiki kikundi cha Black Panther ni ufunguo mzuri sana wa hatua kwa watu Weusi tunazotakiwa kupiga ili kuukanyaga ukoloni(uwe mamboleo/mambo sasa!) na kuwaamsha Waafrika waliolala kifikra...

 
At 12/16/2005 07:29:00 PM, Blogger Jeff Msangi said...

Ndesanjo,
Binafsi hawa watu wa "New Black Panther" wananivutia sana.Nimewahi kuwaambia rafiki zangu fulani kwamba tufike mahali na sisi tuwe "wabaguzi".Hii inatokana na ukweli kwamba yanapoongolewa masuala ya ubaguzi wa rangi kimsingi watu wanaoongelewa ni weusi na weupe.Na katika hili weusi ndio waathirika.Tumeishia kusononeka tu," jamani waangalieni hawa,wanatubagua wakati sisi hatuwabagui" ndio kilio chetu na zaidi cha weusi wa marekani.Kwa kuendelea kusononeka kwa staili hii kunawafanya weupe waendelee kujiona "kubwa kuliko".Ndio maana unaona hata vitoto kama vile vianamuziki vinapandikizwa hiyo "kubwa kuliko" hewa.Mimi nasema na sisi tuwabague,tuwaambie wao ni wajinga na hawawezi kitu,tuandike historia zetu upya.Wakipata maumivu ya jinsi gani inauma kubaguliwa itafikia mahali watakaa chini na kuongea kwa herufi kubwa.Hivi sasa weusi wamejiwekea mazingira kwamba wao ni watwana na wenzao ni wafalme.Ndio maana unaona watu kama Kanye West ambaye kimsingi anasema ukweli kabisa hawaungwi mkono kwa nguvu inayostahili.Siamini kwamba kesi ya Katrina imeishia hewani tu.Imerudi historia ile ile "jamani mbona hamji kutusaidia?".Unaweza kupata mwanga zaidi kwa kufungua hii http://www.blackpanther.org/newsalert.htm

 
At 12/17/2005 07:30:00 AM, Blogger Indya Nkya said...

Jeff, hilo lingezama vichwani mwa weusi basi ubaguzi ungeisha. Yaani inabidi wakiwa kwetu nasi tuwabague kikamilifu. Wataona kumbe tunawaona nao pia hawana maana.

 
At 12/19/2005 12:28:00 PM, Anonymous Fred Massawe said...

Ndugu Jeff na Idya mnanikumbusha hotuba kali sana ya kuwaonya watu weupe aliotoa Dr. Kamau Kambon ambaye alikuwa mhadhiri wa stadi za historia ya Afrika katika chuo cha NC State University kilichoko kwa Joji kichaka. Hotuba hii ya mwezi wa kumi mwaka huu unaweza kuiona moja kwa moja akiongea ukienda katika hiki KIUNGO. Huyu mtu kunavitu vingi anavyosema nimevitiwa navyo ila maswala mengine ni tata na yanahitaji upembuzi wa kina kuyafanikiwa. Kama kuna mtu anajua habari nyingine njema za huyu bwana nengependa kuzipata. Ndesanjo huyu bwana hukunipa tathmini zako nilipokutonya habari zake, nae ni 'Mwanaume wa Shoka' anaetisha kuondoa kizazi cha watu wote weupe duniani ikiwa ndio suluhisho pekee ye analoliona lilobaki la Mtu Mweusi kuwa Huru!

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com