12/10/2005

Matumizi ya Bendera Kuashiria Lugha kwenye Tovuti

Tovuti ya chama cha Chadema ilikuwa ina picha ya bendera ya Waingereza ikiashiria toleo la kiingereza la tovuti hiyo. Mwanablogu Nkya wa Pambazuko akahoji kuhusu matumizi ya bendera ya nchi nyingine kwenye tovuti ya chama cha siasa Tanzania. Bonyeza hapa usome Nkya alipoandika kuhusu bendera hiyo. Chadema wakakubaliana na Nkya na sasa wameondoa bendera hiyo.
Kuna makala inayoelezea jinsi ambavyo sio sahihi kutumia bendera katika tovuti kuashiria lugha fulani. Huyu ndugu anasema kuwa wakati mwingine tendo hili linaweza kuchukuliwa kuwa ni tusi hasa kama bendera inayotumiwa ni ile ya wakoloni. Bofya hapa usome makala hiyo.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com