12/09/2005

Mkutano wa Wanablogu Uingereza

Jumamosi tarehe 10 ndio siku ya ule mkutano mkubwa unaokutanisha wanablogu toka pande zote za dunia. Majina ya wanablogu watakaodhuhuria unaweza kuyaona ukibofya hapa.
Nitaandika kuhusu mkutano huo moja kwa moja toka katika makao makuu ya shirika la habari la Reuters. Lakini pia unaweza kufuatilia mkutano huo kupitia video ya moja kwa moja ya mtandaoni kwa kubofya hapa. Au bonyeza hapa. Mjadala nitakaoshiriki mimi ambao utatazama maingiliano na mahusiano kati ya uandishi wa habari wa asili na blogu utakuwa ni saa tano u nusu kwa saa za London. Unaweza kujua itakuwa saa ngapi hapo ulipo kwa kubonyeza hapa. Lakini pia unaweza kushiriki kwa kuchangia mawazo kwa njia ya "Internet Relay Chat" (IRC). Kwa maelezo jinsi ya kushiriki kwa njia hii bofya hapa.
Halafu kuna kitabu cha picha ambacho kina baadhi ya picha wahudhuriaji. Bofya hapa uwaone.
Mkutano huo utakapomalizika, kwakuwa tutakuwa tumechoka, itabidi kujimwaga katika jiji la London ili kupumzisha mwili na akili. Ukitaka kufuatilia mapumziko yetu hayo bonyeza hapa.
Siku ya ijumaa baadhi ya wanablogu watakutana kwa chakula cha usiku. Kukutana huko kunafanikishwa kwa kutumia teknolojia ya "wiki." Bonyeza hapa uone.
Mkutano huu umeandaliwa na Kituo cha Intaneti na Jamii cha Berkman. Bonyeza hapa ukitaka kujua zaidi kuhusu kituo hiki. Wengi wa washiriki ni wanablogu wanaojihusisha kwa namna moja au nyingine na blogu ya Mradi wa Sauti za Dunia. Bonyeza hapa kuhusu mradi huo.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com