12/01/2005

Padri Karugengo: Mwafrika Ni Mnafiki au Mjinga?

Jana, katika barua pepe ambayo Mrisho Mpoto aliandika kwa watu kadhaa alisema kuwa Waafrika ni kama kituko vile. Tena ni wanafiki. Bonyeza hapa usome kuhusu barua hiyo kisha ndio uendelee na ujumbe wa leo toka kwa Padri Karugendo (ambaye makala zake zitarudi hapa kwenye blogu, pamoja na zangu, wiki hii).
Basi Padri Karugendo anauliza swali zuri sana. Soma waraka pepe wake aliotuma kwa watu wale wale Mrisho aliowatumia:
"Wanafiki au Wajinga. Mrisho Mpoto, anasema sisi niwanafiki, lakini mimi ninafikiri alitaka kusema sisini wajinga? Labda ninayaweka maneno haya midomonimwake, lakini ningeomba tujiulize juu ya unafiki naujinga - mnafiki na mjinga, ni nani wa kukwamisha maendeleo ya nchi yetu? Na kudai pesa mtu ili umjadili ni unafiki au ni ujinga? Mtu kuiuza nchi ni unafiki ama ni ujinga?"
Mbarikiwe,Padri Karugendo.

5 Maoni Yako:

At 12/01/2005 06:40:00 PM, Anonymous Anonymous said...

Ni naogopa sana kama mwafrika ni Mnafiki. mjinga na mnafiki mimi ningempendelea mjinga. kwa maana mjinga anafundishika. Ila mnafiki inamaanisha anajua anachofanya. Na kama kaamua kuomba pesa kwa wazunguu ili wamsaididie ajikwa mue kutoka kwa wazungu kinafiki inamaana haitaji kujikwamua. lakini kama ni mjinga basi ni kweli anajitahidi kujikwamua. Kumbuka playing fool fe get wise inawezekana pia.

 
At 12/02/2005 02:33:00 AM, Blogger mloyi said...

Mnafiki, mjinga Miaka ya sabini kwenye essay yake ya kuombea digrii ya kwanza pale mlimani au pale kivukoni college alikataa kuingiliwa ma mzungu, lakini leo sijui huyo mzungu amebadilika kuliko matatizo ya afrika, anakimbilia huko kuomba misaada.
Utandawazi unakuja, ndio ni sera za kibeberu, hatutaki kuzikwepa ingawa zinakwepeka Hatatutaki kukubali kwamba Urusi imeanguka na tumekuwa yatima tujitegemee tusihamie kwao wale tuliowapinga miaka yote.
Angalia ukingani uliopo hapo juu uamue ni mjinga au mnafiki?

 
At 12/02/2005 03:08:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Kuuliza si ujinga bali ni katika kutaka kujua...."Hivi Ndesanjo"...wewe na Fredy Macha ni nduguuuu!!! au ni majina na sura tuu?

 
At 12/02/2005 03:16:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Kuuliza sio ujinga na pia sio unafiki! Ndio, mimi na Freddy Macha ni ndugu. Ukipenda kutembelea tovuti yake hii hapa: http://freddymacha.com

 
At 12/03/2005 05:44:00 AM, Blogger nyembo said...

KWA HILI LA UJINGA NA UNAFIKI, KIMOJA NI CHANZO CHA KINGINE...UJINGA NI MZAZI WA UNAFIKI,NI ROHO NA KIASILI MZIZI CHA UNAFIKI..PENGINE NI RAFIKI KAMA MAMA NA DADA AU KAKA NA BABA NI ADUI WA BINADAMU NI MZIZI WA TAWALA ZA AFRIKA,NI SUMU SUMBUFU KWA JAMII YETU,NI UVIVU WA KUFIKIRI WA WAFALME WA ENEO LETU,NI USHAMBA WA KISASA WA WAFLME
PIA NDIO UKISASA WA MABWANA NA UPUUZI KWA WATWANA NI UMALUUNI UHUNI NA USHETWANI KUUENDEKEZA NDESANJO

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com