11/30/2005

Mrisho: Mwafrika ni Kama Kituko!

Msanii wa nguvu na rafiki yangu wa karibu, Mrisho Mwana wa Mpoto, wa kundi la Parapanda, ambaye niliwahi kuandika habari kuhusu harusi yake ambapo "shampeni" ilikuwa ni maji ya madafu (bonyeza hapa uisome) kaandika ujumbe ambao umenichekesha ingawa aliyosema sio utani. Anasema kuwa Waafrika ni kama kituko vile. Usome. Naubandika hapa chini:
"Mwafrika nikama kituko maana wanaomba Funding kwa wazungu ili wajadili matatizo yao na jinsi ya kujikomboa toka utumwani sasa icho si kituko yaani mtu akupe pesa ili umjadili yeye alafu unachekelea. Huwezi kubisha .....(hapa Mrisho kataja jina la mtu ambalo nimelitoa)... Maana juzi tu tulikuwa zanzibar kujadili ujinga wetu mbele yao huku wakitulipa pesa na kulala sehemu nzuri huku tukiomba siku ziongezwe hata bila posho."

All the Best
Mrisho Mpoto
********************
Huyo ni Mrisho Mpoto, wewe unasemaje kuhusu kuomba fedha kwa wazungu ili tujadili jinsi ya kujikwamua toka kwenye makucha yao ya uchumi, fikra, siasa, na utamaduni tegemezi?

3 Maoni Yako:

At 12/01/2005 01:29:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Huyo Mrisho ni sawa na kuku anayetambua kuwa "kajengewa nyumba ya matofali tena yenye umeme, analishwa chakula milo 20 kwa siku na kupewa maji muda wote, anatibiwa na mtaalamu wa mifugo na kulindwa na kampuni ya ulinzi asishambuliwe na fungo na majambazi; kuwa ni mbinu tu za huyo mfugaji kujitayarisha kumtafuna vizuri". Basi ina maana moja tu, upeo wa Mrisho ni mkubwa. Siyo kama sisi tunaoona lugha kama mawasiliano, bendera kama kitambaa yenye mirangirangi, dini kama imani na olimpiki kama michezo. Inaonekana hakuwa msanii kwa kubahatisha. Na wala hana bahati ya kuwa msanii, bali taasisi ya sanaa ina bahati kumpata mtu kama yeye. Hilo jambo alofanya lina maana kubwa sana kwa jumuiya yetu na Afrika nzima, na anastahili tuzo. Na ingekuwa pengine pale basi vyombo vya habari vya nchini vingelilivalia njuga suala hilo maana hayo ndo mambo ya kufanya Mwafrika katika dunia ya utandawazi kwa manufaa ya wananchi. Kwenye harusi umepambwa na viatu, shela, suti, pete, dawa za nywele, leso, magari, matarumbeta; hata moja ya vyoooote hivyo havijatengenezwa nchini kwako au havijatoka kwa mmoja wenu wananchi ------ hizo tunazodhani ni harusi sizo, ni biashara.

 
At 12/01/2005 02:23:00 AM, Blogger mloyi said...

hata nyati alipomcheka ng'ombe kwamba anakosa amani kwa kujiweka kwa binadamu, ng'ombe alijiona bado ni bora kuliko nyati, lakini aliishia kukatwa shingo na kisu cha huyohuyo binadamu.
Mrisho anatuambia kitu cha ukweli lakini sisi tunakuwa wabishi au tunaendeleza falsafa yetu ya chukua chako mapema na huwa wanapata wanachotaka kwa kiasi walichoombea kwa miungu yao! ila je huwasaidia walioombewa hiyo masaada? Tusiwe kama ng'ombe kujipeleka machinjioni tuwe kama nyati ingawa pia huishia mezani lakini inabidi umtafute kwa juhudi na maarifa kumpata.

 
At 12/01/2005 06:43:00 AM, Blogger Innocent Kasyate said...

Mimi nina kibwagizo changu "TUMEKWISHA" hii ndio hisia yangu manake naona siku hizi kwa mfano wanasiasa kama una sera za kutetea maslahi ya nchi yako nakwambia hufai.
Ndio maana watwawala wetu wanafurahia ubinafsishaji kweli.
Wajinga ndio wali wao. Huku Afrika ukiwa na mawazo ya akina Mrisho unaonekana mshamba kweli.
Akina Mrisho ni watu hadimu hatunao tena tufanyeje sijui.

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com