11/30/2005

Mwalimu Alikuwa ana uwezo wa kuona kuleeeeee...

Kituo cha Kusini kina mradi wa tovuti ya kumbukumbu ya Mwalimu. Baadhi ya hotuba zake zinapatikana kwenye tovuti hiyo. Nimemaliza kuzisoma. Mwalimu alikuwa ana namna yake fulani ya kufikiria...ila katika yote ni ule uwezo wake wa kuona mbele kuleeeeeeeeee....wakati wa-twawala wengi tulionao hata leo hawaioni (sembuse kesho). Bonyeza hapa uzisome.

2 Maoni Yako:

At 11/30/2005 06:35:00 AM, Blogger msangimdogo said...

Pua zao zimekuwa ndefu sana hivi sasa sawa na wale jamaa ambao Mtikila anawapiga vita, unadhani wataweza kuona huko kweli, na hata wakiona hawawezi kwenda maana wataanguka, matumbo yao pia ni makubwa sana kiasi kwamba hawaoni hata wanapokanyaga, ndio maana daima wamekuwa wakichomwa na mbigiri (sijui kama unazikumbuka)

 
At 11/30/2005 07:21:00 AM, Blogger Boniphace Makene said...

Wamelewa wale na wamejigeuza wafalme, tangu lini mfalme alipata kuwaza na kujua yatakayotokea kesho? Hadi siku watakapogeuka kuwa wananchi ndipo fikra zao zaweza funguka na kukaribishwa Kasirini.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com