Nitablogu Toka Uingereza Mwezi Ujao
Kama kuna mtu ana mpango wa kujilipua ndani ya treni au mabasi pale London kwa Malikia Lizabeti, namshauri asithubutu kufanya hivyo mwezi ujao. Mwezi ujao nitakuwa yaliyo makao makuu ya shirika la habari la Reuters, Canary Wharf, London. Nitakuwa hapo kwenye mkutano wa pili wa kila mwaka wa Mradi wa Sauti za Dunia. Mradi wa Sauti za dunia uko chini ya Kituo cha Berkman cha Intaneti na Jamii katika chuo kikuu cha Harvard. Habari zaidi kuhusu mradi wa Sauti za Dunia ulivyoanza na pia kuhusu mkutano wa London mwezi ujao na watu wanaohudhuria, bonyeza hapa. Utaona kuwa kati ya wanaohudhuria ni wanablogu wawili mahiri wa Kenya, Kenyan Pundit na Mshairi. Mshairi huandika habari kuhusu wanablogu wanawake wa Afrika kila jumatatu katika blogu ya Sauti za Dunia.
Kwahiyo wasomaji wangu, ndugu, na marafiki wa Uingereza, tuwasiliane ili tuweze kunywa chai na kupiga gumzo (Masawe, Maruma, Kibwana, Mgosi, Theodore, Freddy, Neema (JALO!!!) ...mpo?).
3 Maoni Yako:
Karibu sana Ndesanjo nina "uchu" sana wa kuonana, kuongea ana kwa ana na mengineyo mengi! Mapambano na Uhuru
natumai utatupa mambo mengi toka huko,lakini usisahau kumtafuta na kumpata mzanzibar yeyote huko aliyeandama kupinga uonevu katika matokeo zenj ili akupe walau muono wake na kisha upanue katika mawazo yako kabla ya kuuleta barazani...safari njema na uwajibikaji wa kina
Massawe, safari hii lazima tukutane na kupanga mikakati. Mapambano yanahitaji kupanga.
Hivi unawasikiliza jamaa wa Midnite? Kama huwasikiliza, basi unakosa mengi.
Post a Comment
<< Home