11/14/2005

Mafisadi wale wale, Chama kile kile, uozo ule ule...

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinafanya kampeni kwa kutumia barua pepe. Nimefurahi kujua hili maana haya ndio kati ya mambo ninayotazama kwa karibu (kwasababu za kitaaluma). Ninaamanisha matumizi ya zana mpya za mawasiliano katika kampeni za urais na ubunge.

Kuna mistari ambayo iko katika barua pepe yao ambayo nimeona niwagawieni kidogo (iwapo hujapata barua pepe hiyo). Nabandika hapo chini mistari hiyo:

Maendeleo ya Kweli
hayawezi kuletwana
Mafisadi wale wale
wa Chama kile kile
chenye Uoza ule ule
Wakiendeleza yale yale
eti kwa Kasi mpya,
Nguvu mpya
na Ari mpya.

2 Maoni Yako:

At 11/18/2005 05:22:00 AM, Blogger nyembo said...

kaka nimeona,ujumbe wa kisiasa kutoka Chadema,nashukuru kuwa nimeusoma kupitia blog yako.
katika blog nyingi nilizoangalia yako na ya msangi hunifurahisha sana hongereni,
Nachoweza kusema kwamba yaliyoelezwa pale ni sawasawa,lakini yapi wao watafanya mapya...nanije Leo Kabourou ni makamu M/kiti wa Chadema,aliletwa nchini na Ccm kwa ajii ya kugombea ubunge jimbo la Kigoma Mjini,leo ni mtuwa cheo cha juu katika chama....angekuwa Ccm hadi leo nae angekuwa Fisadi?...muhimu ni kuangalia kuna mafisadi wenye fikira isiyo ya kifisadi kama Kabourou,wapo wengi tu...na katika chama kile kile,lakini wana uoza tofauti,na wanayoendeleza ni tofauti kidogo lakini wanahitaji kuwa hapo kwa kasi mpya nguvu mpya ari mpya....
Hapa ndio naweza kusema sio tu checheme (ccm)wenye tatizo la Mafisadi bali vyama vyote vya tanzania kwa kuwa havina dira wala mlengo si wa upande wowote,
hata Mungu aliweka fisadi pamoja adamu na eva...sahemu moja wale hawakuwa mafisadi,tatizo ni chekecha la kuondoa hawa mafisadi na kubaki walio safi(kazi kubwa hiyo)Mungu aliwatupa washikaji wale Duniani..lakini wapi mzee wa kazi shetan akwanyatia hadi huku
Macha nimesoma makala zako nyingi kwenye Mwananchi j2,lakini kwa huu ujumbe wa Chadenma leo naomba uwe na akili kama mwendawazimu.....
nakukaribisha kupitia kwangu pia kwa kuwa bado ni kijaa mbichi kwenye mambo haya ya kublog nahitaji fikra pevu..asante nimejadili ujumbe.....nimezungumza nani wa kujibu ili tuingie katika ukamili wa mazungumzo,

 
At 11/19/2005 08:29:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Nyembo,
Asante. Nimeshakaribia. Nakubaliana nawe kuwa mwanasi-hasa akiwa mpinzani haina maana kuwa basi ndio atakuwa anaweka maslahi ya umma mbele pale atakapochaguliwa. Tuna mfano hai wa wabunge wa upinzani ambao wamekuwa ni wabovu kuliko hata wale wa chama cha chukua chako mapema.

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com