11/10/2005

Yanayotokea Ethiopia je?

Sijui kama wandugu mnafuatilia yanayotokea kule Ethiopia. Bara letu litavuja damu hadi lini? Kumbuka Mwizi Mkuu, samahani, Waziri Mkuu wa Ethiopia alikuwa ni miongoni mwa wa-twawala wa Afrika waliokaribisha kule Usoti kupiga picha za pamoja na wa-twawala wa Kundi la Nchi Nane (G8). Mkapa naye alikuwemo. Eti hawa ndio wa-twawala toka Afrika vipenzi vya akina Joji Kichaka na timu yake. Bonyeza hapa usome kwa kina wanablogu wanavyotupasha maafa yanayotokana na maguvu ya dola.

2 Maoni Yako:

At 11/10/2005 05:39:00 AM, Blogger Indya Nkya said...

Moja ya sifa za kazi ya kiongozi mkuu wa nchi ni lazima uwe hodari wa kumwaga damu!! Hakawii hata kusema mbona Iraq wanakufa kila siku? Si ulimsikia yule wa kwako akisema kwamba hakuna shida kwa wanajeshi kutawanywa Zanzibar kama ilivyokuwa Iraq wakati wa kupiga kura.

 
At 11/11/2005 03:14:00 AM, Blogger mloyi said...

Kwanini ni Afrika tu?. Mbona joji kichaka aliiba kura na watu wake hawakufanya "vurugu" yeyote?. Inakuwaje waafrika inawauma kiasi hiki kwa kudhania wameibiwa kura? Tuliangalie hili kwa makini.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com