11/06/2005

Maisha Dasalama Magumu Unaweza Kunywa Sumu

Ferdinando Paul ni mmoja wa wasomaji wa makala zangu katika gazeti la Mwananchi. Yeye ni msanii wa muziki wa rapu. Kanitumia zawadi ya beti chache toka kwenye moja ya mashairi yake. Nami nawapeni nyote zawadi hiyo. Kwenye waraka wake anatuambia kuwa maisha Dasalama ni kama jehanamu ya kufa na kupona! Hapo chini ni sehemu ya waraka wake na beti (ameziita "vesi" zenyewe):

Tunakupa hi sana masela wa bongo. Si unajua darisalam maisha magumu mithili ya jehanam ni kufa na kupona yani unaweza ukanywa sumu. Hizi ni baadhi ya vesi zangu. Mimi ni msanii wa kurap nina misongi mingi lakini ndo hivyo mambo tight ngoja nikupe vesi hii kidogo:

Nanuka dhiki
Sina kipato mwendawazimu
nakuwa sina rafiki
ila wafitini na wanafiki
kwa kuwa ni masikini
nimezungukwa na wazindiki
lakini bado naamini
mwenyezi mungu atanibariki
hivyo nakuwa makini
nahangaika riziki popote na simwamini mtu
walimwengu hawaaminiki
na tena hawariziki
nikipendeza wanakuwa wanoko
wanataka nivae kaniki
maisha niwe mshabiki
wakati haiwezekani
mwendawazimu sibadiliki
- Ferdinando Paul

3 Maoni Yako:

At 11/07/2005 05:23:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Msanii jina Ferdinando Paul, unatoa HI, msanii wa ku-RAP, unasema ..... mambo TIGHT, ....unatoa VESI, mh... makubwa. Huyo ndo msanii wa Tanzania, kioo cha kuendeleza na siyo kupotosha jamii, balozi wa nchi popote duniani. Kitu kidogo tu, iweje U-rap? wakati tuna makabila zaidi ya 120 nchini yenye utajiri wa sanaa mbalimbali na ya hali ya juu, na huko ulikonuukuu rap pia wanalijua hilo. Sasa ukienda nje na ukacheza rap utadai kupiga muziki wa Tanzania au. Maisha Dasalama siyo jehanamu, wapi ni peponi? Arusha, Mza, Tanga, eh.. au unalinganisha na wapi?. Nadhani Dar siyo mahala pa rap ila pa mahadhi ya madogoli, sindimba, bhughobhoghobho, mdumange, n.k. Pia ni kwa wale waliyeko hapo na si kwingineko kwa mwili, akili na fikra zao. Hivi hi, mambo tight na vesi ndiyo nini? ... msanii, balozi wa nchi!!!!!. Hongera Kingwendu, Saida Karoli .....

 
At 11/08/2005 05:16:00 AM, Blogger mloyi said...

Nani anamtenga? mbona sote uswahilini ni masikini! anandoto gani? na yeye akifa apelekwe kuzikwa na ndege ya sirikali? au gari la sirikali likamchukue shuleni kama wale anaowazimia? hajiamini nini? Labda hajui anachoimba ilimradi anamdundo na watu wanafurahia tu basi na yeye ni mwanamuziki, sijui tofauti ya mwanamuziki na DJ, au uwendawazimu wake ndio unamsumbua?
Wapo wengi wa hivyo, kama Mr. Temba anakaa kuimba alivyofanikisha azma yake ya ngono kwenye wimbo wa nampenda yeye na watu "wote" waliufurahia. Sijui anazania kile kilikuwa ni kitu cha sifa!
Unajua watu hawa huwa hawaishi Tanzania, ingawa wapo Tanzania siku zote! Anaona kwa sababu hayupo jirani na JLO basi ametengwa.

 
At 11/08/2005 08:03:00 AM, Anonymous Anonymous said...

hapana jamani mloyi kachanganyikiwa hebu muangalieni kwa ukaribu yaani ni kituko anachekesha sana azma ya ngono!!!!! yaani tuache tuu. inachekesha.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com