10/30/2005

Hivi ukawapa watoto vijijini kompyuta bila mafunzo itakuwaje?

Mradi wa The Hole in the Wall ndio unachofanya. Hawa jamaa wanachukua kompyuta, wanakwenda maeneo ambayo watu hawajui na hawajawahi kuona kompyuta, kisha wanawapa watoto kompyuta bila kuwapa mafunzo yoyote. Swali ni kuwa ukimpa, kwa mfano, mtoto wa kijijini kompyuta, ataifanyia nini? Bonyeza hapa uone yanayotokea unapowapa watoto kompyuta bila kuwaambia cha kufanya.

1 Maoni Yako:

At 10/30/2005 06:09:00 AM, Anonymous Anonymous said...

hichi ni kisa cha kama wale wa canada waliopeleka matrekta ya kulimia kwa watanzania bila ya kuwaonyesha ni jinsi gani ya kuzi fanyia trekta hizo matengenezo ikiwa zimepata kuharibika kidogo watu hawakujua nini cha kufanya basi trekta zimeharibika zikaa kaa tuu zimeoza. si unajua hawa wazungu wanamatatizo ya akili alafu wanajifanya wao wanaakiiili na kuziambia nchi wanazozipa misaada ni sawa na wanawake wajawazito eti utumie uume wako kumpa mimba, ulee mimba, umpeleke leba siku ya kujifungua, na akisha jifungua umlele mtoto. kwanza nani anawaomba msaada kama si kimbelele chao watu hawataki misaada wanataka wafanye biashara kwa sababu mali wanazo kila kitu cha kufanyia biashara wanacho. ila huo urasimu wao na eti wanachokiita standards ndo wanawekea watu usiku. hzo komputa ni zile za dola 100 nini ambazo wanasema wanatengeneza ili wapeleke huko kwa wanaowaita masikini nini???

Au unakumbuka mradi wa global fund ulivyoipa Tanzania mabilioni ya dola ili iweze kupambana na Ukimwi malaria na Tb. Tanzania ikanunua vyandarua hebu jiulize hivi vyandarua vitadumu kwa muda gani?? ninaimini vingi mpaka sasa vimeisha na unavyojua watanzania wanavyopenda kufua!!!!! hivi kwa nini serikali isingechukua ndege zao wakanunua dawa za kuua mbu wakamwaga dawa kwenye vina vyote vya maji machafu na kila mahali uoni hapo tungemaliza mchezo kuliko vyandarua si unajua tena hapo na wale wanaotaka kuiba hizo pesa. mimi hata na choka sijui nasema nini tena hadi na changanya maneno maudhi ni mengi sana kwakkweli.

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com