Pop!Tech: Huyu jamaa anaongelea kitu gani?
Tumetoka kwenye chai na mandazi ya kizungu. Neil Gershenfeld wa Taasisi ya Teknolojia ya Massachussetts (MIT). Sielewi kabisa anaongelea kitu gani. Ninajisikia kama vile niko darasa la Fikizia la mwalimu Mashingia pale sekondari ya Mawenzi. Mashingia ni yule mwalimu aliyetazama mwandiko wangu siku moja na kusema, "Wewe kijana mwandiko watu tu unaonyesha kuwa hesabu zinakupiga chenga." Da, hapo ni kidato cha pili. Maneno yake yalikuwa ni kama unabii kwani kwenye mtihani wa kitaifa wa kidato cha pili nilipata 11 kwenye hisabati. Nkya, usicheke!
Haya, Neil anaongea. Labda ili uelewe kwanini sielewi, soma kuhusu utafiti anaofanya pale MIT kwa kiingereza, sitaki wala kujaribu kutafsiri):
"His unique laboratory investigates the relationship between the content of information and its physical representation, from molecular quantum computers to virtuosic musical instruments."
Labda pia majina ya vitabu alivyoandika vitakupa picha ya tabu ninayopata kumwelewa anazungumzia mdudu gani. Hivi ndio vitabu vyake:
When Things Start to Think, The Physics of Information Technology, na The Nature of Mathematical Modeling (hasa hiki cha mwisho!!!).
Pale MIT anapofanya kazi kuna watu wanafanya utafiti ambao ukielezwa unaweza usiamini. Katika maabara za MIT, wana msemo mmoja. Wanasema kuwa kama jambo linasemekana kuwa haliwezekani, basi jambo hilo ndio watataka kulifanyia utafiti na majaribio.
2 Maoni Yako:
e bwana macha poa sana kaka nafagilia sana articles zako niko hapa chuo kikuuu cha dar es salaam.
endelea hivyo hivyo kutupa habari za huko na kuweka mambo bayana
gaston amosi
dsm
haki ya mungu umenichekesha sana hicho kisa cha mwalimu wako, kwakeli hesabu duuuuu hapana si wewe peke yako. yametusibu wengi
Post a Comment
<< Home