10/29/2005

Fide anashangaa waliombeba Livingstone bado wapo

Fide Tungaraza anasema kuwa alidhani kizazi cha Watanganyika (ambao pia huitwa Wadanyanyika) walibeba maiti ya Dakta Livingstone toka Kigoma hadi Bwagamoyo kwa miguu kilikwisha. Kwanini anasema hivyo? Soma waraka wake hapo chini:
Mimi nilifikiri kizazi cha wale Watanganyika waliombeba Dr Livingstone tena akiwa kafa kilikwisha! La hasha! Kumbe wajukuu zao bado tupo na tunaendeleza waliyoyafanya! Nilipokuwa Chuo cha Sanaa Bagamoyo nilikuwa nikienda kanisani na kutazama pale mahala waliposimama wale Watanganyika waliombeba mfu Dr Livingstone na kuwaambia wazungu wenziye kwamba "..Bwana amefariki.." Nilikuwa sipati majibu kwamba: Wale Watanganyika walikuwa na utu sana? Au walifanya vile kwa sababu walikuwa wanataka walipwe mishahara, marupurupu, mafao na pensheni zao kwa kukileta kidhibiti cha maiti? Au walimpenda sana Hayati Dr Livingstone? Au walikuwa wafanyakazi watiifu na waaminifu kwa mwajiri wao? Au walikuwa kama Waswahili wasemavyo mafala? Au walikuwa wapumbavu kupindukia? Au kama uchawi upo walikuwa wamelogwa?

Siku zilizopita nilikarahishwa na habari kama hii kwenye gazeti la Dar Leo
(http://www.bsctimes.com/). Habari hiyo ilikuwa na kichwa cha habari ASKARI WA KIINGEREZA WAUA CHANGUDOA. Habari hiyo niliituma kwa baadhi yetu na kwa Mheshimiwa Waziri Omar Mapuri na Balozi Abdulkadir Shareef ili kwamba ichukuliwe hatua. Sijui kama kuna hatua iliyochukuliwa. Leo nimekumbana tena na habari za kabila hiyo hiyo yenye kichwa cha habari MCHINA AMTWANGA 'HEDI' MBANTU NA KUZIRAI. Kuna tusi limenijia lakini nalihifadhi, hivi ingekuwa MBANTU KAMPIGA 'HEDI' MCHINA NA KUZIRAI ndani ya mitaa ya Beijing huyo Mbantu angekuwa hai mpaka saa hizi? Leo imenipasa kusema kwamba wajukuu wa wale Watanganyika bado tupo baada ya kukumbana na taarifa hii kwenye gazeti la Nipashe (

2 Maoni Yako:

At 10/30/2005 09:53:00 AM, Anonymous Anonymous said...

hivi ninyi nani aliwaambia Mapuri ana akili stahili, yule bwana ni mtambo wala usihangaike kumtumia chako chochote mimi kila siku kicwhani kwangu nasema kama kuna nchi inahitaji mapinduzi ni Tanzania jamani hapa kumeoza kama mti anaweza kuwaibia na yuyuko hapohapo nchini na hakuna mnaloweza kufanya kulalamika huyo anayetoka nje ndo mtamfanya nini??
mtabaki kusemea vibambazani tuu.hii nchi haina haki jamani ni mengi yananyo endelea hakuna wakumpa mwenzake maji. watu wananyang'anywa mali zao mikoni. wewe unasema mambo ya changudoa tuu ghaa (sijasema huyu si binadamu, na hastahili kufanyiwa loloye bila ya ridhaa yake), hivi umeshafati;lia kisa cha pale Ashanti Mines yule kijani alivyopighwa puu na wale wazungu mpaka leo, na wale wachimbaji kule mererani waliopigwa risasi za ndege kesi ikaishia tuuu hivyo hivyo si unajua tena huyo fupi nyundi yaani mkapa anashea na hao wazungu sijui kawaambia na mkitaka kupiga watu virungu kuwanyonga kuwabaka fanyeni tuu hii pesa yenu inatisheleza kabisa. kwa hiyo wazungu wachina waarabu na je kile cha kule loliondo umefatilia weeeee Tanzania inasikitisha tumemalizika hebu tokeni huko mliko jamani angalau tuisaidie nchi tumekwisha.
yaaani ni kama hawa jamaa wakiomba visa ya kuja kuitembelea Tanzania wanaambiwa hii visa yako inakuruhusu kubaka, pamoja na kutenda maovu mengineyo yoyote hakuna atakaye kufanya lolote hiyo ni nchi ya mandindicha kwanza wakiona ngozi nyeupe wanaiabudu..

 
At 11/01/2005 08:24:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Kwa maoni yangu mimi nadhani sisi Watanzania tumekuwa tunaziabudu sana rangi nyeupe na mpka sasa siujui ni kwa nini na lini tutaacha upumbavu huu, matukio kama haya ni mengi yanatokea hapa tanzania lakini na hata ukienda kwenye viombo vya sheria huwezi kupata msaada zaidi ya kuambiwa wewe ndiye mkorofi ni si ajabu ukambiwa ulitaka kumuibia huyo mtu. Mambo kama haya yatokea sana kwenye mahoteli, makampuni yanayomilikiwa na wazungu hasa kupiga wafanyakazi wanapokosea. Hata vyama vya wafanyakazi hapa Tanzania havina maana kwa sababu haviwezi kutetea maslai ya wafanyakazi. Viongozi wenyewe wanawaabudu hawa watu, kwa kweli haya matukio kama yote yangekuwa yanaripotiwa basi ingefika ni aibu tupu nina mengi ya keleza lakini wacha niishie hapa.Nashukuru sana kwa wote mnaofuatiria mambo yanavyokwenda hapa Tanzania nafikiri itafika siku tutapata mahala pa kusemea machungu yetu.

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com