10/29/2005

Wawekezaji, waezekaji na "nunueni vya nyumbani"

Bwana mmoja kanitumia makala moja kiboko. Anazungumzia hadithi ambayo Watanzania tumekuwa tukipigiwa na wezi wa kalamu. Wezi wa kalamu ni watawala. Fela Kuti ana wimbo anasema kuwa wezi wanaotumia silaha wasitutishe kama wezi wa kalamu. Unajua mwizi wa silaha anaweza akaenda dukani kwa Mangi akaiba na kuua watu wawili. Wezi wa kalamu walioko madarakani wizi wao unaua taifa zima.
Basi makala hiyo inazungumzia hadithi ya toka mwaka 1973 ya kuhamia "makao makuu" Dodoma. Makala hiyo itatoka kwenye blogu mojawapo za Kiswahili karibuni kwahiyo sitaizungumzia. Nilichotaka kusema ni kuwa ndani ya makala hiyo huyu bwana hataki kuita wakoloni wapya "wawekezaji." Anawaita "waekezaji." Anasema kuwa kazi yao wakoloni hawa, wanaoshirikiana na akina Mangungo wa Msovero wa siku hizi ambao wanaishi kwenye jengo lenye kuta nene kuliko gereza la Ukonga, ni kuezeka kwani Watanzania tayari tumejenga. Kwahiyo jina lao ni waekezaji.
Makala hii imezungumzia suala la Watanzania kutopenda vitu vyao. Hii inanikumbusha jambo moja linalokera sana. Utasikia wakati fulani Rais Mkapa akiwataka Watanzania kujenga tabia ya kununua bidhaa za Tanzania. Ajabu ni kuwa wakati Mkapa anasema hivyo kila kitu mwilini mwake kuanzia anjifu/leso, tai, viatu hadi nguo ya ndani (kinasa) vimetoka kwenye nchi za viongozi anaopenda sana kupiga nao picha. Ukienda pale ikulu huoni vitu vya Tanzania, hata mapambo...sasa anapotuambia tununue vya Tanzania anakuwa anatutania au? Sio Mkapa tu anayefanya hivyo, hotuba za kuwataka Watanzania wanunue bidhaa zao hutolewa mara kwa mara na watu mbalimbali.
Huenda watawala hawa wanaohubiri wasichofanya wanaiga kwa wahubiri wa kidini wanaosema, "Fuata ninayohubiri sio ninayotenda." Unafiki wa-hedi!

2 Maoni Yako:

At 10/29/2005 08:33:00 PM, Blogger Jeff Msangi said...

Ndesanjo,
Anachokifanya Mkapa na ndumilakuwili wengine ni unafiki,utumwa wa akili,upuuzi,ushetani,ukuda,ukosefu wa maadili,@##%%&&*^)(&()(_)&*^%$%$### na kila kitu.Nimekasirika,umenikumbusha ukweli mbaya kuhusu unafiki huu!

 
At 10/30/2005 10:15:00 AM, Anonymous Anonymous said...

kwanza anahamasisha wawekezaji ili aweze kutuibia zaidi unajua yule jamaa ni kibaka, alafu akapata na yule mwenzake jambazi sugu. wameshatuuza Tanzania kwanza hata kuna nini tena cha kununuliwa Tanzania, zaidi ya kuwakejeli hawa kina mama masikini ya mungu ambao wameanzisha vibiashara vyao vidogo vidogo ili wafikirie ee Mkapa kasema hivi lakini kwa hiyo achali yangu itanunuliwa au mashati yangu hamana kitu anasema hivi ili watu tuu wafikiri chama tawala kinatufanyia kazi jamani kwa hiyo kinastahili kura zetu si ndo maana kwenye mkutano Bono akamwiya kibaraka wa Bush na Blair kwa sababu bado ni mtumwa wewe mtu unayedai nchi yako iko huru, mbona kila tunachikuambia unafuata na unakubaliana nacho huna unalokataa hata moja we ni kufuata tuu na kutunisha mashavu, na wakikuangalia unakuja kuomba msaada wakati umeulamba suti designer cheni kubwa viatu nini si wanakuona huyu jamaa badi antuhitaji pale nchini kwake, kwa mavazi yake kwa shida zake kila kitu. ngija turudi kuchukua nchi kiulaini kuekeza, yaani hiki ki mtu ni kifasiki, fisadi, yaani hii ni mbegu mbaya.
Lakini ni hivi watanzania wanavyopambazuka vita vitatoke jamani. hawa watu wameshatowesha amani. baasi tuu ni vile vuguvugu ndo linaaza ngoja paanze kuchemka.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com