10/26/2005

Napumua

Baada ya siku kadhaa za pilikapilika za mkutano katika mji huu mdogo (pichani) wa Camden, ninapumua. Mji huu wa ajabu sana. Siku ya mwisho ya mkutano wa Pop!Tech (ambao hufanyika kila mwaka, kwa miaka tisa sasa), hoteli, migahawa, lojingi, n.k. hufungwa. Mimi na rafiki yangu, Denver Hopkins wa ThoughtFarm, tulikwenda kula chakula cha mchana hoteli moja siku ya mwisho wa mkutano. Tunafika pale tunakuta wenye hoteli na wafanyakazi wanajichana. Wakatukaribisha na kutuambia kuwa siku hiyo ni mwisho wa biashara hadi baada ya miezi sita kipindi cha baridi kitakapomalizika. Ninapokaa mimi na anapokaa Denver napo wanatia kufuli. Hoteli nyingine walitia kufuli toka asubuhi. Mji huu hasa ni wa jamaa wenye nazo wanaokuja kupumzika kipindi cha majira ya joto. Jamaa mmoja wa Google ambaye nyumbani kwake kila jioni kulikuwa na tafrija ya kukata na shoka, yeye hukaa kwenye nyumba yake hiyo mwezi mmoja kwa mwaka. Camden ni ile miji Marekani ambayo imejaa watu wenye siasa za mrengo wa kulia, wenye pesa, wenye kupenda kuchangia pesa zao kwenye miradi ya maendeleo. Ni miji ile isiyo na uhalifu...sikuona polisi hata siku moja. Ni miji ambayo iko kama vile kisiwa, ukikaa hapo unaweza kudhani kuwa Marekani ni mbinguni...toka kidogo uone.

Napumua.


2 Maoni Yako:

At 10/27/2005 08:25:00 PM, Blogger Jeff Msangi said...

Ndesanjo,
Ahsante kwa ujumla kwa yote uliyotupatia kutoka Maine kwenye mkutano wa Pop!Tech.Mwenye macho,masikio na akili haambiwi ona,sikia wala tambua kuhusu umuhimu wa tekinolojia katika ulimwengu wa sasa na habari.Maine pamenivutia,itabidi nipatembelee siku za hivi karibuni.Ahsante

 
At 10/28/2005 06:16:00 AM, Blogger Rama Msangi said...

Ni sababu ya utamaduni wa kudai kila kitu tumeiga kwa wazungu (magharibi), poengine ndio maana kiasi nilishangaa kusikia unapumzika, lakini kumbe hilo si suala la kuiga bali ni muhimu. Nadhani hata hawa jamaa zetu wanaogombea ulaji kwenye SIHASA za hapa DANGANYIKA wangekuwa na utamaduni wa kupumzika bilashaka wangekuwa na akili waingiapo kwenye MIKUTANO ya Bunge...lakini wanaingia wakiwa wameshachoshwa na kusema uongo ndio maana wanaishia kuligeuza Bunge sehemu ya MIVUTANO
Pumzika kaka

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com