10/30/2005

TANGAZO: MUHIMU NA HARAKA SANA

Kuna nafasi za kuhudhuria warsha kuhusu matumizi ya programu huria za kompyuta kwa wanaharakati wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya wanawake. Barua pepe iliyonitaarifu kuhusu warsha hii sikuifungua mapema. Washiriki wa warsha hii (hasa wanawake) watagharimiwa kila kitu. Tarehe ya mwisho kuomba kushiriki ni tarehe kwanza/mosi mwezi wa 11 (Novemba). Ingawa siku zimebaki chache, fomu yenyewe inauliza maswali machache sana.
Kama uko kwenye shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala ya wanawake au unafahamu mtu yeyote, tafadhali chukua hatua ya kuomba au kutaarifu wanaohusika. Muda ni kidogo hivyo fanya hima.
Taarifa za warsha hiyo na fomu ya maombi bonyeza hapa.
Au nenda kwenye anuanni hii:

1 Maoni Yako:

At 10/30/2005 01:10:00 PM, Anonymous Anonymous said...

sante sana ndugu nitawatumia wakina mama fulani wakichelewa kufungua email zao si makosa yetu tena lakini tumejitahidi

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com