11/07/2005

Ewe mwanamuziki wa Tanzania...wewe ni balozi wa nchi yako

Niliweka barua toka kwa msanii Ferdinando Paul. Pia niliweka beti alizoandika. Bonyeza hapa utasoma barua yake ni beti yake. Sasa ametokea msomaji amempa changamoto kupitia sehemu ya maoni. Changamoto hiyo naiweka hapo chini:
Msanii jina Ferdinando Paul, unatoa HI, msanii wa ku-RAP, unasema ..... mambo TIGHT, ....unatoa VESI, mh... makubwa. Huyo ndo msanii wa Tanzania, kioo cha kuendeleza na siyo kupotosha jamii, balozi wa nchi popote duniani. Kitu kidogo tu, iweje U-rap? wakati tuna makabila zaidi ya 120 nchini yenye utajiri wa sanaa mbalimbali na ya hali ya juu, na huko ulikonuukuu rap pia wanalijua hilo. Sasa ukienda nje na ukacheza rap utadai kupiga muziki wa Tanzania au. Maisha Dasalama siyo jehanamu, wapi ni peponi? Arusha, Mza, Tanga, eh.. au unalinganisha na wapi?. Nadhani Dar siyo mahala pa rap ila pa mahadhi ya madogoli, sindimba, bhughobhoghobho, mdumange, n.k. Pia ni kwa wale waliyeko hapo na si kwingineko kwa mwili, akili na fikra zao. Hivi hi, mambo tight na vesi ndiyo nini? ... msanii, balozi wa nchi!!!!!. Hongera Kingwendu, Saida Karoli .....
*********************************
Changamoto hii inanipeleka kwenye mjadala mzito alioanzisha Jeff Msangi. Kwanza aliandika makala ambao ukibonyeza hapa utaisoma. Alipoandika makala hiyo mjadala ukaanza. Bonyeza hapa uusome. Mjadala haukuishia hapo. Uliendelea. Bonyeza hapa usome muendelezo wa mjadala huo.

5 Maoni Yako:

At 11/08/2005 07:57:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Ndesanjo nani amekupa ruhusa ya kubandikiza maoni ya mjadala ya na blogu za wenzako kwenye blogu yako? au ndo unataka kudai mjadala utatangazika vizuri zaidi?
na wewe unaanza eee. nataka umepewa ruhusa hii mbona haujatuambia wala aliyeanzisha mada hii hajatutaarifu kama ruhusu hii mpeana ya ushirikiano?
naona utulivu wako unaanza kutoweka. tuliza kipago!!!!!

 
At 11/08/2005 02:53:00 PM, Blogger Boniphace Makene said...

Ndesanjo sina vita kabisa na msanii wa Rapu au muziki wa kufoka foka sijui badala yake namtazama huyu msomaji aliyeandika yake! Je anaweza kutoa uthibitisho wake kuwa kuna wangapi wanaotamani maonyesho ya sanaa na muziki wa kienyeji hapo Bongo? Na kama hawapo walianzaje kuukataa hadi kufanya wasanii waupe kisogo!

Huyu hatambui kuwa kiuzwacho sokoni ndicho kizalishwacho? Yeye hajua dhana ya kioo kama alivyoizungumza. Mosi hiyo ni nadharia finyu ya fasihi na pili anataka Ferdinando aweke kutu kwenye hicho anachokiita kioo ili asibainishe anavyoyaona maisha yake na Jehanamu.

Huyu jamaa kama anataka kuimba wimbo mwingine aimbe lakini wa kijana huyo umeishia kuitaja Bongo na hana nia ya kufananisha Jehanamu na peponi. Sina shaka Frdinando si kasuku bali huyu msomaji wako aliyeibua dhana za namna ya kuuza soko la nje muziki na fani ya muziki.

 
At 11/09/2005 08:35:00 AM, Anonymous Anonymous said...

wewe boniphace unaongea nini unajua umekua ukionge utumbo kwa muda mrefu sana yani unatetea kitu gani?? kweli wewe juha!!!!! hebu kama unausingizi rudi kitandani kalale ukiamka utaweza kufikiria vyema zaidi.

 
At 11/09/2005 11:11:00 AM, Blogger Boniphace Makene said...

Siku zote mwenye fikra njema hafichi uso! Kuna tofauti ya muziki katika soko la Nje na lililopo Bongo. Wengi wanaopenda muziki wa Bongo Flava ni vijana ambao wanalilia maisha yao kuwa magumu na huo sio uongo. Tutaishi hadi lini kuficha mambo yetu tuykidhani walio nje hawayafahamu. Nakumbuka sasa wagosi wa Kaya walioelezea juu ya mambo ya ndani ya watu yanavyofahamika nje pale Tanga bnila kujulikana nani anayetoa habari.

Kila mjenzi wa hoja hupata liwazo pale aitwapo Juha, lakini yule aitaye bila kupiama mawanda ya hoja zake ni heri asingezaliwa. Ana shida zaidi mama aliyemzaa na titi alilonyonya. Kila upande wa hoja una thamani na haina haja ya kutumia nguvu zenye bezo katika upingaji wa hoja. Wasalaam.

 
At 11/09/2005 03:50:00 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Nakubaliana na hoja kuwa hakuna haja ya kutumia bezo kupinga hoja. Twende kwa mtindo wa hoja bin hoja. Nipe, nikupe. Nguvu ya hoja.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com