11/27/2005

Kibaki: Mavi ya Kuku Nyie!

Macharia Gaitho wa Daily Nation la Kenya anasema kuwa siku moja baada ya kambi ya Ndizi (iliyokuwa ikiunga mkono katiba mpya ya Kenya) na kambi ya Machungwa (iliyokuwa ikiipinga katiba hiyo) kufanya mkutano katika jiji la Nairobi, alipelekewa ujumbe wa maandishi wa simu ukisema kuwa shirika la uongo la CNN lilikuwa na masikitiko makubwa kwani lilikosa habari ya kutangaza kuhusu Kenya. Maana ya ujumbe huu ni kuwa kwakuwa shirika hilo hupenda kutangaza habari za vita na maaa zaidi ya zile za maendeleo na furaha, hakukuwa na habari nzuri maana walidhani kuwa siku kambi hizo mbili zilipofanya mkutano jijini Nairobi, lazima zingepigwa. Wapi.
Mashirika haya ya uongo yanapenda sana maafa. Tazama Liberia. Nchi hii wakati ikiwa kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe, vyombo vya habari vilijaa habari kuhusu nchi hiyo. Lakini hivi majuzi baada ya kufanya uchaguzi ambao ni kati ya chaguzi za amani ya juu kabisa duniani, hakuna vyombo vya habari vinavyotuambia habari hiyo. Katika uchaguzi huo wamemchagua Mama Ellen Johnson-Sirleaf kuwa Rais. Mwanamama huyu amemshinda mwanasoka wa zamani George Weah. Ingawa yeye ni rais wa kwanza mwanamke Afrika, yeye sio mwanamke wa kwanza kuongoza nchi barani Afrika. Malkia Zauditu wa Ethiopia aliongoza nchi hiyo toka 1916 hadi 1930. Pia mwanamama Ruth Perry aliwahi kuwa kiongozi wa nchi (sio rais) wa Liberia baada ya kuangushwa kwa Sajenti Samuel Doe na kufa kwa Rais Amos Sawyer. Perry alikuwa ni mwenyekiti wa Baraza la Taifa toka 1996 hadi 1997 alipomwachia madaraka mwizi na muuaji Charles Taylor baada ya "kushinda" uchaguzi.
Sielewi kwanini nimepitia njia ndefu namna hiyo hadi kufikia kwenye jambo nililotaka kusema. Niliyoandika hapo juu na ninayoandika hapa sasa hivi hayana uhusiano wa moja kwa moja. Nilifungua ukurasa huu ili niandike kuhusu Kibaki lakini mawazo mengine yakanijia. Sasa niko kwa Kibaki.
Nadhani Kibaki alipokuwa mdogo alikuwa ni matata sana kwa matani. Akina Moi nadhani walikuwa hawafungui mdomo kwa matani. Basi wakati wa kampeni zake za kutaka wananchi waunge mkono katiba iliyokuwa imfanye kuwa mfalme, aliwaita wale wanaoipinga kuwa ni wapumbavu. Ila kali kabisa ni pale aliposema kuwa wao ni "mavi ya kuku." Sijui huwa anatumia mdomo huu huu unaoshusha haya matani kula chakula na pia kusali au ana mdomo mwingine?

4 Maoni Yako:

At 11/27/2005 08:13:00 PM, Blogger Jeff Msangi said...

Ndesanjo,
Ulikuwa hujaenda nje ya mstari sana ulipoweka masuala ya Liberia.Umekumbusha historia muhimu sana juu ya watawala wa bara la Afrika.Ni muhimu sana kukumbushana historia kama hizo.

 
At 11/27/2005 09:02:00 PM, Blogger msangimdogo said...

Ni miongoni mwa athari mojawapo za hiki kilevi cha madaraka, hasa inapokuwa madaraka yenyewe yako kwa mtu ambaye amelewa utamaduni wa nje ya bara la Afrika. (nahofia kusema mataifa ya Magharibi), sababu hata mataifa hayi siamini kuwa yana asili ya huo utamaduni wa WALALAHAI wao kuwatusi WALALAHOI

 
At 11/28/2005 07:46:00 AM, Blogger Boniphace Makene said...

Safi kukumbusha historia hiyo maana siku hizi kuna dhambi ya kusahau na kubatiza kila jambo kuwa la Mara ya kwanza lakini si ile ya Mwandishi wa Blogu Msangi Mdogo bali hawa ambao hawatulii kabla ya kutangaza jambo kuwa limetokea kwa mara ya kwanza

 
At 11/28/2005 11:23:00 AM, Blogger Innocent said...

Oh Mheshimiwa Ndesanjo hiyo ni kazi nzuri kunikumbusha hili.Unajua nilikuwa nakumbuka nikisikiliza redio kipindi kile juu ya bibi Perry.
Ila hapa siunajua tena watu hawasomi historia kabisa.Nina wanafunzi wenzangu hapa hawajui ni kwanini uchaguzi umefanyika liberia wala hajui kama ilikuwepo serikali ya muda.
Nakwambia TUMEKWISHA.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com