12/01/2005

Siku ya "Umeme" Duniani

Leo ni siku ya Ukimwi duniani. Tunachofanya ni kutafakari kuhusu ugonjwa huu. Hivi Ukimwi ni nini? Ulitoka wapi? Mbona haukuwepo zamani? Au kama ulikuwepo mbona haukutumaliza? Je dawa yake itakujapatikana? Je kwanini hauna dawa? Au kama dawa ipo mbona wengi hatujui?

Basi katika kukumbuka hii siku, mwanablogu Sokari Ekine wa blogu ya Black Looks, ambaye pia ni mhariri wa blogu za Kusini mwa Afrika wa mradi wa Sauti Za Dunia, anachambua wanablogu walivyoikumbuka hii siku. Uchambuzi huo uko katika jarida la Pambazuka. Bonyeza hapa umsome.

Sokari Ekine mwenyewe bonyeza hapa umsome.

1 Maoni Yako:

At 12/02/2005 02:47:00 AM, Blogger mloyi said...

Maswali mazuri ya kujiuliza umeyaweka hapa! UKIMWI ni kitu cha ukweli na kinatutesa sana sisi waafrika! Rejea mwafrika ni mjinga au mnafiki kumuona jinsi asivyokubali ukweli.
Siyo kwamba tusiokuwa na ukimwi tumekubali ukweli wake , bali inawezekana kwamba siku yetu haijafika bado katika ujinga wetu, tuna hofu ya hali ya juu hatuthubutu hata kwenda kupima!, kwanini hali hii iwe hivi, wewe na rafiki yako mliweka ahadi ya kutokuwa waathirika wa ukimwi?
Muda sahihi wa kuangalia akili na malengo yetu.

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com