12/09/2005

Siku ya Uhuru ni Kama Mchezo Fulani wa Kuigiza?

Fidelis Tungaraza, Mti Mkubwa, ametupa tafakari kuhusu wimbo wetu wa taifa. Msome katika waraka niliouweka katika ujumbe nilioutuma kabla ya huu. Sasa katupa ujumbe mwingine ambao umeniacha nikishika tumbo kwa kicheko. Katika ujumbe wake anaonyesha jinsi ambavyo matukio ya kitaifa yalivyo kama vile mchezo fulani wa kuigiza usio na mbele wala nyuma. Ujumbe huo hapo chini:

KAMANDA: HIMA! HIMAAA!!!

ASKARI NA CHIPUKIZI WA CHAMA: TANZANIAAAA!!!!

KAMANDA: HIMA! HIMAAA!!!

ASKARI NA CHIPUKIZI WA CHAMA: TANZANIAAA!!!

KAMANDA: GWAR'DE! HESHIMA KWA JEMEDARI MKUU WA MAJESHI NA RAIS WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, NA KWA WATANZANIA WOTE, HESHIMAAAA TOA!

ASKARI NA CHIPUKIZI WA CHAMA: WAH, WAH, WAH!

INAINGIA NYIMBO YA TAIFA IKIPIGWA NA BENDI ZA JWTZ, JKT, MAGEREZA, NA POLISI.

Kama namuona Marehemu Mzee Mayagilo akiimbisha bendi ya polisi.

Mungu Ibariki Afrika
WABARIKI VIONGOZI WAKE (Hapa ndipo kilipo kiini cha mgogoro wa nyimbo hii)

Nyimbo ya taifa imekwisha sasa inakuja hotuba toka kwa Mtukufu Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Jemedari Mkuu wa Majeshi na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Mjumbe Tume Ya Waziri Mkuu Tony Blair, Mwakilishi wa Rais Bill Clinton kwenye asasi ya UKIMWI na mambo mengine mengine. Huko mikoani wakuu wa mikoa kina Nicodemus Banduka, Athumani Kabongo na wengineo nao wanatoa hotuba zao. Baada ya hapo sikuu imekwisha tunaendelea kama jana.

1 Maoni Yako:

At 12/09/2005 06:36:00 AM, Blogger Innocent said...

Hii ni siku ya wale wa tabaka tawala-elites-sisi makabwela tulie tu.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com