12/03/2005

Mkutano wa Wanablogu Uingereza Wiki Ijayo

Ule mkutano mkubwa wa mradi wa Sauti za Dunia unaofanyika nchini Uingereza katika makao makuu ya shirika la habari la Reuters umeiva. Nimepangwa kushiriki katika mjadala kuhusu blogu na uandishi wa habari. Bonyeza hapa kwa taarifa za kina kuhusu mkutano huo. Katika mkutano huu kutakuwa na wanablogu wawili toka Tanzania. Mwingine ni mwanablogu pekee wa Tanzania anayeishi na kusoma Uingereza ambaye unaweza kumsoma hapa. Orodha ya watu wote wanaohudhuria bonyeza hapa utaiona. Pia ukibonyeza hapa utaona sura za wanaohudhuria.
Kwa wale ambao hawahudhuria mkutano huu, unaweza kufuatilia kwa kupitia video ya mtandaoni (matangazo ya moja kwa moja). Unahitahiji kuwa na iTunes, au programu zenye mp3. Urushaji utaanza saa nne asubuhi kwa saa za London siku ya jumamosi tarehe 10. Bonyeza hapa ili uweze kujua saa hiyo ni saa ngapi hapo ulipo. Bonyeza hapa kwa anuani ya kufuatilia video ya mtandaoni ya mkutano huo moja kwa moja.
Kwa wale ambao hawatakuwepo London bado kuna uwezekano wa kushiriki katika mkutano huu kwa kupitia programu ya Internet Relay Chat (IRC). Kwa maelezo ya jinsi ya kushiriki kwa
Kumbuka pia nitablogu mkutano huo moja kwa moja kupitia hapa Jikomboe.
Kama nilivyosema hapo juu mimi nitashiriki katika mjadala kuhusu blogu na uandishi wa habari. Nabandika hapa chini maelezo ya mjadala wenyewe na watu ambao nitakuwa nimekaa nao kwenye kiti moto:
SESSION TWO 11:30-1:00
Best of both worlds
Much is made of the “blogging vs. journalism” argument. We believe there can and must be room for both in this world, and that the world will be better for having both.
Led by Rebecca MacKinnon, with input from Jeff Ooi (Malaysia), Ndesanjo Macha (Tanzania), Dina Mehta (India), Georgia Popplewell (Trinidad & Tobago), David Sasaki (Americas Editor), Onnik Krikorian (Armenia), Ben Parmann (Eurasia Blog), Lisa Goldman (Israel), and Dean Wright (Reuters)
Mkutano huu umedhaminiwa na Kituo cha Intaneti na Jamii cha Berkman cha Chuo Kikuu cha Harvard na Shirika la Habari la Reuters.

1 Maoni Yako:

At 12/06/2005 08:15:00 AM, Blogger Boniphace Makene said...

Mheshimiwa, mimi nikutakie safari njema na uwakilishi mwema. Wewe sio kama wale akina Mkapa ambao taarifa za safari zao zatakiwa kuandikwa na wengine, wewe kiongozi kwelikweli maana utaripoti mwenyewe kwenye ukumbi wako huu. Wasalaam

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com