12/06/2005

Usidharau Nguvu ya Blogu Kuleta Mabadiliko

Pongeza za dhati zinamwendea mwanablogu Nkya wa Pambazuko. Hivi karibuni Nkya alitaka kujua bendera ya Uingereza inafanya nini kwenye tovuti ya Chadema? Wasomaji wake wakatoa maoni yao. Hazikupita siku mara bendera hiyo ikaondolewa. Bofya hapa usome aliyoandika na bofya hapa utazame tovuti hiyo ya Chadema bila bendera ya kule kwa Malikia Lizabeti.
Pongezi zinawaendea pia Chadema kwa kukubali mantiki na uzalendo vichukue nafasi.

2 Maoni Yako:

At 12/07/2005 11:35:00 PM, Blogger mwandani said...

Nimeridhika kwamba watu wa chama hiki cha chadema wameiondoa bendera hiyo.
Ujumbe uliopelekea kuondosha hiyo bendera ulikuwa mfupi na wenye kulenga bilajazba wala kuumiza akili. Wala haukuchapwa na gazeti kubwa, bali na mtu mmoja tu (Nkya)ukifuatiwa na maoni kadhaa.
Hii ni nguvu na uhuru unaoletwa na mtandao. Shukrani.

 
At 12/08/2005 07:59:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Ndio Tunga. Baadhi ya watu wanaweza kuona kuwa hili ni jambo dogo bila kujua kuwa haya mambo madogo ndio ishara ya mambo makubwa. Kwa wanaofuatilia blogu nchi za Magharibi tumeona tayari kuna viongozi wameachia ngazi, waandishi wa vipindi vya luninga wamejiuzulu, wagombea wameshinda uchaguzi, serikali zimebadili sera, n.k. kutokana na nguvu za wanablogu.

Umetaja kipengele kikubwa sana, kuwa aliyefanya hii kazi ni mtu mmoja na blogu yake na mawazo mawili matatu ya wasomaji. Oyeeeeee!

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com