12/10/2005

Balaa Bin Mkosi!

Balaa. Mkosi. Kisirani. Bahati mbaya.
Haiwezekani. Mkono wa mtu. Kuna namna. Sio hivi hivi!!

Ni kwamba siko ndani ya ukumbi wa mkutano wa wanablogu Uingereza. Ndege niliyokuwa niondoke nayo haikuondoka kutokana na hali mbaya ya hewa. Nina huzuni kubwa. Nitaeleza zaidi hili baadaye kwani mkutano umeanza na ninaufuatilia mtandaoni. Kama hufahamu ninazungumzia mkutano gani basi bonyeza hapa utapata taarifa zote. Pia utapata taarifa jinsi ya kuhudhuria mtandaoni na kutoa maoni yako pia na jinsi ya kutazama kwa video ya mtandaoni.

Nitaandika mara kwa mara mambo yanayojadiliwa kwa wale ambao hataweza kujiunga kwa kutumia teknolojia ya IRC.

Nimepata ujumbe toka kwa mwanablogu Fatma Karama kuwa tayari yuko ukumbini hapo Uingereza. Mtanzania mwingine anayehudhuria ni Paul Kihwelo. Mshikaji Paul ni mkuu wa kitivo cha sheria katika Chuo Kikuu Huria Tanzania.

Baadaye jamani maana napitwa na mjadala.

Ukiingia IRC (kwa wanaoweza) unaweza kuingia: idhaa hii: #gvtrans
Au hii: #globalvoices

3 Maoni Yako:

At 12/10/2005 05:44:00 AM, Blogger Jeff Msangi said...

Pole sana kaka,
Ninafuatilia mijadala mtandaoni.Kuna mijadala mizuri sana jamani.Kama bado hujaingia tafadhali fanya hivyo,popote ulipo.
Ndesanjo,kwa kweli kuna mkono wa mtu hususani kwenye mikutano yako ya nje ya Marekani.Nitamuuliza babu!

 
At 12/12/2005 08:29:00 AM, Blogger Kenyan Pundit said...

Pole sana Ndesanjo...nilisikitika sana nilipo sikia vile ulikumbwa na bahati mbaya.

 
At 12/12/2005 09:37:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Ahsate Ory, ndio mambo ya theluji hayo. Ila nilifuatilia kwenye IRC toka mwanzo hadi mwisho. Hongereni mliotuwakilisha.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com