12/10/2005

Simu za Mkono na Intaneti Tanzania

Wakati mkutano wa wanablogu ukiendelea (bonyeza hapa kuhusu mkutano huo) katika mjadala uliokuwa ukiendelea katika ukumbi wa majadiliano kwa njia ya Intaneti (kwa kutumia "Internet Relay Chat".....kuhusu "Internet Relay Chat" bonyeza hapa. ), Angelo Ambuldeniya aliniuliza juu ya upatikanaji wa huduma za Intaneti kwa kutumia simu za mkono nchini Tanzania. Wakati huo tulikuwa tunajadili juu ya blogu za mkononi iwapo hii ni moja ya njia za kuwawezesha watu wasio na mtandao wa Intaneti (ila wana simu za mkono) kublogu. Swali kuu lilikuwa: je ni namna gani tunaweza kuongeza blogu duniani hasa katika nchi ambazo wananchi wake wengi hawana kompyuta?
Nina swali kwa wale walioko Tanzania, je kuna kampuni ngapi kwa jumla ambazo zinawezesha watumiaji wa simu zake za mkono kutembelea mtandao wa kompyuta? Gharama yake je?

4 Maoni Yako:

At 12/11/2005 02:49:00 AM, Blogger Hector John Mongi said...

Nitachunguza na nikipata habari za kitafiti zaidi nitakutumia. Hata hivyo nafahamu hapa nchini kwa sasa kuna kampuni 4 zinazotoa huduma ya simu selula. Vodacom, celtel, Mobitel na Zentel. Kampuni zote hizi hushindana kujitangaza katika vyombo vya habari wakielezea huduma wanazotoa. Hii ya Mtandao sijawahi kuisikia. Na najua miongoni mwa wasomi ni watu wchache sana wanatumia huduma hii kupitia IP. Hii inaonyesha kwa watu wengine ambao hata matumizi ya compyuta hawayajui, ni vigumu kufikiria kupata intaneti kupitia simu. Nitachunguza zaidi.

 
At 12/11/2005 02:56:00 PM, Blogger Fatma karama said...

Ndesanjo,
huduma ya internet kupitia simu iko Tanzania nafikri toka mwaka jana au juzi sikumbuki vizuri lakini huduma zake zilikua juu kwa kipindi hicho sijui sasa si kitu kigeni Tanzania na ninaamini ni watu wengi kiasi wanatumia hii huduma.

 
At 12/13/2005 09:05:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Hector na Fatma, asanteni kwa taarifa. Hector, ukipata taarifa zaidi basi nitumie.

 
At 12/13/2005 11:21:00 PM, Blogger msangimdogo said...

nimesoma kazi hii muda mfupi sana kabla ya kuichangia, na kitu cha kwanza kabisa nilichokifanya ilikuwa ni kuongea na watu wa Mobitel, ambao mimi natumia huduma zao na kwa mujibu wa maelezo ya mhudumu aliyepokea simu yangu, japo yalikuwa ya mkato mkato sana sawa na ugali wa hotelini (sijui sababu hakupumzika siku ya kupiga KULA, au vipi), ni kuwa hawana huduma hiyo kwa sasa

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com