12/10/2005

Mkutano wa Wanablogu Uingereza: Blogamundo kusaidia tafsiri

Mjadala mzuri sana unaendelea hivi sasa kuhusu jinsi ya kufanya "Sauti za Dunia" kuwa kweli ni Sauti za Dunia. Suala kubwa ni kuhusu jinsi gani mradi wa Sauti ya Dunia utajumuisha lugha nyingine zaidi ya kiingereza. Je zianzishwe blogu chini ya mradi huu za lugha mbalimbali kama Kiswahili? Au kuwe na ukurasa maalum wa kutafsiri kwa lugha mbalimbali?
Pat Hall amekuwa akifikiria maswali kuhusu blogu na lugha kwa muda mrefu. Yeye na wenzake wanatengeneza programu ambayo itawezesha mambo yanayoandikwa katika blogu ya Sauti za Dunia kwa kiingereza kutafsiriwa kwa lugha nyingine. Tena unaweza utafsiri kitu toka kiingereza kwenda Kichina kisha Kiswahili! Bofya hapa uone tovuti ya mradi huo uitwao Blogamundo.
Kama nimekuacha hewani, ninazungumzia mkutano wa wanablogu unaoendelea jijini London. Bofya hapa kuhusu mkutano huo.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com