12/10/2005

Mwanablogu Mpya: Malenga na Wataalamu wa Kiswahili Kaeni Chonjo!

Kasri la Mwanazuo kaa chonjo. Rashidi Mkwinda ni mwanablogu mpya wa Kiswahili ambaye anapenda sana lugha ya Kiswahili. Na pia ni mshairi anayependa kujibu wasomaji wake kwa mashairi. Tazama shairi lake hili:

Kilo chako ndicho, hicho sitarijie kisicho,
Katu sikodoe macho,ukadhani ndicho hicho,
Kwa macho utamanicho, kitakutoboa macho,
Epuka njia za chocho,si maisha pochopocho.

Blogu ya Mkwinda inaitwa Fasihi za Ufasaha. Bofya hapa umtembelee na pia kumkaribisha uwanjani.

5 Maoni Yako:

At 12/11/2005 02:10:00 PM, Blogger boniphace said...

Ndesanjo acha udhia, kidole ninyooshea
Gange umemgusia, vitisho kumtupia
Kasri limechimbia, mizizi imarishia
Itakuwa songombingo, kutaka libomolea.

Wazo la kulijengea, asili mbali anzia
Nikali bado tambua, Baba Mama ungania
Pumzi ilinambia, Kasri kwenda jengea,
Itakuwa songombingo, kutaka libomolea.

Mkwinda mwana fikia, Kasirini jifunzia
Fikira kutafunia, Fasihi kufahasia
Kisha weledi jazia, gange bora patilia
Itakuwa songombingo, Kasri libomolea.

Ndesanjo nanyamazia, karatasi kushikia
Kesho napaswa ketia, mtihani kufanyia
Nikisha kumalizia, Mkwinda ntamchapia
Kasri jumba la ghali, kicheko kubomolea!

 
At 12/12/2005 08:16:00 AM, Blogger Jeff Msangi said...

Makene nimekubali,
Hongera ndugu yangu,kazi safi ya ushairi.Sishangai kwamba kwanini ulishaanza kunisakama na ahadi yangu "hewa" ya kuweka ushairi kila wiki kwenye blogu yangu.Maisha ya magharibi hayana adabu ndugu yangu.Wewe unaelewa vyema kuhusu hili.

 
At 12/12/2005 09:32:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Makene naona huna utani. Umeamua kushusha aya bin aya...poa sana. Ngoja nimshtue Mkwinda...kazi kwake!

 
At 12/12/2005 10:12:00 AM, Blogger boniphace said...

Sina ajizi fyatua, bomu nilolizindua
Awali nilidhania, muda bado kufikia
Kumbe mwanichungulia, kwa lengo kunilipua
Nataja hali hatari, Kasri kulilindia.

Ugaidi sikujua, waweza kunifikia
Hima sipendi jutia, tahadhali naanzia
Ijapo sitasemea, Walinzi naandalia
Hii ni hali hatari, Kasirini sogelea.

Nilisema nakimbia, kurasa kutazamia
Bado sijamalizia, ni mbili zilobakia
Moja itashika tama, leo napoifutia
Nikirudi hadithia, Kasri mtazamia.

Mkwinda u wapi kaka, utata umezulia
Umechupa kwa haraka, kisa watu nitishia
Tambua sijatishika, cheche ninakutemea
Kama wataka ingia, balaghashia vulia.

 
At 12/13/2005 05:09:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Ya mja ada unene, nimepata makene,
Katu si vyema ujivune,kauli pasi mapene,
Kalamu iwe ni nene,andiko lionekane,
Ndesanjo nawe makene, kalamu vyema tumieni.

--- Rashid Mkwinda

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com