12/13/2005

"Uhuru" wa Tanzania na kichefuchefu cha Wimbo wa Taifa

Fide alituma ujumbe wa barua pepe kwa watu kadhaa hivi karibuni akihoji mantiki ya kumtaka Mola awabariki viongozi wa Afrika. Nilipenda sana ujumbe wake ule nikaufanya kuwa ni sehemu ya makala yangu ya jumapili iliyopita katika gazeti la Mwananchi, nchini Tanzania. Katika makala ile nilijadili kwa kifupi sana jambo ambalo msomaji na rafiki yangu, Frank Massawe, ameuliza hapa kwenye blogu. Katika makala hiyo nimegusia pia tukio tulilofanya jeshini (mwanablogu Nkya akiwemo) la kuchora mstari ardhini na kutamka afande mmoja pale Ruvu aruke huo mstari kama ni mwanaume!
Ninaiweka makala hiyo hapa na pia katika kona ya makala zangu, upande wa kuume wa blogu hii, chini ya picha yangu. Bonyeza hapa uisome.

2 Maoni Yako:

At 12/14/2005 10:58:00 AM, Blogger Indya Nkya said...

Unakumbuka baada ya lile tukio la kuchora msitari kesho yake afande Kaaya alitufukuza jeshi? Alipoona tunakwenda kuchukua mabegi kwenye hanga akatufukuza tukaingia porini!! Acha kabisa na Afande mwenyewe alikuwa mjanja hakuruka mstari kaishia kusema tumeshalamba unga!!

 
At 12/16/2005 06:16:00 PM, Anonymous Fred Massawe said...

Baada ya kusoma ile makala ulioipa kiungo nimepata mtazamo 'chanya'. Uliposema 'NI kweli kabisa Tanzania haikupata uhuru mwaka 1961!' nazidi kubaki katika tafakari ya bado Tanzania ipo kifungoni mwa 'Wajanja Wachache' wa hapa duniani. Ila kwa kauli ya kusema haikuwa imetawaliwa na ina sherekea uhuru inachanganya kidogo, labda tu hilo jina Tanzania ndio halihusiki na kutawaliwa. Ila najaribu kufikiria tatizo letu kubwa ni la Viongozi shupavu hatuna, hatuna 'mipango ya mbele' ya kiutawala, hatujiulizi miaka kumi au hamsini ijayo tutakuwa wapi. Kwa nini tusiwe na 'mipango mbele' madhubuti ya kuanda viongozi ambao hata kama ni wa chama cha upinzani au chama ki-twawala wawe ni shupavu na sio 'rojorojo' kama hao 'wezi' walioko sasa. Maana yangu kubwa ni kwamba mtazamo wa kiongozi wa kisiasa Tanzania ubadilike, kutokea 'kwa mpiga umbea' jukwaani kwenda kwa 'mpigania haki za mwananchi'. Hivi Tanzania haiwezi ikawa na kitengo/chuo cha kuandaa viongozi toka wakiwa vijana mpaka watapofikia umri wa kugombea nafasi mbalimbali? Huyu David C wa chama cha upinzani hapa, historia yake inaonesha ni dhahiri alikuwa mmoja wa vijana walioandaliwa kuja kuwa viongozi siku moja. Simaanishi Tanzania iwaige hawa wakoloni ila ni afadhali kuchukuwa vilivyo na maana kwao na tuvitumie ili kupata maendeleo ya Mtanzania/Mtu Mweusi/Mtu Anayepaswa kuwa huru kiroho, kiutamaduni, kisiasa, kiuchumi, kimaendeleo, kisaikolojia, kiitikadi, kifikra... Pia kama tunakubaliana hatuna uhuru katika hayo, basi kuanzia sasa tuanze/tuendelee rasmi kwa kuweka 'mipango mbele' ya wapi huu uhuru wetu ulipo, tuyaendeleze vipi haya mapambano ngazi kwa ngazi(maana najua yatafanikiwa, iwe kuna waliopewa mezani!), tujadili kwa kina kwa nini 'Uhuru' bado ili kufahamisha zaidi raia... Unajua kina Mao, Hitler, siri kubwa ya mafanikio ni kwamba ni watu waliokuwa na Ari ya kutimiza wanayotaka kwa kuunganisha raia wote kuwa kitu kimoja (kitamaduni, kifikra, kiitikadi...), sijui kwa nini nina mengi ya kusema....

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com