12/17/2005

Tuko Tayari Dakika Hii...


Naendelea kuweka picha zaidi nilizopiga wakati wa maandamano ya Vuguvugu la Watu Milioni na Zaidi kule Washington, DC, Oktoba mwaka huu. Hawa ni wanachama wa kundi la New Black Panther Party (tofauti na lile kundi la wazee wengine wa shoka la Black Panther). Hapa unaona mwenyewe wanaume wa shoka wako tayari tayari kwa lolote lile. Joji Kichaka, we endelea kuleta za kuleta...

Picha hiyo hapo chini ndio kiongozi wao, Malik Zulu Shabazz. Huyu bwana analindwa na utitiri wa wanaume wa shoka sijapata kuona. Bonyeza hapa usome kwa kifupi juu yao.1 Maoni Yako:

At 12/22/2005 10:05:00 PM, Anonymous Anonymous said...

Ndiyo mzee,

Nakumbuka takribani miaka ishirini na kitu iliyopita jinsi nilivyokuwa nimeingiwa na wale Machui Weusi wa kwanza kina Huey Percy Newton, Bobby Seal, Eldridge Cleaver, David Hilliad, Fred Hampton, Masai Hewitt, Bobby Hutton, hadi Mwenyekiti wao wa mwisho Bi Elaine Brown. Wale wa kwanza walikuwa mapaka kweli mapaka walipopoteza mwelekeo kuja kuwa Mapaka Weusi. Tena kuna mmoja yupo Arusha kawa Bwana Maendeleo. Sasa tuwaangalie hawa wapya kama na wao watawainua watazamaji vitini. Nawatakia kila la heri kwenye mapambano yao.

Aluta continua,

F MtiMkubwa Tungaraza.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com