12/30/2005

Unaifahamu Afrika Kwa Kiasi Gani?

Mmoja wa waanzilishi wa Mradi wa Sauti za Dunia, Ethan Zuckerman, ameaandaa ka-mtihani kadogo kuhusu Afrika. Jaribu kufanya mtihani huo uone unafuatilia masuala ya Afrika kwa kiasi gani. Nimekosa swali moja kwa ujinga! Tena swali lenyewe linahusu jambo ambalo ninalifuatilia kwa karibu sana, matumizi ya simu za mkono Afrika. Bonyeza hapa ujaribu bahati yako. Kisha bonyeza hapa usome aliyoandika kuhusu ka-mtihaki hako na maoni ya waliojaribu. Iwapo hutaki "kuibia" nakushauri ufanye mtihani wenyewe kabla ya kusoma maoni ya watu maana pale utapata baadhi ya majibu. Ukifanya hivyo utakuwa unajidanganya mwenyewe. Ukipata F tuambiane!
Huko nyuma niliwahi kutoa jaribio jingine lilloandaliwa na mradi wa SchoolNet. Jaribio lao, kama ambavyo utaona, linakupa nafasi ya kuchagua unataka maswali magumu au mepesimepesi. Kama umetoka Afrika, chagua maswali magumu kabisa. Chini ya ramani utakayoiona ukibonyeza kiungo nitakachokupa ndio kuna sehemu ya kuchagua kama unataka mteremko au la. Bonyeza hapa ujaribu. Kama umepata sifuri tuambie usifiche!


2 Maoni Yako:

At 12/30/2005 08:34:00 AM, Blogger mloyi said...

Heri ya mwaka mpya
Sijui aliyetufundisha kwamba mwaka unaishia sasa. Lakini kila mmoja yuko katika harakati za kufunga mwaka.
Tuufunge kwa usalama ili usijegoma kufunguka siku tukitaka.
2006 tuikaribishe kwa habari na mijadala motomoto inayojenga.

 
At 12/30/2005 05:52:00 PM, Blogger Jeff Msangi said...

Ndesanjo,
Ka-mtihani ka Ethan kazuri sana.Nimepata 80%.Nikajisikia aibu kwa sababu ka-mtihani kalikuwa karahisi ukizingatia jinsi ninavyofuatilia masuala ya Afrika!Au nimefuatilia zaidi ya Tanzania nini!!??Ngoja niangalie daftari langu la wapiga kura tena!

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com