12/26/2005

Kumbe Kaka Pori naye anablogu?

Jua ndio linachomoza kwenye uwanja wa blogu za Kiswahili (huku tukiwa bado tunatafuta neno muafaka la chombo au uwanja huu...Da Mija ameweka kiungo cha uwanja wa kuendesha mjadala huu). Napenda kumtangaza mwanablogu mpya, Kaka Pori. Kwa maneno yake mwenyewe anasema kuwa lengo la blogu yake ni:
"Tumetawaliwa kiakili kiasi kwamba tumesahau kabisa sisi ni akina nani. Sasa basi, kwa kupitia blogu hii, tutaamshana, kukumbushana na kupeana hamasa ya kujitambua kwa kupeana habari chanya na mawazo jengevu. Ili tuweze kujenga jamii chanya, tunahitaji umoja, mshikamano, kujielewa na kuelewana, kuhabarishana, n.k. Nipo nanyi nyote na ninaomba kujiunga nanyi."
Bonyeza hapa umtembelee na kumkaribisha. Utamaduni wa kukaribishana ni mzuri sana na ninaombe tuuendeleze.
Kiungo nilichoongelea hapo juu cha kibanda cha kubunga bongo kuhusu neno muafaka la blogu utakipata ukibonyeza hapa.

1 Maoni Yako:

At 12/28/2005 03:45:00 PM, Blogger Boniphace Makene said...

Ndugu Ndesanjo, nadhani nimetimiza kiu yako muda si mrefu katika KASRI. Waweza pita hapo na kutupa macho. Nado nakumbuka hoja ya kuweka maandishi yangu katika Ripway. Sijapata muda kucheza na kompyuta nadhani nikifika Texas itakuwa ni jukumu langu la kwanza. Ok salamu na karibu.

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com