1/02/2006

Mjadala wa Neno Muafaka la Teknolojia ya Blogu Unaendelea

Ule mjadala wetu kuhusu neno muafaka la teknolojia hii ya blogu bado unaendelea. Maneno ambayo yamependekezwa hadi hivi sasa ni haya:
Duru, Kasiri, Lipuli,Vuga, Dondoo, Lipuli, Vuga, Uwanja wa Fikra Komavu, Gazeti Tando, Ngwanga, Bawazi, Dimba, Pukutu, Dafinapepe, na Ungo.
Bonyeza hapa ili usome sababu za kupendekezwa kwa maneno haya. Mtu yeyote anaweza kushiriki kwenye mjadala huu hata kama sio mwanablogu.

1 Maoni Yako:

At 1/04/2006 04:15:00 AM, Blogger Bwaya said...

Nimesoma mapendekezo. Nimepata changamoto sana.
Mimi naunga mkono neno BAWAZI kwa sababu kwanza ni fupi na limebeba maana yenyewe ya blog. Halafu halileti picha kuwa Blog ni mahali fulani.
Heri ya mwaka Mpya Ndesanjo!

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com