12/30/2005

Kikosi Kamili Chini ya Kocha Fide Pale Helsinki

Sio muda mrefu nimemaliza kuonga na Jeff Msangi ambaye alikuwa akimzungusha mjini Toronto Boniphace Makene. Katika maongezi yetu tuligusia umuhimu wa kuanza kupanua matumizi ya blogu zetu kwa kuweka picha pale panapofaa na hata kuingilia blogu za sauti na video. Wakati wake utafika.

Baada ya kuongea na Jeff kuhusu picha nikatembelea kamera ya Michuzi nikakuta amewaka picha ambayo imenikumbusha picha ambazo nilisahau kabisa kuziweka kwenye blogu. Bonyeza hapa uone picha aliyotupiga Michuzi nikiwa na mzee mwenyewe Mti Mkubwa (ambaye amebatizwa jina jipya: Mti Mkubwa Mkavu). Basi ndipo nikaanza kuchimba picha nilizonazo toka Helsinki.

Nimeweka picha ya kikosi kamili cha Watanzania wanaoishi Helsinki na wale ambao tulikuwa tuko ziarani hapo. Utamuona Michuzi mwenyewe na Mti Mkubwa Mkavu wakitabasamu. Picha hii ilipigwa na rafiki yangu, Vikii wa jarida la mtandaoni la nchini Malaysia, Malaysiakini. Hapa tulipokuwa ni eneo la kujidai la Watanzania wanaoishi jijini hapo (Fide: klabu ile inaitwa nini tena?).
Ukitaka kuiona picha hii vizuri, peleka mkono wa kipanya chako juu ya picha kisha bonyeza.
**Nyongeza:
Ametokea mtu akaweka majina ya walioko kwenye picha hii kwenye sehemu ya maoni. Pia jina la klabu yenyewe, Chelsea Sports Pub. Majina ya walioko kwenye picha haya hapa:
Pichani kutoka kushoto ni Lwitiko Mwalukasa, Benard Kakengi, Mapinduzi Mwankemwa, Mzee Kimaro, ? , Raymond Mutafungwa, ? , Dennis Londo, Muhidin Issa Michuzi, F MtiMkubwa Tungaraza, Ndesanjo Macha, Magonera Malima, na Kisakisa Kiwara. Picha ilipigwa ndani ya Sports Pub Chelsea. Ukifika Helsinki usiwe na wasiwasi wa kuwapata Watanzania fika Chelsea Sports Pub utawakuta wakinywa na kusogoa masuala mbali mbali ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi.

2 Maoni Yako:

At 12/30/2005 05:41:00 PM, Blogger boniphace said...

Nimekubali Ndesanjo una kasi yaani sasa hivi umeanza kutoa hadidu za rejea za mazungumzo kabla hata sisi hatujaanza. Ok nitaanza kuweka yangu baadaye kidogo. Hongera kwa kuanza uwajibikaji mara moja.

At 12/31/2005 06:58:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Pichani kutoka kushoto ni Lwitiko Mwalukasa, Benard Kakengi, Mapinduzi Mwankemwa, Mzee Kimaro, ? , Raymond Mutafungwa, ? , Dennis Londo, Muhidin Issa Michuzi, F MtiMkubwa Tungaraza, Ndesanjo Macha, Magonera Malima, na Kisakisa Kiwara. Picha ilipigwa ndani ya Sports Pub Chelsea. Ukifika Helsinki usiwe na wasiwasi wa kuwapata Watanzania fika Chelsea Sports Pub utawakuta wakinywa na kusogoa masuala mbali mbali ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi.

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com