12/30/2005

Hukujua Kuwa Michuzi Anaimba Sauti ya Nne?

Michuzi sio tu ana ujuzi wa kupiga picha bali pia ni mwimbaji mashuhuri sana hasa akiwa nchi za nje. Katika picha hii Watanzania tuliokuwa katika mkutano kuhusu utandawizi na demokrasia katika jiji la Helsinki, Ufini mwezi Septemba, tunatumbuiza. Siku hii ilikuwa ndio mwisho wa mkutano. Tukiwa katika tamasha la kuaga wana mkutano, Mama Maria Shaba ghafla alitufuata mimi na Michuzi nje. "Watanzania lazima tuwakilishe."
Nikamuuliza, "Tuwakilishe vipi?"
Akasema, "Toka tuje wanaoimba na kutumbuiza ni Wafini, kwani sisi hatuna sauti? Lazima tukaimbe."

Basi akatukusanya Watanzania mmoja mmoja. Hakuna kukataa. Hao jukwaani. Mnajua tuliimba wimbo gani? Buni....tuliimba Malaika. Michuzi akiwa ndio sauti ya nne. Katika picha unamuona Mama Shaba akiwa ameshika kipaza sauti. Pia unaweza kumuona Mama Mwingira wa Tango kushoto kwa Maria Shaba. Mimi nadhani nilikuwa naimba sauti ya 60! Baada ya kumaliza wimbo wa Malaika, tuliaga jukwaa, huku tukishangiliwa kwa nguvu, kwa wimbo wa Bob Marley: Get Up, Stand Up. Wimbo huu ndio wimbo rasmi wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International.
Ili uione picha kwa uzuri zaidi bonyeza juu ya picha yenyewe (peleka mkono wa kipanya cha tarakilishi yako).

9 Maoni Yako:

At 12/31/2005 01:21:00 AM, Blogger nyembo said...

hi!
kwa kweli ninavyomjua Michuzi huyu, sauti yake inaweza kuwa ni sawa na bati zinazogongana ni hatari kweli kweli muulizeni Miss World Afrika Nancy Sumari anatambua hili,kwa kuwa alikuwa karibu sana siku ile ya kupata ushindi wake kama miss Tanzania

 
At 12/31/2005 01:27:00 AM, Blogger nyembo said...

kama angekuwa Mtangazaji pale katika kiredio chetu cha vijana tulio wengi cha Clouds of Ruge Mutahaba basi sote tungekuwa viziwi kwa kweli ni hatari ndio maana anatumia Focus tu,jicho kwake ni silaha na kalamu....lakini kwa wimbo wa Malaika kunauwezekano wa yeye kuimba kwani si kama wimbo wa Katika Misiba na sehemu za vifo nani hawezi kuimba Parapanda italia parapandaa...parapanda italia parapanda naye bw...atakuwa amekwisha nyakuliwa kwenda kumuona bw.....mawinguni....mh!iiiiiii
inawezekana maana hapo hatuhitaji mtu kunyata na bit, wala kuprogram vionjo..acha sauti yako ya sitini Ndesanjo pale kupanda na kushuka kunategemea pumzi yako tu muungwana

 
At 12/31/2005 02:07:00 AM, Blogger Bwaya said...

Nafikiri huo sasa ni mwanzo mzuri na anaweza kabisa kuzindua albamu yenye vibao vikali...ila asisahau kukiweka na kile cha...Mungu ibariki Afrika...wabariki VIONGOZI wake...ili na Msekwa atulie kidogo. Ujue dhahama aliyoipata sio mchezo anahitaji liwazo la sauti kama ya Michuzi ilirembeshwa na ile ya 60 na kitu ya Bwana Macha.

 
At 1/01/2006 04:31:00 AM, Blogger nyembo said...

BWAYA umenifurahisha kumtaja komredi Msekwa,unajua siku moja nilikuwa nyumba jirani na ile ikulu ya spika iliyopo Dodoma,sasa mama mmoja anafanya kazi Nishati na Madini ambae ndie mwenye makazi hayo jirani ya ikulu hiyo akaniambia unadhani jirani yangu ataiacha hii nyumba,sijui! maana amesimamia ujenzi wa sehemu ya kuogelea ya kisasa kweli kweli huko nyuma ya nyumba,sasa itawezekana kweli kumjengea mwingine?
mimi nilibisha kabisa nikakataa majadiliano kuhusu hilo,kwa kigezo ameona vingi amefanya vingi ana busara ya kutosha...mh kumbe mwili unazeeka lakini nafsi haizeeki inapeta tu mwanangu!
sijui watampa cheo gani cha kumsetiri maana wimbo wa Michuzi na Macha na vionjo vyote haviwezi kumliwaza labda kinubi cha nabii Daudi na sijui kama kinapatikana kwenye hekalu la bwana pale Yerusalemu ktk ukanda wa Gaza.tumuulize sharon

 
At 1/01/2006 05:27:00 PM, Blogger HappySam said...

very cool

 
At 1/03/2006 12:39:00 PM, Blogger John Mwaipopo said...

Uzuri wa wabongo ni wazalendo sana wanapokuwa-ga nchi za mbali. Ka-spirit hako kananikumbusha Tulipokuwa Washington, DC na waswahili wenzangu wakina Boniface Makene (yule anayeishai Dar lakini amezaliwa Mara) na wengine ambao Boniface Mazenga aliwahi kuwaweka bloguni kwake. Tulipoona hatumo kwenye karatiba kao tukajikusanya, halafu tukawapembeja wakenya tukaunda East African Crew. Unajua tuliimba wimbo gani.

Jambo, jambo
Jambo bwana
Habari gani
Nzuri sana
Wageni mwakaribishwa
Afrika yetu (ona mabadiliko kidogo)
Hakuna matata

Safi sana wa-Bongo wote wenye mwamko kama huu

 
At 1/07/2006 06:20:00 AM, Blogger Chemi Che-Mponda said...

Nimefungua hii picha na kumwona Dada Maria Shaba kashika Microphone anaimba kwa furaha kabisa! Na Michuzi na ndesanjo ni back-up singers! Ama kweli wasanii utawajua!

Pizha safi sana, naona mlituwakilisha vizuri!

 
At 1/08/2006 09:50:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Nadhani itabidi niwasiliane na Michuzi ili turekodi kabisa santuri. Nadhani mchanganyiko wa sauti ya nne ya Michuzi na sauti ya 60 na ushee ya kwangu utatoa muziki ambao dunia haijapata kuusikia. Tutawakilisha kisawasawa katika ulimwengu wa muziki. Nadhani itabidi muziki wenyewe uwe mchiriku maana ninauzimia sana. Lakini Michuzi unajua tena, sijui kama atakubali kuwepo kwenye santuri ya Mchiriku.

 
At 1/25/2006 05:48:00 AM, Anonymous Anonymous said...

Ndesanjo hilo wazo la muhimu sana, mimi najitolea kuwa 'producer'.
Dennis

 

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com