1/05/2006

Ethan Zuckerman Kafurahia Blogu ya Mwandani

Mwandani kaandika kisa kimoja kikali sana. Nilipokuwa namsoma nilikuwa najisemea, "Hivi bila blogu habari kama hii Tunga angeitoa wapi?" Ingebidi labda atafute gazeti au labda atume barua pepe kwa marafiki zake. Kisa murua sana maana kinaonyesha masahibu ya kuishi Ughaibuni na pia madhara ya vyombo vya habari vya magharibi ambavyo habari za Afrika kwao ni zile zinazohusu maafa au ufedhuli wa watwawala. Pia kisa hiki kinaonyesha jinsi ambavyo wananchi wengi wa magharibi wana ufahamu mdogo sana wa dunia iliyowazunguka.
Furaha yangu imekuwa kubwa zaidi nilipogundua kuwa sisi wazungumzaji tu wa Kiswahili waliofurahia aliyoandika Mwandani bali pia wazungumzaji wa Kiingereza. Rafiki yangu na mmoja wa waanzilishi wa mradi wa Sauti za Dunia, Ethan Zuckerman, amependa sana aliyoandika Mwandani. Amemzungumzia Mwandani kwenye blogu yake (na niliposoma pale kuna msomaji mwingine alishatoa maoni na kusema amependa sana). Bonyeza hapa usome aliyoandika Ethan kuhusu Mwandani. Bonyeza hapa usome alichoandika Mwandani.



2 Maoni Yako:

At 1/05/2006 10:08:00 AM, Blogger Jeff Msangi said...

Kwa kweli hata mimi Tungaraza alinisisimua sana na kisa kizima cha maisha ya ughaibuni nk.

 
At 1/05/2006 11:08:00 AM, Blogger Shaggy said...

Nami lugha ya kiswahili sikielewi vyema lakini nitajaribu.

Hujambo ndugu yangu. Mimi ni mkenya halisi na lugha sasa imefika ukingoni. Kingereza na sheng sasa mii ni mwenyewe.

Bonyeza kidude au sio.

 

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com