3/22/2005

MWANAHARAKATI WA MTANDAO WA KOMPYUTA AFARIKI

Mwanaharakati wa haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari anayetumia mtandao wa kompyuta (cyber-dissident) wa nchini Tunisia, Zouhair Yahyaoui (36), amefariki dunia hivi karibuni. Aliaga dunia tarehe 13 mwezi huu kwa ugonjwa wa moyo. Yahyaoui atakumbukwa kwa mchango wake katika kupigania haki na uhuru wa habari nchini Tunisia. Yeye ndiye mwanzilishi wa webu ya tunezine.com. Yahyaoui alikuwa ndiye mtu wa kwanza kushinda tuzo mpya ya Cyber-Freedom mwaka juzi. Tuzo hii hutolewa na shirika la Waandishi Wasio na Mipaka (Reporters sans frontières ). Ukibonyeza hapa utaona webu mbalimbali zenye habari zaidi juu ya wanaharakati wanaotumia teknolojia ya kompyuta na nguvu za dola zinazotumiwa dhidi yao.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com