3/21/2005

KUOA MZUNGU

Jana nilimzungumzia yule bwana aliyeniandikia akisema kuwa watu wanaooa wazungu wanasahau Uafrika wao. Alikuwa akinishitumu pengine kwa kudhani kuwa nimeoa mzungu. Rafiki yangu mmoja kaniandikia akijibu tuhuma ya huyu bwana ambaye anataka tuamini kuwa aliyeoa Mwafrika hana Uafrika kama aliyeoa Mwafrika mwenziye. Ninaibandika barua yake hapo chini muisome:

Hali gani?

Vipi mjomba, naona unaamsha hisia za watu mbalimbali.
Haya, kuna jambo linatatiza. Hivi kuoa mtu mweupe au mchina ni kusahau uafrika? mbona Agostino Neto wa Angola alikuwa na mke mtu mweupe wakati Mobutu alikuwa na mke mweusi ti, yupi mwafrika sana Mobutu au Neto? Sina hakika, Gamal Nkrumah si mtoto wa Nkrumah mwanamapinduzi tunaemuenzi.. mama yake si ana asili ya kiarabu..wakati washenzi wengi wengi wengine akina Abacha wana wake weusi. Wezi wote tanzania wameoa waarabu? Utu wa mtu, au Uafrika wa Mwafrika si pambo la kuvaa au kito cha kuonesha..au kwa mahusiano ya unyumba tu.
Nawaona wengi wenye siasa za kushutumu watu weupe kwenye vilabu huku ughaibuni, ikesha mwisho wa usiku utawaona hao wanachukua vimada weupe kwenda kufanya zinaa mbele huko.

Kesho yake utawasikia tena wakicheka fulani kaoa mweupe, kwenye kiza vipembeni haoooo! nao wanashiriki weupe.
Nafikiri suala kubwa hivi sasa ni hili - Je tunafanya nini kwa Afrika. Mchango wetu ni upi. katika siasa watu wanao ogopa ukweli siku zote hutaka kumuua tarishi, kumtusi tarishi ili ujumbe wake udharauliwe. tukitizama vita ya kichaka huko umangani... watu wote waliotaka kusema kweli wako wapi... utu wao na kazi zao vyote vilitiwa dosari ili ukweli juu ya vita usitoke.

Basi twende mbele na turudi nyuma, tutahadhari na mambo ya binafsi, huyu anakula makdonad basi si mzalendo, huyu kavaa tai basi si mwafrika safi, huyu kaoa mchina basi si mwafrika safi...

Kwaheri.
***********************************************************************************

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com