3/16/2005

KWANINI WATANZANIA HAWAFUNGI MIKANDA?

Ninapokutana na wakoloni wanaokwenda Tanzania kutembelea wanyama...(ndio, sio kutembelea binadamu. Wanyama wa Afrika wanapendwa zaidi ya Waafrika), katika mambo ambayo hawaelewi ni tendo la madereva kuendesha magari bila kufunga mikanda. Watalii wana akili fupi sana. Kitu gani wanashindwa kuelewa? Hawajui kufunga mkanda ukiwa ndani ya gari ni kujitakia kifo? Ndio maana mimi hadi leo sifungi mkanda. Polisi wakinisimamisha ninawasomesha. Nawaambia kwenye utamaduni wetu usalama ni kutokufunga mkanda.
Wananiuliza, "Kuna sababu gani ya msingi inayowafanya msifunge mikanda?" Nawaambia jibu ni rahisi sana: Ukifunga mkanda wakati wa ajali utashindwa kuruka! Full Stop!

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com