3/11/2005

NAKUBALIANA NAWE KITURURU

Kitururu (sifahamu jina lako la kwanza) wa Tanganyika (kama ulivyoeleza mwenyewe) ninakubaliana kabisa na maneno yako. Umenitumia ujumbe huu hapa chini ukinukuu maneno niliyoandika hapa bloguni juzi:

Nimependa sana blog yako. Lakini katika maandiko yako hakuna hoja dhaifu ulioiandika kama hii hapa (chini hapo ananukuu maneno yangu):
Rafiki yangu wa karibu kanionya niache kuandama "watumishi" wa mungu maana wanaweza kuniombe! Naona anaweza kuwa anasema kweli. Itabidi nipunguze kidogo. Kidoooooogo. Sitawagonga sana.

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Ninakubaliana nawe. Na kwa msingi huo nitapambana kisawasawa na watu wanaojiita "watumishi" wa mungu. Hasa wale wanaotuhadaa kwa kutuambia kuwa tukubali kuteseka hapa duniani chini ya sirikali za kidhalimu kwani tutapata raha ya milele tukifa. Wanakubali tubebe chakula kichwani huku tunalia njaa. Tunaweza kuanza kupata hiyo raha ya ahera hapa duniani kama wanavyoipata wao. Kwahiyo, ndugu Kitururu. Sitapunguza hata kidogo.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com