PADRI KARUGENDO: BURIANI JUSTIN KALIKAWE
Nimeweka makala mpya ya Padri Privatus Karugendo. Makala hii iliandikwa baada ya kufariki kwa mwanamuziki wa Rege, Justin Kalikawe. Alifariki Agosti 12, 2003. Ingawa makala ni ya muda mrefu, ujumbe wake una uhai hadi leo. Nakumbuka mara ya kwanza kumsikiliza Kalikawe, ilikuwa ni 1991/92 nikiwa Ilboru. Nadhani Tunga ndiye alikuwa na kanda moja yenye nyimbo zake ambazo sijui kama alikuja kuzirekodi rasmi. Nilijua kuwa nyota mpya ya Rege Tanzania inachomoza. Wimbo wake wa Mizimu ambao Padri Karugendo kauzungumzia unaweza ni wimbo wake ninaoupenda kuliko zote. Wimbo wake wa Machinga nakumbuka ulipigwa sana katika mitaa ya jiji la Dasalama. Na wimbo wa MV Bukoba ulitukumbusha msiba mkubwa wa taifa uliotokea kwenye lile ziwa lenye jina la Malikia wa Uingereza, Vikitoria (au Vikii kwa kifupi). Bonyeza hapa usome makala hiyo ya Kalikawe. Bonyeza hapa usikilize baadhi ya nyimbo zake. Ukifika kwenye webu ya Mzibo, bonyeza juu ya picha ya Kalikawe. Kumbuka makala nyingine za Karugendo ziko kwenye safu yake hapa bloguni iitwayo Kalamu ya Karugendo.
0 Maoni Yako:
Post a Comment
<< Home