12/07/2004

MAGAIDI NA URUBANI

Nimecheka kweli leo. Nilikuwa natazama kituo cha luninga cha C-Span ambacho hakina utumbo wa matangazo. Basi jamaa mmoja anasema kuwa walimu wa urubani wa wale jamaa waliofanya shambulio la Septemba 11, 2001 walikuwa hawawaelewi wanafunzi wao kabisa. Walimu hao walikuwa wanashangaa sana inakuwaje hawa mabwana wanasomea urubani lakini hawataki kujifunza kutua? Yaani wakati wote wao walikuwa wanataka tu kujua jinsi ya kuendesha ndege ikiwa angani. Kutua? Hata! Hawataki kujua! Mambo ya jinsi ya kutua uwanja wa ndege walikuwa hawana habari nayo hata kidogo. Walimu wakajisemea, "Marubani gani wasiotaka kujifunza kutua?" Kumbe jamaa nia yao ni kutua juu ya orofa la kituo cha biashara!

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com