JINSI YA KUWA "MSWAHILI"
Mwanablogu wa Furahia Maisha Yako sijui kapotelea wapi. Kuna mlolongo wa mambo yanayomfanya mtu ahitimu kuwa "mswahili" ambayo aliyaandika kwenye blogu yake. Kila nikiyasoma lazima nijishike mbavu. Tazama baadhi ya mambo hayo:
1.Una machupa matupu ya shampoo, maji, manukato pamoja na vipodozi vyengine umeweka tu wala huna shuhuli nayo.
2. Watoto wako wote wana majina ya utani mfano babu ali,chidi ,mamu,dida n.k.
3. Hakuna mtu katika familia yako anaetoa taarifa kwako anapo kuja kukutembelea mfano kaka,shangazi n.k.
4. Mifuko yako imejaa vitu kama vile vijiti vya kusafishia meno,tissue n.k ulivyochukua sehemu kama vile mikahawani.
5. Mama yako wanamigogoro na ndugu na hawazungumzi kwa muda wa siku 10 au zaidi.
6. Hupigi simu isipokuwa katika muda ambao gharama za kupiga ni nafuu(mfano usiku sana)na mara nyingi huwa una beep tu.
7. Ulipokua mdogo nguo unazonunuliwa pamoja na viatu ni vikubwa mara mbili ili uweze kuvivaa muda mrefu zaidi.
8. Stoo yako imejaa vitu (makorokoro) kwa kuwa hutupi kwa kuamini kua ipo siku utayahitaji kwa mfano kapeti ukilitoa hulitupi n.k.
9. Unapomsaidia mtu na akafanikiwa basi utakua unasema kama sio mie asingekuwa vile yule.
0 Maoni Yako:
Post a Comment
<< Home