12/06/2004

TUZO YA FASIHI YA KISWAHILI...N'TANYONGA MTU!

Mwandishi wa gazeti la The Guardian, Bilal Abdul-Aziz, ndiye aliyepokea tuzo ya fasihi ya Kiswahili mwaka huu kufuatia kitabu chake upelelezi kiitwacho Ushindi. Nakupongeza ndugu Bilal.
Baada ya kusema hayo napenda kuwaomba ndugu zangu muone jinsi gani tumetekwa fikra na nyoyo zetu. Hii tuzo ni ya Kiswahili...unajua imepewa jina gani? Inaitwa: Kiswahili Literature Series (KLS) Award. Kulalek! Tuzo ya Kiswahili lakini jina lake ni la kiingereza. Walahi, n'tanyonga mototo wa mtu. Tumefikwa na gonjwa gani? Ikitokea siku tuzo ya fasihi ya watunzi huko Uingereza ikapewa jina la Kiswahili na kuitwa: Tuzo ya Fasihi ya Kiingereza...nitakuruhusu unitukanie....(jaza mwenyewe!). Naapa, haki ya nani vile...sisi tu wagonjwa mahtuti. Virusi vya Kupunguza Uwezo wetu wa Kufikiri kama Waafrika vinatumaliza kama vile vingine vya kupunguza kinga ya magonjwa mwilini.

Ndugu zanguni, lazima tufikie kikomo cha upuuzi huu.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com