12/03/2004

NINAKUMBUKA...

Ninakumbuka nilipokuwa kidato cha kwanza pale sekondari ya Mawenzi, siku moja, Kisanga ambaye alikuwa ni mwalimu wa hesabu, ali[ita kukagua kazi kwenye madaftari yetu. Basi alipofika kwangu, alitazama kazi yangu. Kisha akachukua daftari langu na kuligeuza ili asome jina langu. Akatazama tena kazi yangu na kuanza kucheka huku akiondoka taratibu. Akasema katikati ya kicheko, "Kijana mwandiko wako unaonyesha hesabu zinakupiga chenga." Nakumbuka marafiki zangu, Richard Shilangale na Ramadhani Issa (Ojukwu) walikuwa hawana mbavu kwa kucheka maana walijua kuwa ni kweli nilikuwa "mweupe" kwenye hesabu. Rafiki yangu Cosmas wa Majengo alinitania juu ya tukio hili kwa miaka minne hadi tulipomaliza shule. Hapana, zaidi ya miaka minne, maana tulipokuja kukutana miaka ya baadaye alinikumbusha na kuendelea kunitania.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com