12/01/2004

SIKU YA "MIWAYA" DUNIANI

Leo ni siku ya miwaya duniani. Utakapoamka hadi kwenda kulala leo hii, watu zaidi 16,ooo watakanyanga "umeme." Kwa habari zaidi na takwimu juu ya Ukimwi tembelea tovuti ya UNAIDS hapa.
Pamoja na ukweli kuwa gonjwa hili linatumaliza mmoja baada ya mwingine, inaaminika kuwa kuna baadhi yetu ambao bado wana ule mtazamo wa "ajali kazini." Na wengine wanasema, "Kama ni kufa, binadamu wote tutakufa." Ukimwi ni hatari, tukubali au tukatae. Ni watu wachache sana hivi sasa katika nchi za Kusini mwa Afrika ambao hawafahamu mtu au watu ambao wana Ukimwi au wameshakufa kwa Ukimwi. Mimi mwenyewe kijijini kwetu nimeshaacha kuhesabu siku nyingi. Sitanii. Sio ndugu, majirani, marafiki, n.k.
Wakati tunakumbuka siku hii ya Ukimwi Duniani, tusisahau kuwa Malaria bado ni ugonjwa unaoua watu wengi zaidi ya ugonjwa wowote duniani.
Tutumie siku hii kukumbuka ndugu zetu, marafiki, majirani, wafanyakazi wenzetu walioaga dunia na wapendwa wao walioachwa duniani. Pia tutumie siku hii kuamua kuishi kwa usalama na wajibu-binafsi maana uhai wako tunauhitaji sana. Mapambano bado hayajaanza. Lazima uwe tayari. Kama umesoma makala mpya niliyoipandisha jana utajua mapambano ninayozungumzia.
Tafadhali, tembelea pia tovuti ya cheza salama. Kongoli hapa.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com