12/01/2004

"RINDA" LA TAIFA KENYA

Kumbe Kenya wako kwenye msako kabambe wa vazi, au kama wanavyoita wao "rinda," la taifa. Nimeipata hii leo wakati nikisakura blogu ya mawazo na mawaidha. Kuna tovuti inayohusu msako huo. Kongoli hapa.
Nadhani Tanzania ndugu Merinyo na mkewe Ailinda Sawe wa Afrika Sana wako katika kampeni kama hii. Sina taarifa rasmi. Nitaulizia. Lakini unaweza kutembelea tovuti ya Afrika Sana hapa.

Halafu jamaa wa mawazo na mawaidha kanishangaza. Sikuwa najua kuwa Kenya wana gazeti moja tu la Kiswahili: Taifa Leo. Huwezi kuamini kuwa hii ndio nchi aliyotoka Ngugi wa Thing'o aliyeandika: Decolonising The African Mind. Hoja yake kubwa katika kitabu hiki ilikuwa ni umuhimu wa kuendeleza lugha za kwetu kama moja ya mapambano dhidi ya ukoloni mamboleo na utegemezi.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com