12/01/2004

BLOGU NI NENO LA MWAKA!!!!!!!!!

Kwa mujibu wa kamusi ya Merriam-Webster, neno "blog" ndio neno la mwaka 2004. Hili ndio neno ambalo watu wengi zaidi wametafuta maana yake katika kamusi hiyo maarufu duniani. Kila mwaka kamusi hiyo huwa na orodha ya maneno 10 ambayo maana yake imetafutwa na watu wengi. Kwa mwaka huu neno hilo ni blogu! Itabidi nikanywe bilauri ya mvinyo kusherehekea!
Tafadhali, jiunge katika mapinduzi yanayoletwa na nyenzo hii mpya ya habari, mtandao, na mawasiliano.
Nambiza Tungaraza (Jah Tunga!), tunakusubiri!!!!!!!!! Mapinduzi haya hayatakamilika bila wewe. Kila kitu kimesimama...unasubiriwa!
Soma habari zaidi juu ya kushinda kwa neno "blog" kwa kukongoli hapa na hapa.

0 Maoni Yako:

Post a Comment

Links to this post:

Create a Link

<< Home

FREE hit counter and Internet traffic statistics from freestats.com